Uliwahi kuzingua kwenye mapishi, iwe ni mara ya kwanza unapika ama ukiwa mzoefu tayari?

Uliwahi kuzingua kwenye mapishi, iwe ni mara ya kwanza unapika ama ukiwa mzoefu tayari?

Mimi ugali mpaka leo inatokea bahati utoke mzuri kama hujatoka na mabuje basi hauivi
Ugali ukiwa mkubwa vile kuanza kudandia mwiko unasweti mpaka nyonyo inaboaga sana,

Familia unaipikiaje sasa.!?
 
Wakati niko mdogo, wazazi walitoka nyumbani na kuniachia samaki waliokuwa kwenye chungu kwenye mafiga wakichemshwa. Mi katika kumbukumbu zangu, huwa naona baada ya muda fulani huwa wanachukuwa mwiko na kugeuza geuza chakula wakati kinapikwa. Basi nikachukuwa mwiko nikawachanganya changanya kama mboga za majani wale samaki wakawa uji! Waliporudi, walishangaa sana na kusikitika.
Hahaa.
Wakakuta kitu kimerojeka kabisa walaqhi'..!!
 
Mabuje/ mabuja, yaondoe kwa kuanza kukologea uji then uache uchemke kama ni dona lichemke haswaa. Then songa

Ila wakati wa kukologa uji usitoke jikoni mpk uji utengemae.
Naomba kukazia hapo pa dona chef mkuu, akimaliza kusonga, apunguze moto kisha afunikie ili dona liive lisiwe na harufu ya unga.!
 
mkuu hii mambo ni ngumu kidogo, nakumbuka
1. nilitaka kula ndizi zilizochanganywa na nyama. ktk mapishi nikachanganya vyote vikiwa vibichi baada ya muda kilichotokea sikuona ndizi hata moja na nyama bado zikiwa mbichi, nikahisi hapa kuna sinema na chezewa na wazee wa kaz. baadae nilipo kuja kugundua nikajiona bonge la fala.
2. kuna siku nikataka kutengeneza supu ya ng'ombe nika katakata kila kitu nikaweka kwa jiko including nyanya, kilichotokea ni kama mboga ya kulia ugali. Dogo akaniuliza kwani umefanyaje? nilivyomuelekeza akaniambia malizia kupika ugali tule.
3. mwaka huu mwezi wa 9, mtoto wangu wa kiume kapika kitu kinachofanana na pilau, nikamuuliza hii nn? with confidence akajibu pilau!! nikapiga picha nikamtumia mama ake nikamwambia mwanao kasema kapika pilau, nikamuuliza wewe unadhan nn hii? akajibu sijui labda ningekuwepo.
Enjoy your life.
bonus
juz mwanangu mdogo wa kike kanivalisha wigi la mama ake alaf kaniambia baba umependeza.
Naseama enjoy your life as it is tooooo short
 
Wakati niko mdogo, wazazi walitoka nyumbani na kuniachia samaki waliokuwa kwenye chungu kwenye mafiga wakichemshwa. Mi katika kumbukumbu zangu, huwa naona baada ya muda fulani huwa wanachukuwa mwiko na kugeuza geuza chakula wakati kinapikwa. Basi nikachukuwa mwiko nikawachanganya changanya kama mboga za majani wale samaki wakawa uji! Waliporudi, walishangaa sana na kusikitika.
😆😆 Kweli ulizingua mwenyewe bi mkubwa aliniachiaga samaki wa kubanika watoka kutanda (kuvua kwa kutumia chandalua ) wengine akaenda kuwauza , na wengine akaniachia maagizo niwabanike Sasa badala ya kuweka mkaa tu juu ya mfuniko Mimi nikajaza majivu kabao na mkaa...wakati nafunua ningalie wamefikia wapi mfuniko ulikuwa wa moto nikaurusha jivu lote kwenye samaki...Maza alivyorudi akataka kujua imekuaje nikawa Nampa taarifa huku nimekaa mita 100
 
Shukuru tu haiwi mbele ya watu.!!
Ya mbele ya watu mbona kawaida saana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nishawahi kimbia nikawaachia ugali sijui mchele jikoni maana ulikuwa unatawanyika tu[emoji2297]
 
hakika,
Na utamu wa chakula ni kampani, mnajikuta mmeshusha mlima.!
Mimi pamoja na kua ME lakini nilifunzwa na nimejua kupika ugali ulioiva kabisa bila mabonge nikiwa darasa la 4 tu. Tena nilikua napikia familia yetu ya watu 6 sema sometimes kukadilia ndiyo ilikua shughuli siku nyingine ugali unakua mdogo [emoji16] hivyo italazimika ambao hawajashiba wasonge wa kukazia.

Sababu iliyopelekea kujua kupika nikiwa bado mdogo ni malezi niliyoyapata kwa bibi na babu kijijini walikua wazee so walikua anaishi na sisi wajukuu tu make mshua aliniondoaga mjini akihofia kidume ntaharibika na makundi niwe mla dagsativa akaona bora nikasomee primary kijiji, mwanzo nilipata shida sana kuzoea mazingira ila mwishoe nikazoea tu, ila maisha ya kijijini yana raha yake na yanafunza vitu vingi sana ambavyo ni faida ya baadae katika mzunguko wa maisha kwa ujumla.
 
Mabuje/ mabuja, yaondoe kwa kuanza kukologea uji then uache uchemke kama ni dona lichemke haswaa. Then songa

Ila wakati wa kukologa uji usitoke jikoni mpk uji utengemae.
Aisee hakuna upishi wa ugali ulioniachaga mdomo wazi kama huu wa kuanza kukologa uji kwanza, mara ya kwanza niko geto mkoa wa nyanda za juu kusini huko najitegemea mshkaji wangu mmoja hukohuko tu tulitokea kujuana na tulizoeana sana akawa anakuja kwangu mara mosimosi tunapika na kula and vice-versa kwake kwa hakika tuliishi kama marafiki wa utotoni wa kutoka sehemu moja.

Nilkua nashangaa anavyoanza kukologa uji kwanza anakua anaongeza unga tu mpaka unakua ugali vilevile mimi alikua ananishangaa upishi wangu wa kuanza kuchemsha maji then napunguza na kuweka unga na kusonga hapo lazima uive tu..Ki ufupi kila mtu alikua anamshangaa mwenzake upishi wake wa ugali na hata pishi la wali ilkua tofauti kila mmoja!
 
Kwanza kabisa mie napenda kupika . yano raha ya maidha yangu naipata jikoni😂😂😂😂😂
Nilipozingua sasa, siku ya kwanza kujifunza vileja nikaandaa vizuri mpka kuweka kweny oven kuchoma, baada ya muda nkachungulia nakaona vinabonyea nikaona nipunguze moto niswali magharibi nije nitoe, vitu nilivyokuta hapo vimekua kama mkaa vyote vimeungua sasa zile mbwembwe za kuwaambia watu leo nawaandalia vileja zikakata zote.
Mara ya pili kuzingua ilikua kweny chapati. Kiufupi mie fundi wa chapato sasa ktk kuzidisha manjonjo nikawa nimekata yale madonge tayari kwa kuyatia mafuta kishaa baadae nichome chapati, pembeni kukawa na peanut butter, sa siunajua mafuta yake hupenda kujichuja juu nikaona niyatumie ktk kusukumia zile chapati ili nifunge yale madonge, bwana bwan chapat zikawa tayari.mezani sasa chapat mchambuko ila ile harufu ya karanga ikabaki.kweny chapati zikawa haziliki pona yangu nilikua na mtoto mdgo ndo nikasingizia nilikuta amemiminia mafuta ya peanut kwny chapati
 
Siku moja niko home maza akanipa kazi nipike ubwabwa. Ilibidi nimuite mdogo wangu wa kike ana 9yrs akawa ananielekeza jinsi ya kufanya. Siku hiyo nilikoma maana kalikua kananielekeza kananisema na kunicheka
 
Ubwabwa umenisumbua sana enzi hizo.. I mean ule ubwabwa standard kabisa.

Nilikuwa natoa boko' kila nikipika lazima maji yazidi. mpaka nilipoelekezwa kuwa kabla ubwabwa haujakaukia maji usiugeuze geuze sana.

Now natoa vitu fresh.

Heeeey. Hebu nifundishe vyakula vya bsness... Ndio vipi?
Namie nataka kuonja vitu fresh jamani.!!

Vyakula vya kawaida tu ila inakuwa business oriented.! Unapika fresh una-pack na kadhalika, nitakuambia vizuri kule duniani..!
 
Back
Top Bottom