Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

mkubali mkatae lazima mtafanya mazungumzo na chama cha ukombozi cha fldr tu

Hahahahahahaha....chama cha ukombozi. Cha kukukomboa wewe? Utasubiri sana. Utarudi Rwanda kwa pingu tu wakati tunakupeleka kwenye mahakama ya ICTR kujibu mashtaka. Unasikia wewe interahamwe.
 
Mkuu Flash Hider, heshima yako mkuu.

Mimi nimekuta mjadala upo kileleni sasa lakini naomba kuuliza maswali makuu mawili.

Je huu mkataba ambao M23 wanasigana na Serikali ya DRC kwamba uitwe Peace Agreement au Vaguer Agreement kwamba kila mtu anajiona mwamba?

Swali la pili je unafikiri ni kwa vipi kutakuwepo udhibiti kwa baadhi ya waasi ambao kwa sasa wamesambaa nchi nzima baada ya wenzao kusalimu amri kwa maana kwamba bdo pengine wanazo silaha au ndio katika moja ya ubishani kutoka kwenye swali la kwanza?
 
Hivi huyu flash hider naona mmemfanya Kofi Anan! Ametuambia hapa kuwa yeye ana tubishara twake huko goma sasa haya ya kampala atajuaje? Akae dukani halafu afuatilie mambo huko Kampala. Biashara Goma ni madini tu kwa hiyo si ajabu hela zake ndizo zinachochea machafuko huko kwa kununua "blood minerals"
 
Wacha wivu
humu ndani tunachambua mengi tu ambayo bila kuwa na utaalam wa uchambuzi, utalaam wa mada husika na mara nyingi huwa tuko nje kabisa ya mfumo husika lakini bado tunafanya hivyo sasa kwa nini unafanya mchango wa mwenzako siyo kitu ?????
 
Ukweli inaonekana ni umwamba ndani yake. Kumbuka awali M23 walipokuwa imara wao ndiyo walikuwa wanaitishia Serikali na wakati mwingine kukataa kusaini mkataba. Mara kadhaa wamekuwa wakitoka nje na kuacha mazungumzo. Sasa kama vile imegeuka. Serikali imeshinda vita hivyo haioni sababu za msingi za kukaa meza moja na M23. Wanachokifanya ni kutoa matakwa yao ambayo jamaa wapende wasipende serikali inataka lazima wayakubali. Ndiyo maana serikali imekataa hata term agreement kwa madai kuwa agreement huingiwa baina ya pande mbili, sasa M23 haipo tena inabidi iitwe Declaration. Magazeti ya leo yote hapa DRC yamesifu kitendo cha Serikali kukataa kusaini. Wacongoman wengi (wapenda amani) wanaona kuwa kusaini mkataba na M23 (ambao hawapo sasa) haina maana yoyote.

DRC ina zaidi ya vikundi 20 vyenye silaha. Vimesambaa maeneo mbalimbali hasa huku East. Kusambalatishwa kwa M23 logically kutakuwa kumewashtua kwani wao ndo kundi lililokuwa well organised. Sijajua reaction ya hayo makundi mengine ikoje.
 
Siku hizi taarifa zote zipo kwenye mtandao. Mtandao upo wazi kwa yoyote mwenye interest. Nipo wazi na x-mass hii nitakuwa Tanzania MWENGE nyumbani kwangu. Wanaotaka kuwasiliana nami waje tu tudadiriane masuala ya biashara na mgogoro wa DRC na Maziwa makuu kwa ujumla, nitakuja na reference nyingi tu. Sihitaji kusema uongo kwa lolote na haina haja kunitilia wasiwasi.

Usijali ndugu yangu. Mimi nimeamua ku-share ninachofahamu na watanzania wenzangu. Kama kuna lolote si la kweli nipo wazi kukosolewa kwani nami nimejifunza mengi sana kupitia uzi huu. Awali kuna baadhi walidhani mimi nitawalisha pumba lakini bila shaka tumekosoana na kuhabarishana ipasavyo. Nilitegemea kuwepo watu kama hawa wenye mtazamo hasi.

Wacha wivu
humu ndani tunachambua mengi tu ambayo bila kuwa na utaalam wa uchambuzi, utalaam wa mada husika na mara nyingi huwa tuko nje kabisa ya mfumo husika lakini bado tunafanya hivyo sasa kwa nini unafanya mchango wa mwenzako siyo kitu ?????
 
Siku hizi taarifa zote zipo kwenye mtandao. Mtandao upo wazi kwa yoyote mwenye interest. Nipo wazi na x-mass hii nitakuwa Tanzania MWENGE nyumbani kwangu. Wanaotaka kuwasiliana nami waje tu tudadiriane masuala ya biashara na mgogoro wa DRC na Maziwa makuu kwa ujumla, nitakuja na reference nyingi tu. Sihitaji kusema uongo kwa lolote na haina haja kunitilia wasiwasi.

Mwenge sehem gan kiongozi mi nipo pale opposite na TRA njia ya kwenda mwenge primary karibu na uwanja wa mpira
 
Ukweli inaonekana ni umwamba ndani yake. Kumbuka awali M23 walipokuwa imara wao ndiyo walikuwa wanaitishia Serikali na wakati mwingine kukataa kusaini mkataba. Mara kadhaa wamekuwa wakitoka nje na kuacha mazungumzo. Sasa kama vile imegeuka. Serikali imeshinda vita hivyo haioni sababu za msingi za kukaa meza moja na M23. Wanachokifanya ni kutoa matakwa yao ambayo jamaa wapende wasipende serikali inataka lazima wayakubali. Ndiyo maana serikali imekataa hata term agreement kwa madai kuwa agreement huingiwa baina ya pande mbili, sasa M23 haipo tena inabidi iitwe Declaration. Magazeti ya leo yote hapa DRC yamesifu kitendo cha Serikali kukataa kusaini. Wacongoman wengi (wapenda amani) wanaona kuwa kusaini mkataba na M23 (ambao hawapo sasa) haina maana yoyote.

DRC ina zaidi ya vikundi 20 vyenye silaha. Vimesambaa maeneo mbalimbali hasa huku East. Kusambalatishwa kwa M23 logically kutakuwa kumewashtua kwani wao ndo kundi lililokuwa well organised. Sijajua reaction ya hayo makundi mengine ikoje.

Ahsante kwa jibu hilo.

Hata hivyo mimi nafikiri M23 bado itaendelea kuwepo kutokana na baadhi ya wanajeshi wa Uganda kuwasaidia kwa namna fulani hawa M23 na pia hata Serikali ya Rwanda kuhusishwa na kuwasaidia hawa jamaa.

Ninasema hivyo kwasababu kama kweli Uganda nayo inataka kuona vita hivyo vinamalizwa kwa kuwepo na mkataba wa makubaliano baina ya upande wa serikali ya DRC na M23, basi wao (Uganda) wangewakamata waasi wote ambao wamekimbilia Uganda baada ya kuvurumushwa na majeshi ya Congo DRC.

Inasemwa kwamba kamanda wao Sultan Makenga na kundi lake la waasi wapatao kama 1665 hivi wamekimbilia nchini Uganda na ingekuwa vizuri kama wangekamatwa wote na kusubiri kufunguliwa mashtaka ya ukiukaji wa haki za binadamu na sharia zingine za kimataifa.

Pia bado Rwanda ina maswali ya kujibu hata baada ya kumpeleka Bosco Ntaganda kule mahakama kuu ya Kimataifa maana alipokimbilia nchini Rwanda alikuwa na kundio linguine kubwa tu la hao M23 ambao inabidi Rwanda iseme imewachukulia hatua gani mpaka leo.

Ila kama migawanyiko ikiendelea ndani ya M23 ambayo imewatenga Ntaganda na Batenga na kupungua kwa misaada kutoka baadhi ya kambi za kijeshi za Uganda na baadhi ya watu ndani ya serikali ya Rwanda, basi sidhani kama M23 itadumu.
 
it will never happen. We don't negotiate with terrorists.## #THE RWANDAN GOV'T MUST ACCEPT IT'S PEOPLE,IS THE LAND OF THERE ANCESTOR WHENEVER THIS HAPPEN BUT THEY SHOULD REMEMBER ONE DAY THEY WILL COME HOME FORCIBLY,SO NEGOTIATION iS BETTER FOR NOW
 
Any way cha msingi umeeleza vizuri sana...pongezi kwa kutumia muda wako kuelewesha umma wa watanzania..!
 
serekali ya DRC ime mshtukia mpatanishi, wamekata title ya mkataba wa amani. kwamba unawapa hifadhi wahalifu m23[/QUOTnE]

Mimi nilijua wazi hawa wazungu hawawezi kubali congo kua na amani,kwani kutokuwepo kwa amani itasababisha kabila kuendelea kuwahitaji ili wamlinde kwa tishio la kuibuka tena uasi wa M23 na kwahilo watamchota milele na milele.
 
Uganda haiwezi kuwakamata,kwani kuwepo kwao uganda na kuacha mapambano ni deal lililo simamiwa na USA ,sasa hapa kunaelekea kuna mgongano wa interest za france na USA,inabidi tusubiri tuone itakua vipi,to me kama DRC itaendelea na msimamo wake naona vita nyingine itaibuka ndani ya kivu.
 
Siku hizi taarifa zote zipo kwenye mtandao. Mtandao upo wazi kwa yoyote mwenye interest. Nipo wazi na x-mass hii nitakuwa Tanzania MWENGE nyumbani kwangu. Wanaotaka kuwasiliana nami waje tu tudadiriane masuala ya biashara na mgogoro wa DRC na Maziwa makuu kwa ujumla, nitakuja na reference nyingi tu. Sihitaji kusema uongo kwa lolote na haina haja kunitilia wasiwasi.

Bwana Flash Hider, usijiweke wazi sana. usimwamini kila mtu kwenye mtandao huu mpaka uwe na uhakika naye sana. Wapo agents wengi wa PK hapa ambao wanaweza wakakuona sawa na wale wanajeshi wetu waliowapa kichapo hao wabakaji wanaojulikana kama M23.
 
Well said Mkuu, hata mimi nilikuwa nataka kumpa tahadhali hiyo hiyo - kuna jamaa mmoja aliwahi kukuhuliza kwamba wewe ni mfanya biashara gani mwenye uelewa mkubwa kiasi hicho! Nafikiri alitumia term ya kwamba "watakupata au something close 2 that" wewe kama Mtanzania najua una uwezo mkubwa wa ku-cover your tracks, Kivu wamejaa mamluki wa PK na wengine wanajua kuzungumza kiswahili kwa ufasaha mkubwa kuwa mwangalifu/makini nao husi-entertain urafiki husio na kichwa wala miguu, tukija kwenye eneo la mtandao husijibu watu wanao ku-PM au wanao kueleza habari ambazo ni 2 good 2b true which's true - Mungu akulinde mkuu.
 
ahahahhha sindio maana unasikia watanzania wanakufa,je uliisha sikia mu south amekufa? hapo utaelewa sababu,nilikua na shangaa jamaa humu akiuliza sababu gani wanakufa watanzania tu,sasa jibu umelitoa mwenyewe,wa south wao hawako tayari kufa.

Wewe ni mtu wa ajabu. Unafikiri kabla ya kuongea au? TPDF kwenda congo ilikuwa ni kwenda kuleta amani. Nilidhani mtu wa kawaida atafurahia kitendo hiki cha kishujaa cha TPDF kwenda congo kwajili ya amani ya watu wa congo leo unaibeza Mashujaa wetu ?
Unaushabiki wa kagame as if he gives a damn about you? Kwasababu kagame ni mtusi? Au sababu maslahi ya kagame na sio rwanda yameingiliwa?kama kufikiri kwako unatumia ukabila wewe ni mtu duni na mjiinga sana.
And warning you usiongee juu ya TPDF. Someone can find you my friend.
 
Kwa wanaojua Kimombo na kufanya analysisi, soma hapa na tujadiliane. Habari hii kwa urefu ipo katika gazeti la New Times la Rwanda unaweza kuifuatilia zaidi. Kwani walijitoa na kwanini wanataka kurejea tena.
Rwanda is now seeking to rejoin the Economic Community of Central African States (Eccas) after it pulled out of the regional community of 10 Central African states composed of Angola, Burundi, Cameroon, Central African Republic, Chad, Republic of Congo, DRC, Equatorial Guinea, Gabon and Sao Tome & Principe in 2007. Rwandan Ambassador to DRC, Amb Rugira is quoted in the newspaper as explaining that Kigali’s chances of readmission are very high, and that it will be welcomed back to the regional bloc at its next heads of state summit, due to take place early 2014 in N’Djamena. As for Rwanda’s decision of giving up its membership in 2007, the Ambassador explained that, having just joined the EAC, Kigali tried to concentrate on the Eastern African regional bloc.

Mkuu wanajaribu kuingia congo kwa mlango mwingine. Pengine kuna mathaifu huko central maana huku east kimenuka kwa rwanda. Hv ndio nafikirja. Wewe unaonaje
 
Mimi naona kwa nchi yetu ni bora kuwapoteza Kenya, Uganda na Rwanda tukajenga ushirika na Congo nchi tajiri kuliko zote Africa.
 
Back
Top Bottom