Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Heee mbona mnahangaika sana kutafuta wanafunzi
Kutoa taarifa Kwa watu ni muhimu Kuna watu wanahitaji kusoma na Hawana taarifa.
Naona vyuo vya nnje vikijitahidi kutoa taarifa Sana lakini kwa Tanzania ni tofauti.
Ukienda maeneo mengi Hawana taarifa na kutokua Na taarifa sahihi kunaweza kukufanya ukose fursa au ufanye maamuzi yasiyo sahihi.
 
Course nzuri kwa aliesoma PCB advance ni ipi kwa apo OUT
BSC environmental Science
BSC food, nutrition and dietetics
BSC energy resource
BSC Biology
BSC Chemistry
BSC in Physics
BSC ICT
BSC with Education
Etc
 
Nina GPA ya 2.6 Bsc IT. Nimefanya kazi (logistics) miaka mitatu. Je naweza jiunga na OUT kwa ngazi ya masters Logistic?
 
Udahili umeanza, Chuo Kikuu Huria Tanzania na vyuo vingine hapa nchini.

Tuna chuo kimoja hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla kinachotoa elimu wazi na Masafa(Open and distance learning)

Serikali ilianzisha chuo hiki kwa sheria ya bunge namba 17 ya mwaka 1992. Hii ilikua kuwapa fursa wafanyakazi na watu wenye majukumu yanayowafanya washindwe kwenda conventional university, hivyo kujikuta mahitaji yao ya kujiendeleza kielimu yakishindwa kufikiwa.

Kwa mwaka huu wa masomo udahili utakua ni bure.
Ingia tovuti ya chuo www.out.ac.tz na ufanye online application. Unahitaji kuwa na soft copy ya vyeti na picha(passport size moja).

Kwa tuliosoma na kufanikiwa tujitahidi wenzetu pia ambao wanauhitaji, kuwatangazia waweze kuitumia fursa hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nipe utaratibu wa mtu anayehitaji. Kusoma postgraduate hapo open .
Naanza wap na vtu gan vinahtajka nashkuru
 
Open elimu yao ngumu sana. Na ugumu unaletwa na wao wenyewe kujifanya wajuaji. Kama hutaki usumbufu na kurudiarudia mara 100 kusoma convertional university kuliko Chuo Kikuu Huria. Conversion (kama mzumbe au Udom au UDSM) una uhakika wa kusoma degree miaka mitatu na kumaliza chuo na degree yako mkononi, Open unaweza kusoma miaka 7 na ukaambulia patupu( Ninaweza kusema kumaliza open university ni kama bahati) Kati ya wanafunzi 10. 8 wamekata tamaa kabisa na hawana hamu ya kumshawishi au kumshauri mtu kujiunga na chuo kikuu hiki.

Mbovu zaidi inayowakatisha tamaa wanafunzi wake ni kwamba wanasoma kama vipofu na kwa kubahatisha sana.

Toka alipotoka Mkuu wa chuo msaidizi Prof. Mwete. Huyu wa sasa kakiharibu sana chuo.

HAWAJUI kwamba lengo la mwanachuo ni kujifunza, kuelewa na kufafaulu mitihani.


Wanachuo wakifeli haiwasumbui wala haiwapi shida.

Mfumo wa kupima wanafunzi katika mitihani ni wa kikatili sana, mfano mtihani wote wa kumaliza end semester unaweza kutoka katika topic/lecture moja tena inaweza kuwa kipengele kimoja au viwili. tofauti kabisa na vyuo vingine tulivyosoma.

Hawafundishi kitu chochote kwa mfumo wao. Kila kitu unajitafutia mwenyewe.

Maswali katika mitihani yao mpaka uki gooole ndiyo unapata majibu yake. Ni migumu kupindukia.

Open wajirekebishe wanafunzi wanaosoma sasa wamekata tamaa kabisa.

Open ni moja ya vyuo vyenye wanafunzi wengi kabisa labda zaid ya 30,000. lakini idadi imeporomoka kwa kasi sana kutokana na kupandisha gharama zao na karibia zinafanana na vyuo vya kawaida.

Walimu wao ni majeuri kweli!


Open isipo badirika kwa maana ya kumfanya Mwanachuo kupata elimu bora, Ujuzi na kufaulu masomo yao ipo siku watabaki na wanachuo 200.
 
msc finance and accountancy ni shs ngapi kwa kozi
 
Tofauti na oktoba,kuna intake gani nyingine ya masters?
 
Back
Top Bottom