Uliwahi kusikia story gani kuhusu Said Salim Awadh Bakhresa?

Uliwahi kusikia story gani kuhusu Said Salim Awadh Bakhresa?

Namkumbuka huyu mzee Bakhresa 1976 ama 1977 wakati anafanya kazi ya kushona viatu katika fremu ndogo ya duka katika gorofa la mtaa wa Livingston na mtaa wa Uhuru zamani kichwele str.na walikiwa wanakaa sakafuni na wanashona viatu kwa mikono,mwaka huo alienda hijja Mecca,aliporudi aliwaletea mafundi wake saa aina ya seko five,rangi ya gold thamani yake wakati ule shs,250/=.nieleweke shs miambili na shs hamsini tu.mia za Masai mbili na sarafu za shs20 na sarafu ya ahs10/= moja,kipindi cha sikukuu za idd tulikua tunaenda pale anagawa sent 20 kwa watoto maarufu mbuni.kipindi hicho nipo darasa la tatu shule ya msingi mnazi mmoja,kuishi mtaa wa jirani mahiwa na Livingston.akaanza biashara za migahawa restaurant na akaanza kutengeneza ice cream, kiongozi wa mpira Simba sport enzi ya akina Twalib Hilali Thuen Ally,kwa kweli ametoka mbali na mungu ampe umri mrefu,kwani ss tulikua wadogo ss tuneaelekea kwenye 60yrs.
 
Alichonisikitisha ni kuua kiwanda cha mikate ya kibabe ya Siha, watoto wa jana hamjui mikate ya Siha ilikuwaje na ilivyokuwa muhimu kwa wakazi wa jiji hili ukiacha ile ya kiwanda cha Glory(?) kutoka Chang'ombe hawa walikuwa na duka lao karibu kabisa na sanamu la bismin mitaa ya Samora sasa bwana mkubwa katuletea mikate yake ukila utadhani unakula makaratasi,.
 
Back
Top Bottom