Uliwahi kusikia story gani kuhusu Said Salim Awadh Bakhresa?

Uliwahi kusikia story gani kuhusu Said Salim Awadh Bakhresa?

Alichonisikitisha ni kuua kiwanda cha mikate ya kibabe ya Siha, watoto wa jana hamjui mikate ya Siha ilikuwaje na ilivyokuwa muhimu kwa wakazi wa jiji hili ukiacha ile ya kiwanda cha Glory(?) kutoka Chang'ombe hawa walikuwa na duka lao karibu kabisa na sanamu la bismin mitaa ya Samora sasa bwana mkubwa katuletea mikate yake ukila utadhani unakula makaratasi,.

Mkuu bongo kwenye sekta ya mikate bado sana tupo nyuma
 
Hamtakaa kuujua ukweli.

Eti kushona Viatu, kuuza Maandazi.....!

Formula ya Utajiri ni 3 tu!
1. Deal chafu ambazo zipo nje ya mfumo wa Kibiashara.
2. Kwepo Kodi.
3. Kipaji, Music, Ngumi, Mpira etc.

Utatoboa!!
Nje ya hapo tutafute tu hela ya Kula.
Ila kweli mkuu,hua nawazavsana nakutafakari kwa ajira yangu hii ya tamisemi kweli???!!!!nadhani dili chafu hua nikiboko ya yote,ila kipaji napo niukweli mtupu.
 
Ila kweli mkuu,hua nawazavsana nakutafakari kwa ajira yangu hii ya tamisemi kweli???!!!!nadhani dili chafu hua nikiboko ya yote,ila kipaji napo niukweli mtupu.
Ni kweli Mkuu, Watu wengi wametoboa kwa Mishe ambazo zipo nje ya Mfumo rasmi wa Biashara!

Ila kwa nje Watasema alianza kuuza Sigara Mtaani, alikua anauza Kahawa, uza Kahawa wewe uone kama utatoboa!

Soon ukipata deals zilizo nje ya Mifumo ya kawaida ya Biashara, utashangaa pesa inakua sio tatizo, then ndo wanaanza kuwekeza kwenye Biashara Rasmi.
 
Hakika mwana wa adamu,mamayangu mzazi aliwahi kuniambia kua mwanangu,kama unandoto zakua tajiri ningumu lazima utashiriki ktk nguvu zagiza tu,ngumu kutoka huko.
 
Namkumbuka huyu mzee Bakhresa 1976 ama 1977 wakati anafanya kazi ya kushona viatu katika fremu ndogo ya duka katika gorofa la mtaa wa Livingston na mtaa wa Uhuru zamani kichwele str.na walikiwa wanakaa sakafuni na wanashona viatu kwa mikono,mwaka huo alienda hijja Mecca,aliporudi aliwaletea mafundi wake saa aina ya seko five,rangi ya gold thamani yake wakati ule shs,250/=.nieleweke shs miambili na shs hamsini tu.mia za Masai mbili na sarafu za shs20 na sarafu ya ahs10/= moja,kipindi cha sikukuu za idd tulikua tunaenda pale anagawa sent 20 kwa watoto maarufu mbuni.kipindi hicho nipo darasa la tatu shule ya msingi mnazi mmoja,kuishi mtaa wa jirani mahiwa na Livingston.akaanza biashara za migahawa restaurant na akaanza kutengeneza ice cream, kiongozi wa mpira Simba sport enzi ya akina Twalib Hilali Thuen Ally,kwa kweli ametoka mbali na mungu ampe umri mrefu,kwani ss tulikua wadogo ss tuneaelekea kwenye 60yrs.
Afadhali ya wewe umeeleza .....na mgahawa wake wa kwanza ulikuwa unaitwa Nawaz aliununua mtu mwingine na pale ulipokuwa ndo kwa sasa amejenga ghorofa kuubwa pale mtaa wa mkunguni,Sikukuu na hiki kimtaa kinachounganisha mkunguni na mafia

Na wengine wameshindwa kujua kuwa Bakhresa hakuwai kupika maandazi ila kulikuwa na bakery moja pale ilala pembeni ya masjid mwinyi inaitwa best taste ndo walikuwa wanapika na kwenda kuyauza pale opposite na Azam center hivyo watu wakahisi ni product ya azam
 
Hakika mwana wa adamu,mamayangu mzazi aliwahi kuniambia kua mwanangu,kama unandoto zakua tajiri ningumu lazima utashiriki ktk nguvu zagiza tu,ngumu kutoka huko.
Ni sahihi, kwenye ulimwengu wa roho, fahari na utajiri wa Dunia hii ni kutoka kwa Shetani!!!

Ndo maana short cut nyingi za kupata Utajiri ni kupitia huko.
 
Wanasema alianza na U'shoe Shiner akaja na mgahawa wa Azam baadae kuna stage n hapa kati nimesahau, lakin after hio akainunua (NMC) National milling company kutok kwa serikali then booom gurudumu ndio hili mnaloliona sahivi.
NMC ina stori yake na serikali walibugi wenyewe wakampa
 
Back
Top Bottom