Uliwahi kuzingua kwenye mapishi, iwe ni mara ya kwanza unapika ama ukiwa mzoefu tayari?

Mara ya Kwanza kupika wali nilizingua nilitoa boko kharam moja matata Sana...wakaligonga ivyo ivyo wafanyaje Sasa na jiko walinisusia Mimi.
 
Hahaha..!
Kajisemeaga zake Madame B bora ategue sufuria limwagikie huko kuliko hiyo fedheha.! Sasa sijui nawe ungeigusa bahati mbaya iporomokee.!!
Hahaha naimwagia maji 🤣🤣
Sitaki stress mie , nichekwe ili iweje .
Mimi huwa naomba nisikoseee maana unaumbuka mtu mzima .
Nishatupa keki ,naongea nikiwa na experience 😂
 
Unamwagia maji ukiwa wapi sweetie, wakati cake yenyewe unaikuta iko high table huko..!

Nataka hiyo experience akiii..!
 
Watu tushaunguza mpaka mayai ya kuchemsha nyie mnasema nini [emoji1787][emoji1787]
Nyumba nzima shombo unatamani ubadilishe mpaka mapazia
 
Hahahahaa..
Sijawahi ona mayai yaliyoungua walaqhi'..!!
 
Duuh maisha ya getto haya jana tu mimi nimetoa boko la tambi nimepika tambi boko boko leo ndo nakuja huku nichukue ujuz leo napika tena tambi hadi nijue ila kuharibu pishi roho inauma kinoma yanii
 
tambi ni jepesi zaidi, usitie maji mengi ule urefu wake usikudanganye.! kwa kuongeza ladha unaweza tia tangawizi na kitunguu thomu kwa mbali baada ya kuvitwanga.!

Pia kwa muonekano mzuri waweza kata carrots na hoho kwa pieces ndogo na nzuri hizi unazitia maji yakianza kukaukia, ama njegere zikiwa zimechemshwa tayari.!!

Mkorea mwenzangu Jaby'z
 
Mimi wali ndo sijawahigi kuuweza kabisa,ugali fresh kabisa tena mgumu ule wa kisukuma.
 
Nilikuwa napika sambusa ila kwa kutumia manda za dukani (Azam). Basi siku moja katika kufunga sambusa nyama ikabaki nyingi manda zimeisha nikasema leo natengeneza manda mwenyewe. Nilikuwa sijawahi na sijui kabisa.

Basi nikachukua unga wa ngano nikakanda na kusukuma chapati then nikaikata nikafunga nyama. Wakati wa kupika naona sambusa zinaumuka kama maandazi nashangaa imekuwaje ndio nakuja kujua kwamba chapati inabidi zibabuliwe kabla hazijafungwa nyama.
Mimi nilifunga chapati mbichi. Ikabidi nizifiche sambusa maandazi zangu nile mwenyewe kisirisiri hakujua mtu.
 
Haahahahaa..
Hapo pa kula mwenyewe kisirisiri pamenivunja mbavu walaqhi'..!
 
Back
Top Bottom