Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Huna lolote zaid ya roho mbaya unaona ana faidi sana kukaa hapo.. wanawake asilimia ni mashetani
 
Hongera sana,
 
Kwahyo magu alitenda mkuu[emoji1787]
 
Enzi najitafuta nilienda kupambana mkoa Fulani nyanda za juu kusini, mkoa huo unabaridi sana na ilikuwa mwezi wa 5 kwenda 6.
Basi Kuna mwanangu mmoja ni classmate yeye alisoma akiwa tayari ameajiliwa ( in-service), akanipokea maisha yakaanza. Ghetto alinipeleka kwa mshakaji wake pot alikuwa anaishi mwenyewe ( single) lakini misosi naenda kula nyumbani kwake.

Basi bwana life likaenda week ya kwanza na Mimi natafuta fursa tukazungumza na mshkaji tukaona tutafute mabanda ya kuku tufuge kipindi tunaendelea kujitafuta kama ninachochote chakuanzia basi tuchange.
Tukapiga hesabu ilikuwa inaitajika mil.1 kama kianzio, basi kwakumuamini mwenyeji wangu nitatoa laki 3 nikamwambia tuanze. Asee nilipigwa chenga mwamba nikimuuliza anasema Bado. Muda ukaenda asee mara gafla ya huduma ya chakula kwake ikawa ya kusuasua. Kuna siku nimeenda usiku kula nagonga mlango wapo ndani hawataki kunifungulia. Wakajifanya hawanisikii.

Nikaondoka kwa hasira nikaenda kulala, mwamba akaninawa ugenini Sina ndugu namtegemea yeye, pesa imekata halafu amenidhulumu na Sina Cha kumfanya. Pot nae akapata short course Moshi anatakiwa aende akataka kufunga ghetto lake maana hata mwenyeji wangu na yeye hamuelewe. Nashukuru Mungu kwa muda niliokaa nae jamaa alinikubali sana alikuwa ananiachia Hadi ATM yake nitoe pesa niandae misosi maana nilianza kula kwake Sasa
Ikanibidi niishi kwa akiba yangu ya mwisho iliyobakia huku nikipambana kupata pakujishikiza. Nashukuru tu kipindi pot anataka kwenda Moshi alikuwa Hana nauli kama unavyojua maisha ya mapoti, basi akaniomba nimkopeshe nikampa elfu 30 ikawa hamna namna basi aniachie ghetto mpaka atakaporudi.

Baada msela kuninawa nikaanza kupambana pekeangu, Kuna msela alikuwa manager kwenye NGO moja ya kilimo na Mimi niliomba nafasi humo nikawa nikimkuta nambembeleza anisaidie , ila anasema nafasi Bado. Baada ya kumuomba sana akasema yeye ana bar kama Sina mishe nikajishikize kuwa manager kwenye bar yake, nikakubali maisha ya umanager mchwara yakaanza asee, jamaa alivyosikia nimepata kazi ya bar akawa anakuja anakunywa bia halafu halipi nikiitwa anasema huyu nimemleta Mimi. Akawa ananikwaza sana, mara alete fujo da! Boss akafuatilia jamaa akamwambia yeye ameniajiri vp bila yeye kukubali ananijua nimetoka wapi, nikikimbia na pesa zake atanitoa wapi.
JAMAA AKAOGOPA NIKAFUKUZWA KAZI BILA KUPEWA SABABU.
Ilinibidi nitafute nauli nirudi nyumbani nikajipange upya.

Nashukuru Mungu hayo mapito yamepita kwasasa ninamaisha yangu naishi kwangu na nipo jijini dar es salaam maisha yanasonga. Nashukuru mwanangu kwa yote uliyonifanyia Mungu akulinde na akupe unachostahili.
 
Huu nauita ukuda Pro max [emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]
 
Mimi naishi mjini na nimekuwa nilipokea watu kama wewe kwa muda mrefu. Nilichogundua ni hata mtu umfanyie wema upi.bado wanaongea maneno ya jinsi hawakuthaminiwa. Na kibaya zaidi ni kwamba watu wenyewe wanaoishi kwa watu hawana appreciation hata kidogo. Unakuta wao walikuja kwa ajili ya shida zao na wewe unakuwa kama daraja tu. Kwa maana hiyo hata mimi sikubali mtoto wangu aishi kwa mtu hata kama ni ndugu. Atapitia siku moja kisalimia na ya pili aondoke. Ushauri wangu epuka kuishi kwa watu usije kusimulia mabaya na kusahau mazuri uliyotendewa.
 
Ndugu, unaongea uonekane Mjuba ama namna gani!?

Kiustaarabu kabisa, kama una wageni nyumbani kwako na unafuga mbwa unapaswa kuwataarifu uwepo wa hao wanyama wako, usimwambie mgeni wako kuwa hawana Tabu ilihali hawamjui wala hawajamzoea. Na unataka mbwa wamzoee ili iweje ikiwa ni mgeni na kibaya zaidi choo ni cha nje au unakuta ni nyumba ya kupanga ila mwenye nyumba anafuga mbwa! Think Twice even Thrice aisee
 
Hayo mambo ya mjuba mi hta siyajui! Nilichotaka ni kumfundisha jinsi ya ku survive kwenye mazingira yenye mbwa km alipofikia

Kwa mbwa wetu hawa wa uswahilini siku tatu tu zinatosha kufanya wakuzoee.
 
Sisi undugu yaani ushangazi na ubaba uliisha baada ya Baba yetu kufariki. Toka 2018 hakuna hata mmoja amewahi nipigia simu wala nijulia hali kama mtoto wa kaka yao.

Katika kitu ambacho namshukuru Mungu kwa ajili ya Baba yetu ni kufariki sisi tukiwa watu wazima wenye watoto na tunaojitambua. Katika maombi yangu ya kila siku mbele za Mungu ni anipe uhai na afya njema ili nione wanangu wakijua na kujitambua then anichukue nikapumzike. Duniani kuna shida na changamoto nyingi sana. Eehhh Mungu tusaidie.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Shem alikuwa na wivuu kiufupiii...
 
Kama nakusoma vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…