Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Udahili umeanza, Chuo Kikuu Huria Tanzania na vyuo vingine hapa nchini.

Tuna chuo kimoja hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla kinachotoa elimu wazi na Masafa(Open and distance learning)

Serikali ilianzisha chuo hiki kwa sheria ya bunge namba 17 ya mwaka 1992. Hii ilikua kuwapa fursa wafanyakazi na watu wenye majukumu yanayowafanya washindwe kwenda conventional university, hivyo kujikuta mahitaji yao ya kujiendeleza kielimu yakishindwa kufikiwa.

Kwa mwaka huu wa masomo udahili utakua ni bure.
Ingia tovuti ya chuo www.out.ac.tz na ufanye online application. Unahitaji kuwa na soft copy ya vyeti na picha(passport size moja).

Kwa tuliosoma na kufanikiwa tujitahidi wenzetu pia ambao wanauhitaji, kuwatangazia waweze kuitumia fursa hii.

Sent using Jamii Forums mobile app

Habari Mkuu dindilichuma , Naomba kujua:-
1. Ikiwa mtu anataka kusoma PhD hapo OUT entry qualification zipi anatakiwa kuwa nazo?
2. Ada kwa PhD ni shilingi ngapi?
3.Muda wa kozi katika PhD (Maximum) ni miaka mingapi?

Ahsante
 
Wana JF naomba mnisaidie kuhusu ili

Naomba mniambie qualification za kusoma koz hizi
>Business administration
>Procurement and supply
>Procurement and logistics

Na kozi nyingine za biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Open elimu yao ngumu sana. Na ugumu unaletwa na wao wenyewe kujifanya wajuaji. Kama hutaki usumbufu na kurudiarudia mara 100 kusoma convertional university kuliko Chuo Kikuu Huria. Conversion (kama mzumbe au Udom au UDSM) una uhakika wa kusoma degree miaka mitatu na kumaliza chuo na degree yako mkononi, Open unaweza kusoma miaka 7 na ukaambulia patupu( Ninaweza kusema kumaliza open university ni kama bahati) Kati ya wanafunzi 10. 8 wamekata tamaa kabisa na hawana hamu ya kumshawishi au kumshauri mtu kujiunga na chuo kikuu hiki.

Mbovu zaidi inayowakatisha tamaa wanafunzi wake ni kwamba wanasoma kama vipofu na kwa kubahatisha sana.

Toka alipotoka Mkuu wa chuo msaidizi Prof. Mwete. Huyu wa sasa kakiharibu sana chuo.

HAWAJUI kwamba lengo la mwanachuo ni kujifunza, kuelewa na kufafaulu mitihani.

Wanachuo wakifeli haiwasumbui wala haiwapi shida.

Mfumo wa kupima wanafunzi katika mitihani ni wa kikatili sana, mfano mtihani wote wa kumaliza end semester unaweza kutoka katika topic/lecture moja tena inaweza kuwa kipengele kimoja au viwili. tofauti kabisa na vyuo vingine tulivyosoma.

Hawafundishi kitu chochote kwa mfumo wao. Kila kitu unajitafutia mwenyewe.

Maswali katika mitihani yao mpaka uki gooole ndiyo unapata majibu yake. Ni migumu kupindukia.

Open wajirekebishe wanafunzi wanaosoma sasa wamekata tamaa kabisa.

Open ni moja ya vyuo vyenye wanafunzi wengi kabisa labda zaid ya 30,000. lakini idadi imeporomoka kwa kasi sana kutokana na kupandisha gharama zao na karibia zinafanana na vyuo vya kawaida.

Walimu wao ni majeuri kweli!

Open isipo badirika kwa maana ya kumfanya Mwanachuo kupata elimu bora, Ujuzi na kufaulu masomo yao ipo siku watabaki na wanachuo 200.
Kuna shida sehemu inawezekana OUT kuna changamoto lakini nyingi ya changamoto huwa ni kwa mwanafunzi mwenyewe.
Shida inakuja nikwamba kwa OUT Lazima usome hauwezi kupata mtihani au kuonana na mwalimu muongee ufaulu ikiwa Hauna uwezo.

Wanafunzi hawawezi kufaulu wote hata iweje. Tatizo kubwa ni kutokua na commitment na mfumo wa ODL kutoeleweka vizuri na wengi huku dunia ya tatu.

Kwa mtu akiyeserious anamaliza shahada ndani ya Miaka miwili na wapo waliomaliza na kuna wanafunzi wanachelewa kumaliza huo ni uamuzi wa msomaji mwenyewe. Inawezekana uwezo wake kuelewa mambo ni mdogo, hana muda wa kusoma, uwezo wakulipa ada mdogo pia kuuelewa mfumo vizuri wa usomaji.

OUT ipo vizuri Sana kwa tuliosoma na kuwa serious na kumaliza kwa wakati huku shughuli zetu zikiendelea bila Athari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliesoma OFP anaruhusiwa kuomba chuo chotechote??
 
Nipo nachukua public admnistration out ila mpka kuzoea mazingira na mfumo mzima wa kujisomea inachukua muda kidogo bila hvyo unawez jikuta degree unasoma miaka 9

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Open elimu yao ngumu sana. Na ugumu unaletwa na wao wenyewe kujifanya wajuaji. Kama hutaki usumbufu na kurudiarudia mara 100 kusoma convertional university kuliko Chuo Kikuu Huria. Conversion (kama mzumbe au Udom au UDSM) una uhakika wa kusoma degree miaka mitatu na kumaliza chuo na degree yako mkononi, Open unaweza kusoma miaka 7 na ukaambulia patupu( Ninaweza kusema kumaliza open university ni kama bahati) Kati ya wanafunzi 10. 8 wamekata tamaa kabisa na hawana hamu ya kumshawishi au kumshauri mtu kujiunga na chuo kikuu hiki.

Mbovu zaidi inayowakatisha tamaa wanafunzi wake ni kwamba wanasoma kama vipofu na kwa kubahatisha sana.

Toka alipotoka Mkuu wa chuo msaidizi Prof. Mwete. Huyu wa sasa kakiharibu sana chuo.

HAWAJUI kwamba lengo la mwanachuo ni kujifunza, kuelewa na kufafaulu mitihani.

Wanachuo wakifeli haiwasumbui wala haiwapi shida.

Mfumo wa kupima wanafunzi katika mitihani ni wa kikatili sana, mfano mtihani wote wa kumaliza end semester unaweza kutoka katika topic/lecture moja tena inaweza kuwa kipengele kimoja au viwili. tofauti kabisa na vyuo vingine tulivyosoma.

Hawafundishi kitu chochote kwa mfumo wao. Kila kitu unajitafutia mwenyewe.

Maswali katika mitihani yao mpaka uki gooole ndiyo unapata majibu yake. Ni migumu kupindukia.

Open wajirekebishe wanafunzi wanaosoma sasa wamekata tamaa kabisa.

Open ni moja ya vyuo vyenye wanafunzi wengi kabisa labda zaid ya 30,000. lakini idadi imeporomoka kwa kasi sana kutokana na kupandisha gharama zao na karibia zinafanana na vyuo vya kawaida.

Walimu wao ni majeuri kweli!

Open isipo badirika kwa maana ya kumfanya Mwanachuo kupata elimu bora, Ujuzi na kufaulu masomo yao ipo siku watabaki na wanachuo 200.
Mkuu nmepiga LLB hapo miaka mitatu tu.Open pako poa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PHD ni kwa aliyemaliza masters
Gharama payable direct kwa university ni 6,500,000
Time ni 3-5 yrs
Habari Mkuu dindilichuma , Naomba kujua:-
1. Ikiwa mtu anataka kusoma PhD hapo OUT entry qualification zipi anatakiwa kuwa nazo?
2. Ada kwa PhD ni shilingi ngapi?
3.Muda wa kozi katika PhD (Maximum) ni miaka mingapi?

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ODL ni mfumo Mzuri Licha ya changamoto za miundombinu Za dunia ya tatu
IMG-20200313-WA0063.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulipia mitihan ya mwez wa tano ya annual ya OFP mwisho lin????
 
Back
Top Bottom