1: Zamani enzi za mababu zetu walikuwa wanaokota dhahabu juu ya ardhi kwanini isiwe sasa au madini yaliyopo juu ya ardhi yaliisha na kama yaliisha ilikuwaje wakae juu ya ardhi kipindi hicho?
2:Mafuta ni bidhaa muhimu sana kwa dunia ya sasa ni vipi mafuta hutokea?
3: Nasikia Mchanga wa Madini una tabia ya kuzaliana na baadae kuwa madini je kuna ukweli juu ya hili na kama ni kweli kwanini?
4:Kuna aina ngapi za Madini duniani na ni madini gani ni ghali kuliko yote
5:Je hapa duniani 5:Je hapa duniani kuna (nchi) ukanda ambao hauna madini yeyote yale ?.
6:Je Kuna Mahusiano gani kati ya madini na Miamba?
7: Gesi na Mafuta hutofautiana nini?
8: Kwanini Nchi nyingi za Uarabuni zina Mafuta sana?
9:Kipi kati ya Gesi, Mafuta na Madini kina gharama kubwa katika uzalishaji?.
10:Ni dalili zipi za awali huonekana katika ardhi yenye Madini,Mafuta na Gesi kabla ya utafiti kufanyika(huwa kuna dalili zipi).
11:Naomba kujua hii gasi ya kupikia ina tofauti gani na hii gasi iliyopo hapa Nchini (Mtwara).
12: Mafuta ya Ndege Gari na vyombo vingine huwa yanatofautiana nini?
Mbwana Raphael
nitakujibu katia awamu mbili. sasa nakujibu swali la 1,3,4,5,6.
1: Zamani enzi za mababu zetu walikuwa wanaokota dhahabu juu ya ardhi kwanini isiwe sasa au madini yaliyopo juu ya ardhi yaliisha na kama yaliisha ilikuwaje wakae juu ya ardhi kipindi hicho?
jibu.
Kwanza dhahabu ipo ndani ya miamba na wakati mwingine miamba huwa imejitokeza juu ya aridhi na kisha miamba hiyo imeoza na kusababisha dhahabu iwe imetapakaa aridhini. kutokana na hilo mababu zetu wameokota sana dhahabu na hadi sasa watu wanaendelea kuokota sehemu mbalimbali hapa tanzania. lakini ukweri ni kwamba dhahabu za kuokota ambazo kwa kitalamu tunaita(placer deposit ) zimepungua sana na hivyo kinachohitajika ni kufanya utafiti wa miamba na kuchimba. lakini pia kila unapoona kuadhahabu za kuokota au ziliwahi kuokotwa inamaanisha kunamwamba wa dhahabu karibu umeoza kwa kitaalamu(rock weathering) na kusababisha dhahabu hiyo itapakae hapo. hivyo pia dhahabu zilizotapakaa zinatoa kiashilia kuwa kunamwamba kalibu hapo na ukifanya utafiti unaweza kuupata.
3: Nasikia Mchanga wa Madini una tabia ya kuzaliana na baadae kuwa madini je kuna ukweli juu ya hili na kama ni kweli kwanini?
jibu
siyo kweri. napenda kukujulisha kuwa dhahabu imetapakaa kwa kiwango cha 0.004gram/ton katika dunia. hii inamaana ukikusanya mawe tani 1000 unapata gram 4 za dhahabu. sasa kunamichakato ndani ya dunia ambazo husababisha dhahabu zijilude sehemu dongo ambapo tunaita sehemu hiyo mwamba wa dhahabu.(their several process that cause mobiliazation of gold eg hydrothermal activity, metamorphism,and volcanism). michakato hii ndiyo huweza kukusanya dhahabu kutoka kiwango kidogo na kuiweka sehemu moja ikawa kiwango kingi) mfano wastani wa mwamba wa dhahabu ya GGM NI4gram/ton, tulawaka 12gram/ton. ukienda kwa wachimbaji wadowadogo utasikia lugha za kiloba kimoja kinatoa kiasi gani?. yaweza 2gran/kiloba, 4gram/kiloba. lakini viloba vya mawe ya dhahabu vikitunzwa haiwezi dhahabu kuongezeka.. sasa mchanga wa madini wauwezi kuzaliana ni sawa na kutunza mchele stoo. hauwezi kuongezeka wala kupungua. nimekujibu kwa kutumia aina ya madini ya dhahabu lakini naamanisha madini yote hayawezi kudhaliana kwa kutuzwa.
4:Kuna aina ngapi za Madini duniani na ni madini gani ni ghali kuliko yote.
jibu
kunaaina dhaidi ya 2200 ya madini(mineral) duniani. nitakufafanulia kwa udani kidogo kwa namuna mbili ya kitaaluma na kibiashara.
naanza na ya kitaalamu
madini yamegawanyika katika makudi 8 (mineral classification)
1) native elements mfano gold, platinum, diamondi ect
2) sulfides and sulfosalt mfano cinnabar madini yanayochenjuliwa ili kupata mercury,galena etc
3) oxides and hydroxides mfano spinel, corundum, uranium, hematite, chromate,magnetite etc
4) halides mfano halite (chumvu), Fluorite ect
5) carbonates, nitrates, borates mfano calcite, magnesite, malachite na azurite etc
6) Sulfate, chromates, molybdates na tangestate mfano gypsum,barite, etc
7) Phosphates , arsenates, vanadates mfano phosphates, Apatite etc
8) silicates mfano feldisper, garnet,tanzanite, quartz, clay ect
kwa kigezo cha kibiashara
1) metalic minerals mfano gold(dhahabu), copper(shaba), nickel cte
2) industrial mineral mfano graphite, feldsper, calcite, etc
3) Gemstone mineral mfano Tanzanite, Diamond(alimasi), ruby, Lulu etc.
4) Energy mineral mfano Uranium, makaa ya mawe etc
madini ya bei ya juu sana ni madini yanayotoka katika kundi la gemstone
ambayo hasa yanaongozwa na Diamodi na kufuatiwa na ruby. mfano diamodi kutoka mgodi wa williamson mwadui mwaka 2015 yenye ukubwa wa 23.16carat(4.632gram) iliuzwa usd $10.6million. na hivi karibuni 2017 diamond 59.6 carat(11.92gram) iliuzwa usd$71.2million. kunamengine kama spinel, green garnet etc. lakini pia katika madini ya metallic yanaongozwa na dhahabu ambayo kwa leo inauzwa TSH89000-91000) kwa gram. NA BEI ZA MADINI YA BEI YA CHINI KABISA YANATOKA KWENYE KUNDI LA INDUSRTIAL MINERAL. MFANO KIWANDA KILICHOZIDULIWA HIVI JUZI HAPO MKURANGA KINANUNUA TANI MOJA YA FELDSPAR KWA TSH 80000. INAMAANA UKACHIMBE NA UPEREKE KIWANDANI WEWE MWENYE.
5:Je hapa duniani kuna (nchi) ukanda ambao hauna madini yeyote yale ?. na
jibu
madi yako kila sehemu. ila tofauti ni kwamba madini haya yanaweza kupatikanika tanzania na aina nyingine yakapatikanika ghana na vile vile aina moja ya madini yanaweza kupatikanika nch mbalimbali ila kwa wingi tofauti.etc. mfano mzuri madini yamesambaa sawa sawa na unavyoona katika maswala ya kilimo. mfano zao la pamba ni kanda ya ziwa lakini zao la korosho ni ukanda wa pwani. mahindi tunapata rukwa na ruvuma kwa wingi na kahawa tunapata bukoba na kilimanjaro. ndivyo ilivyo katika madini. hivyo hakuna nchi isiyokuwa na madini bali unaweza sema nchi inaweza kuwa na madini ya aina frani tu na isiwe na mengine. kwa dhaidi ninakutumia picha ili uangalie njisi madini yalivyosambaa duniani kila picha itaonesha madini aina maja na njinsi yalivyosambaa duniani. inamaana kila aina ya madini yanahitaji mazingira mfani ili yajitengeneze. na hivyo mazingira hayo yakiwepo nayo nayatokea.
6:Je Kuna Mahusiano gani kati ya madini na Miamba?
jibu
swali hili pia litasaidia sana uelewa na jibu la No5 .
maana ya neno mwamba(rock) ni muunganiko wa madini(mineral) mbalimbali ndiyo yanafanya yatengeneze mwamba ila pia kuna miamba iliyotengeezwa na dini la aina moja. yaani rock is a combination or composition of different type of mineral but in some cases rock are monomineral.
hii maana yake popote pale uokotapo mwamba au jiwe ujue ni dini hili. hii maana yake dunia(earth) ni mwamba na mchanga ote pamoja udongo wote unaouona ni madini kwani umetokana na kuoza kwa mwamba na mwamba ni muunganiko wa madini. mfano mchanga ni madini tena mchanga tuaojengea nyumba au unaouona ufukweni(beach) ni madini yaitwayo quartz na haya hutumika kutengeneza vioo na asilimia 80 ya vioo au niweke vizuri glass (c hupa za soda, bia etc)ni mchanga kama huo. sasa basi miamba imejipanga aridhini kwa utaratibu flani na diyo maana hata madini yanatokea kwa utaratibu flani kulingana na miamba ilivyokaa. cha msingi hapa utambue kuwa siyo kila dini linahitajika kwa matumizi ya shuguli za binadamu. pia siyo kila dini linathamani sana. nitakuwekea ramani ya tanzania kukuoneya miamba njisi ilivyojipanga. kila baka kwenye ramani ya tanzania ya kijeolojia inaamanisa aina flani ya miamba na kwa uchache kutakuwa na madini hasa utaona madini ya dhahabu, chuma na makaa ya mawe
A
SANTE SANA KWA MASWALI WA URENO KARIBU KWA SWALI LA NYONGEZA KAMA KUNASEHEMU SIJAJIBU KWA USAHIHI AU NIMEKUACHA NA DUKUDUKU.