Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilijiskia aibu na mbwembwe nilizokuwa nazo zikaisha,Pole Sana kwenye tembele sipati picha aibu yake,,mi sikumbuki kuwahi kuzingua ila kuna siku napika kienyeji(kuloweka)
hakika,Mimi hakuna pishi linalonichenga kupika, sema tu nashukuru maisha niliyopitia yalinifanya kujua kupika pika vitu vingi nikiwa teenager, so hata geto nikiwaga staki kula migahawani huwa naingia mzigoni chap tu shida ni kua chakula cha kupika mwenyewe afu ule hakina mzuka unajikuta umeshiba tu naamuaga kutafuta msela alie free aje tufinye!
Hahahahaha..!Tukio La kwanza Nilipika wali ukaiva kabisa sasa wakati nahesabu dakika niutoe jikoni nikakumbuka sijaweka chumvi yaani hata punje moja....Maza alisafiri nilibaki mzee.nikaenda kumuita shangazi akauweka sawa baada ya hapo nilipigwa BAN na mzee kupika chakula.
Tukio la pili Mimi na dada yangu tulipika ugali kujaribu kama umeivaa tulikuwa tunatupia ugali ukutani ukinasa hujaiva Sasa kila tukitupa unanasa(yani hujaiva ),sister akaniambia kamwangalie Kaka kama anakuja(ili tupike mwengine) nilivyoenda kumuangalia nikamkuta anakuja ,nakaenda kumpa taarifa sister akesema tukajifiche chini ya uvungu wa kitanda.
bro alivyorudi ana njaa katuka jikoni kumepikwa kufunua msosi hakuna na kumbe aliniona wakati na mchungulia alivyo ingia ndani akatuona tumejificha chini ya uvungu sister aliniweka mbele(chambo) bro akaniambia toka chini huko na sister akatoka katuonyesha jikoni na ukutani mmefanya Nini hapa ,tujitetea kwamba tumepika Sasa tukawa tunajaribu kama umeivaa kauliza na ugali uko wapi (tuliutupa ) sister akachezea kofi mm nimejikunyata pembeni bro alimwambia Yani na ukbwa wako huu hujui kupika unaharibu unga si ungeenda kumuomba shangazi akusaidie......
Nilipigwa fimbo tatu yeye ndio alichezea nyingi zaidi
Tukio LA tatu nilivyokuwa chuo ,geto na washkaji nakumbuka ilikuwa mwaka mpya tukasema oya tusipite hivi hivi tukanunua nyama kilo mbili mchele kilo 4 Mimi ndio stelingi jikoni...loooh mboga iliiva Lkn wali he he he ulikuwa hujaiva ,umeungua na umetoka boko boko yaani wahuni walikuwa wananung'unika huku wanakula yaani mwanangu utanulisha wali na mchele..uzuri sisi geto tuliwekeana Sheria kwamba hakuna aliyemuoa mwezie humu ukiona chakula kibaya kale hotelini so kilo nne zote ziliisha
Kabisa, nisije nikapika chapati haina ushirikiano[emoji23]Haha,
Zile za breakfast in bed.?
Mabuje/ mabuja, yaondoe kwa kuanza kukologea uji then uache uchemke kama ni dona lichemke haswaa. Then songaMimi ugali mpaka leo inatokea bahati utoke mzuri kama hujatoka na mabuje basi hauivi
Jamani, umeteseka, ila sahii si umeshaweza sasa..?Hakuna kitu kimenisumbua kupika kama ugali, nakumbuka katika harakati za maisha nilichomoka home nikaenda sehemu nyingine kupambana na maisha, nikatafuta room, kuoa muda bado, kumiliki mtoto wa kike wa kukupikia chenga mazingira mageni pia mambo hayaruhusu.. Nakumbuka nilikua napika ugali unakua ma uji uji hivi naumwaga, narudia mara ya pili, ya tatu bado unatoka vile vile kazi yangu ikawa n kuweka tu sukari naula kama uji na mboga ambazo nakua nimeshazipika tayari. But nipo good..