Carleen
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 7,982
- 27,272
Hi guys,
Natumaini mmekuwa na J'pili njema na yenye baraka..!
Nakumbuka miaka ya nyuma ndiyo najifunza funza kupika maskiini, siku hiyo nikaambiwa nipike uji tena wa ulezi bhaana bhaana, nikatoa una madonge kama vichwa vya ndege, nilivyo 'phaller special' eti nikautia kwenye chupa na kujikausha kama vile hakuna kilichotokea.
Yule Mama kumimina tu, akakutana uso kwa uso na muujiza, dadeki, alinimind jamani mpaka machozi yakanilenga, wala hakujali nikaambiwa nikunywe hiyo chupa yote hakuna kumwaga.
Nikaambiwa 'ile takataka unataka kunywesha watu, hebu wewe ndiyo uikunywe', hapo yeye kawa wa moto hatari, nikaanza kunywa huku machozi yanatoka, kitu ni 'kipaaaya' jamani, usiombe unywe liuji lina madonge..! Na unaambiwa hakuna kumwaga mpaka uishe.
Jamani, nilikunywa mpaka mchana, ilikuwa niupige tena jioni, cousin akanionea huruma (alikuwa mkubwa) akaniambia mwaga, me nitamuambia shangazi umeumaliza ndiyo ikawa pona pona yangu, vile ni mtu mzima Mama akaamini.!
Ya pili, hii nilizingua kwenye ubwabwa, kama kawaida Mama anakuambia tu 'unajua nini cha kufanya', ila hiyo by that time napenda ubwabwa hata sikuona shida nikapiga vitu vyangu ambavyo havieleweki, sahii nisingeweza kukula akii, wenyewe wakarudi jikoni, sheria ni ile ile 'ile takataka unataka lisha wenzio, unakula wewe yooote',
Hiyo sikuteseka, kesho nikarudi kutoka shule na crew yangu, tukapasha zetu kwa akili ile muujiza kikaleta maana kidogo tukakifuta chooote.
Ya tatu, hii sasa ni mkubwa kabisa nipo chuo, nimeenda ugenini kwa Ba mdogo, hapo nimewapigisha story wamecheqa mbavu hawana wakajua wako na mtu wa maana, wakawa wanapika zao ugali, mboga mojawapo ikawa tembele, nikawaambia 'hilo tembele nataka mtoto wa kike nikae jikoni niwapikie', nilivyoisema kwa mbwembwe, nikaenda chukua na kanga nikajifunga kiunoni unaweza dhani mtoto wa kitanga anaingia jikoni.
bwaana bwaaaana, naomba tusimame dakika mbili tuhuzunike tafadhali sana, nikawasha gesi, kumbe lile jiko halipunguzi moto, nikaanza kuhaha viungo sijaandaa, jiko lina moto mkali..! nyiieeeeeh'.
'ile kiere-ere yoote ikaisha sahiyo hiyo', nilitoa upande mmoja umerojeka mwingine haueleweki, niliona aibu na masifa nikapunguza, wakawa tu wananichekea ila am sure kimoyo moyo walinisema walaqhi'..! Nilikaa nao siku chache kabla niondoke ila niaminini Mimi sikuwaangusha tena ninyi wanangu.
anyways, I'm thankful sahii siyo kupika tu cha nyumbani ila ninapika mpaka chakula cha biashara sometimes na kila kitu kinaenda sawa bin sawia and am still learning.
Je, Iliwahi tokea ukazingua kwenye mapishi na Ilikuwaje?