Darmian
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 17,289
- 46,624
Sahau kuolewa na Msukuma..Mimi ugali mpaka leo inatokea bahati utoke mzuri kama hujatoka na mabuje basi hauivi
Kidding
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sahau kuolewa na Msukuma..Mimi ugali mpaka leo inatokea bahati utoke mzuri kama hujatoka na mabuje basi hauivi
Mkuu nimecheka hadi basi.Hakuna kitu kimenisumbua kupika kama ugali, nakumbuka katika harakati za maisha nilichomoka home nikaenda sehemu nyingine kupambana na maisha, nikatafuta room, kuoa muda bado, kumiliki mtoto wa kike wa kukupikia chenga mazingira mageni pia mambo hayaruhusu.. Nakumbuka nilikua napika ugali unakua ma uji uji hivi naumwaga, narudia mara ya pili, ya tatu bado unatoka vile vile kazi yangu ikawa n kuweka tu sukari naula kama uji na mboga ambazo nakua nimeshazipika tayari. But nipo good..
Lazima nikupeleke kwa gwajima utoe ushuhuda wa muujiza mzee mwenzangu😂😂Haha..
Ni miujiza tu huwa inatokea, kwa ushua upi mzee mwenzangu.?
Nakubaliana na hoja, mazingira yanachangia kwa % kubwa. Mimi darasa la nne as ME nilimpikia mamdogo ugali ukaiva, siku alipoondoka nyumbani alinipa 200 ya noti kama zawadi. Guess what!! Nilikua don shule for almost 2-3 weeks😅😅.Mazingira ndo yanamtengeneza mpikaji,miaka ya nyuma maskani ilikuwa Kama usipopika huwezi kula hakuna wa kumpikia mtu Sasa usipike ufe njaa,kwa Hali hiyo lazima ujue kupika tu Hadi wanawake wanaona wivu...
Ila hapa tutumie kigezo cha kanda utakayo?!Inatokeaga tu bana,mie mwenyewe hadi leo tembele linanipiga chenga
Haha..!.Msinikumbushe maana naweza lia.
Kulikuwa na 40 ya marehemu somewhere Ilala. Mie nikajifanya kushika jungu la pilau la mchele wa kilo 15....acha tu, uchawi upo jamani.
Kila nikigeuza pilau, ni kama nimeloweka mchele yaani full bichi, pilau limepiga msamba kila kiungo kipo upande wake.
Kuondoa lawama,nikategua jifya moja...jungu chini, pilau likamwagika hapo ndo ikawa pona pona yangu. Maana nikaaga na kuaga.
Sahv, hata unipe majungu ya kilo 100 napika.
Uchawi kwenye mashughuli upo jamani.
kutoka rosti maini mpaka ugali dagaa..?? this world is not fair walaqhi'..!Mwezi uliopita tu hapo nilifanya kituko kwenye kupika wali na rost maini. Wali ulitoka bokoboko flani kabisa ila una ladha nzuri tu (mchele wa Kilosa tena)vitunguu vilisaidia flani kuongeza harufu kwenye hii nilijitetea sababu ya kupikia kwenye jiko la gesi. Kwenye maini sasa nyanya kadhaa na tomato paste niliweka yote wakati yale maini yalikuwa nusu mwenyewe najua leo naua kwa diko adimu doh! hiyo mboga kilichotokea balaa tupu. Lengo ilikuwa kumsaidia wife kupika lakini tamati ilikuwa vyote kumwagwa kisha akapika ugali dagaa tukala. Mpaka leo mzuka wa kukaa kitchen bado haupo hata chai sitaki kuchemsha
Wooow,Sikuwahi kupata shida kubwa kwa. Mapishi maana nilikuwa nacheki kwa mama kupita kawaida licha ya kuwa ni mtoto wa kiume nikicheki kitu anapika nikija pika napita mulemule
Siku moja tu nilipika wali kama kilo 5 hivi haukuiva vzr, alipokuja kutest unakaubichi ka mbali akaongeza maji ukaiva sie tushakula hivyo hivyo na kusepa mishe
Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Napenda aina hii ya maisha hakika..!Mazingira ndo yanamtengeneza mpikaji,miaka ya nyuma maskani ilikuwa Kama usipopika huwezi kula hakuna wa kumpikia mtu Sasa usipike ufe njaa,kwa Hali hiyo lazima ujue kupika tu Hadi wanawake wanaona wivu...
asante sana.Nimekuwa fundi sasaHaha.
Pole, ila baada ya hapo si umekuwa fundi..??
😂😂😂hahahaa.
Bwana Yesu asifiwe kanisa..!
Nimekuja kushuhudia ......!!
Kabisa,wakati mwingine akili huja kivingine ili ujinusuru na waja...maana waja wangepata pa kusemea.Haha..!.
Hapo pa kutegua ili jungu limwagike ni idea nzuri, ninaweza itumia siku moja.. Ahsante sana.!;
Hahhahaa....!Kipindi namaliza form four baba alininunulia simu (Nokia jeneza) basi bwana mtoto wa kike napika huku simu mkononi kila kitu na simu mkononi. Jioni naambiwa songa ugali nachukua unga nakoroga vile naanza kusonga nashangaa mbona ugali haukazi naongeza unga ugali haukazi kuja kushtuka ni unga wa ngano [emoji2][emoji2][emoji2] hapo watu wako mezani wanasubiri.
Alooooooo nilipiga rivasi sio ya nchi hii nikapika ugali fasta uliiva japo kwa kuchelewa.
Ule ugali wa ngano nilitupa baada ya kuhakisha watu wameenda kulala.