Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Napata elimu mie! Nitakuwa Goma wakati wa Christmass. Hope tutakula nyama choma pamoja
 
Sidhani kama mjadala umelenga katika kuleta ushabiki wa vita inayoendelea. Mimi si mwuumini wa vita kabisa.Kama ungekuwa huku GOMA ndiyo ungeona madhara ya vita. Hebu fikiria hapo Kariakoo mchana wa saa tano asubuhi mabomu matatu tanatua, nini madhara yake kwa maisha ya watu, mali na akili za watu hao. Huku hayo mambo nimeyashuhudia watu wakifiwa na watoto na ndugu zao, wanapata walemavu na mali zao kuteketea kwa gharama ya POLENI SANA. Hii ni kwa raia, achilia mbali wanajeshi ambao kwa mujibu wa mazingira yao ya kazi, suala la kifo lipo mkononi kwa maana wamejitolea maisha yao kwa mani ya DRC. Asikwambie mtu, maisha ndiyo kila kitu. Msishabikie vita ndugu zangu.

Nafikiri hujajua sababu m23 walihama maeneo yao,katika mapambano yaliyo tokea kibumba walikufa askari wengi wa FRDC pamoja na wasindikizaji wao na kwa sababu hiyo jamaa walikuja na hasira nyingi sana,m23 ikabidi iwapishe lakini unajua inavyo uma kupigwa ukiwa na nguvu halafu unakuja na hasira unamkosa imagine,sasa ndio kubadili mtindo wa mapigano hivi wameamua kua offensive watakua wakishambulia badala ya kungojea kushambuliwa kwani hawa UN wanasilaha kali nafikiri huyo HIDER kama yuko GOMA anaweza kukupa sura ya mapigano kwa kuangalia majeruhi na maiti,vita ni kali sana sio mchezo na watu wanakufa sana.
 
Mbona kuna watu kinawauma sana m23 kushambuliwa,mna interest zipi na wao? ingawaje ni wazi hata wakimalizwa bado matatizo ya congo ni mlima.
 
Bila shaka Wakikimbilia DRC au Uganda najua watanyang'anywa silaha na kurudishwa DRC.

Nikikutazama unamatatizo makuu mawili ni mtu mwenye roho mbaya na tena unawivu hupendi kuona mtu mwingine akiendelea,unamchukia pk anaishi kwa mali zako?
 
Mbona kuna watu kinawauma sana m23 kushambuliwa,mna interest zipi na wao? ingawaje ni wazi hata wakimalizwa bado matatizo ya congo ni mlima.

Na mimi nikuulize mbona kunawatu wanafurahia wakisikia m23 wamepigwa?
 
Nikweli wameombwa ili waje kusaidia kuweka amani kwani wao ni neutral ukilinganisha na tz na SA,kinacho kosekana kongo ni jeshi lililo neutral na pindi likipatikana amani katika kivu itapatikana,lakini wakati wate ukiwa na majeshi yanayo fikiria ku eliminate watu fulani katika agenda yao hakuta kua na amani congo hata ukileta amerika haita wezekana.
hivi... wewe, unataka kusema jeshi la SA, na Tz wana take sides? what about hao Bangladesh Pakistan, na India? na je wajua Agenda ya Angola ni sawa na ya Tz na SA, kwamba serikali ya congo na watu wake waachwe waishi kwa Amani. haya matatizo mengine yanatokana na watu kuambiwa ukweli
 
Umesema Rai Mutomboki umenikumbusha kitu. Nimeambiwa kuwa hiyo inaitwa Raia Mutomboki yaani raia wenye hasira. Sijajua kwanini hawa jamaa wanawashmbulia Watusi siyo Wahutu. Suala hapa ni visasi kaka.


nakubali wahutu waliingia congo na kuanza kuua watusi na inawezekana palikua na revange,na nauliza kwanini makabila mengine ya congo(rai mutomboki) yanapambana na wahutu wa rwanda?.
 
Nadhani mjadala utaaliwe na hoja za msingi na siyo tuhuma au kukashifiana. Tupeane elimu.
Na mimi naungana na wewe Truth Matters kuwa Angola hawezi kuwa neutral, fuatilia ni kwanini aliingia kwenye vita ya kwanza kumwondoa Mobutu, utaambiwa kuwa Maobutu alikuwa anawasaidia RENAMO na mambo mengine. Kaka ukweli kama mnapakana na nchi lazima neutrality inapotea.

huyu dada anaeitwa MUKAMASIMBA anaongea Point za kipuuzi sana, mi sio Mkongo ila inaniuma sana kuona wakongo wanavyofanyiwa halafu yeye eti anakuja kuwatetea hao M23.
 
Na mimi nikuulize mbona kunawatu wanafurahia wakisikia m23 wamepigwa?

wanashangilia kwa sababu m23 ni kikundi kinachomiliki silaha na kuwa tishio kwa serikali halali ya DRC.wanapewa msaada na nchi jirani hivyo ni tisho kubwa sana kwa amani ya eneo la mashariki ya congo,na mpenda amani yoyote lazima ashangilie pale watu wa aina hiyo wanapoadhibiwa na kudhibitiwa,ili amani itawale.kwani m23 wakipigwa kinachokuuma ni nini?
 
let say m23 wanavyokuwa pushed out na kuelekea rwanda au uganda serikali za rwanda huwapokea kwa mitindo gani?maana kama serikali za rwanda zingekuwa haziusiki na m23 ingepaswa waonwe kama wavamizi na watu wabaya ambao pia ni hatari kwa usalama wa rwanda/uganda,je hili likoje?
 
Hebu nikuulize muheshimiwa HIDER,unaweza kuniambia kwanini watusi wanachukiwa congo? na kwanini tz,sa,un na FARDC wanashirikiana na FDLR kupambana na M23 wakati wanajua kwamba hao jamaa ndio waliofanya mauaji ya kuangamiza rwanda? kwamtazamo wako unaona kuwaondoa M23 kutaleta amani congo?.

Mi huwa nakwambiaga ndugu yangu, Mwanaume huwa anakubaligi uhalisia kutokana na ukweli ulokuwepo. Sasa wewe ndugu yangu huna sifa za kuwa mwanaume na kama we ni mwanamke basi utakuwa mwanamke mwenye kuwashwa sana na hutulii kwa Bwana wako. Hivi kama UN unaowasema kuwa wanawasaidia FDLR unadhani mpaka sasa wasingekuwa wamefika kigali? Unaongea pumba mpaka unakera yaani.
 
Hilo lilikuwa wazi baada ya M23 kukataa mazungumzo huko Kampala. Awali baada ya kukalia eneo la Rutchuru, ilikubalika yafanyike majadiriano/mazungumzo ili kuleta amni. Mazungumzo hayo yalianza kuanzia hiyo Apr hadi Nov.Wakati mazungumzo yakiendelea, jamaa wakajitoa na kuchukua mji huu wa GOMA, wakadhulumu, wakaiba, wakaua, wakanyang'anya mali, wakabaka na kufanya lolote lile unaloweza kuliita uovu. (nashukuru wakati huo mimi na familia yangu tulikuwa Bongo kwa mapumziko ya X mass) . Kubwa nasikia waliondoka na shehena ya silaha za FARDC ambazo ndizo wanazitumia sasa. Baada ya kupigwa pressure na jumuiya ya kimataifa waliaondoka Disemba mwishoni siku ya X mas. Baada ya hapo wakawa wanaitishia Serikali hata Jumuiya ya Kimataifa kuwa hawasaini makubaliano na hawawezi kufanywa lolote. Ilikuwa mbaya sana. Hapo ndipo uamuzi wa kuishambulia M23 endapo kama hawatakubali makubaliano tena ulipochukuliwa. Kwa hiyo ajenda ya kuishambulia M23 ilikuwepo na hapa GOMA hawatakiwi kabisa. Kuna watu wamekuwa masikini sana. Magari wanayoyatumia sasa, makontena, mahema, chakaula nk vyote walipora hapa GOMA. KILA KILICHOKUWA KIZURI KILICHUKULIWA NA KUWA MALI YA M23 AU VIONGOZI WAO (NTAGANDA NA MAKENGA).

Watakua neutral wapi bwana hata kabla hawajaenda congo walitangaza kwamba wanaenda kuimaliza M23.
 
mi huwa nakwambiaga ndugu yangu, mwanaume huwa anakubaligi uhalisia kutokana na ukweli ulokuwepo. Sasa wewe ndugu yangu huna sifa za kuwa mwanaume na kama we ni mwanamke basi utakuwa mwanamke mwenye kuwashwa sana na hutulii kwa bwana wako. Hivi kama un unaowasema kuwa wanawasaidia fdlr unadhani mpaka sasa wasingekuwa wamefika kigali? Unaongea pumba mpaka unakera yaani.

kizazi cha lucifer hicho mkuu usijisumbue!
 
wanashangilia kwa sababu m23 ni kikundi kinachomiliki silaha na kuwa tishio kwa serikali halali ya DRC.wanapewa msaada na nchi jirani hivyo ni tisho kubwa sana kwa amani ya eneo la mashariki ya congo,na mpenda amani yoyote lazima ashangilie pale watu wa aina hiyo wanapoadhibiwa na kudhibitiwa,ili amani itawale.kwani m23 wakipigwa kinachokuuma ni nini?

Mkuu, huyu mpuuzi ni bora usingemjibu. Kwani unafikiri hajui basi? Huyu Mtutsi anamtetea sana Bwana wake Kagame, embu ona swali la kijinga alilouliza.
 
Back
Top Bottom