Uliwezaje kutengeneza laki mbili kwa siku?

Kabisa mkuu!

Tena hiyo $500 ni ndogo. Ni basi tu watu hawana mitaji ila hakuna biashara inalipa kama forex ukiipatia
Kama ni biashara halali inayolipa kuliko zote nenda bank pitch that idea wakupe hio $10,000
 
Mbona simple sana inategemeana na mtaji uliyowekeza na aina ya biashara unayofanya. Mfano ukifungua saloon ya kisasa yenye mtaji wa milion 15 mpaka 20 hiyo pesa unaipata
 
Magnificent
 
Kabisa mkuu!

Tena hiyo $500 ni ndogo. Ni basi tu watu hawana mitaji ila hakuna biashara inalipa kama forex ukiipatia
Usiaminishe watu mkuu ivyo. Yaani high risk high return.
High profit high loss ndo kanuni mkuu.
Adi muda huu haujaipatia kwani.
Forex ni ngumu practically Ila theoretically ni rahisi.
 
Usiaminishe watu mkuu ivyo. Yaani high risk high return.
High profit high loss ndo kanuni mkuu.
Adi muda huu haujaipatia kwani.
Forex ni ngumu practically Ila theoretically ni rahisi.
Ni kweli mkuu,

Lakini kama ni mtaalamu kwa mtaji huo wa dola elf 10 haitakusumbua. Labda kama utaanza kujilipua kwa malot makubwa makubwa ukitarajia uwe Bakhresa ndani ya mwezi.
 
Lazima tukubaliane kwanza kwamba maisha tunatofautiana ukiwa unawaza utapataje 200k kwa siku kuna mtu anatafuta 1000 la ugali kwa siku.
Ila unaweza fanya haya
1.tafuta skills zinazolipa mfano ufundi bomba, radio simu umeme nk. kisha anzisha ofisi yako mwenyewe.

2.usiishi kwa kujitutumua; kuna watu wakiwa na pesa hata kidogo tu kila atakaye mlilia shida anampa chunga sana siku ukikata ringi watakucheka sana.

3.kama wewe ni me achana na mademu wa nje ikibidi oa hawa watu huwa hawana huruma na pesa ya mwanaume.
4.tafuta real partiner au friend utawajuaje jifanye una shida tu ya pesa au ushauri wasumbue hata mwezi mmoja kama wanakupa ushirikiano mark them they are real kwako ukiona hawapokei simu wala kujibu sms hao ndio makenge achana nai.
5. Jf kila mtu ni milionea au anamiriki biashara ila siyo kweli usije jiona umechelewa.
6. Kama unakaa home kwenu hama nenda mbali kukaa karibu na ndugu ukishaanza kushika vipesa basi kila mtu atakulilia shida hapa huta chomoka.
7. achana na online freelancer, fx siju consultant wa biashara, mapenzi siasa kwa bongo hakika unapoteza muda wako tu.


8. Kuna jamaa yangu ana skills za mobile phone repair huwa anaingiza pesa/ faida zaidi ya 100k per day. Siyo mauzo nasisitiza faida.

9. Kuna watu huwa wanataka kupata skills for free aise jichunge sana yani mtu atoe muda wake for free hapa unahitaji maombi makubwa sana.
10.tz vitu vya kufanya na tukaleta pesa nyingi mifukoni mwetu bado vingi sana sema tumechagua vitu vya short cut tu.
 
Heshima yako mkuu!
 
Mimi mangi ujanidanganya kabiisa yaani nitumbukise hela yangu kwenye limtambo hatafu nitarajie faida sijafanya upuusi huo,nataka niione shilingi yangu inavosunguka kwa kuishika mikononi bado sijaingia cha kike hata kidogo bwansheee.
 
Mlioweza mliwezaje kutengeneza 200,000/= kwa siku moja?
Mwaka 2015-2018 kuna jamaa alikua anahudhuria sana mafunzo, warsha na makongamano! Basi alikua anahakikisha anafoji risiti ya Tax, risiti ya Basi (kama ni mkoani), atalala chumba cha elfu kumi kwa mbinde au kwa mtu, atasaini hata siku ambazo hataweza kuwepo, kwahio anasubiria ile Jumanne mkisha-submit majina na risiti zote yeye muda huo "anaanza" kuuguliwa na kutafuta fursa nyingine kwingine, yaani mwezi mmoja anahudhuria sehemu kama tano mtu mmoja.

Kwahio kila mtu ana namna ya kutengeneza hio laki mbili au zaidi kwa siku, haiko fixed
 
Aisee leo nimeshangaa naambiwa kuna jamaa anatengeneza MILLION KWA SIKU MOJA wakati hiyo ni budget yangu miezi 2

Malengo yangu kwa sasa ni kuweza kutengeneza laki 2 tu kwa siku!Mlioweza mliwezaje kutengeneza 200,000/= kwa siku moja?
Hiyo 2m mimi ni budget yangu ya miezi mitano na kadedree kangu, Dah ,this life is not fair
 
Kabisa mkuu!

Tena hiyo $500 ni ndogo. Ni basi tu watu hawana mitaji ila hakuna biashara inalipa kama forex ukiipatia
Acha kucheza mabonanza yaliyochangamka zalisha huduma tangible things na utabarikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…