Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Nimesikiliiza .video ya CAG akieleza kuhusu ushuru wa madini takiribani mara 10.
kaniacha na maswali haya na nikiwa na mashaka mengi kama alichokuwa anaongea anakijua au anakifahamu.
1)kutokulipa ushuru wa usafilishaji wa madini nje ya nchi (tax export and VAT for export of mineral). najiuliza
a) anajua sababu za msingi kwa nini hawalipi?
b) je! sababu nizakibiashara au za kisheria ya mkataba walioingia?
c) anamifano ya nchi zingine hasa zilizoendelea wanafanyaje kwenye eneo hili?

2) kuhusu kutokulipa ushuru wa makampuni ya madini zaidi ya miaka 10.( corparate icome tax)
a) kwa nini hawalipi?
b)je! sheria imewakataza kulipa?
c) je! anamifano ya nchi zilizoendelea kuhusu ushuru wa namna hii njisi unavyotozwa?

3} je! hatupati faida kwenye madini kwa sababu ya ubovu wa mikata yasheria yetu ya madini au kwa sababu ya usimazi na wapiga shesabu wetu wabovu?.

CAG HUWEZI KUSHAURI VIZURI NJAMBO USILOLIJUA

W
AZEE WETU MKAPA NA KIKWETE WASILAUMIWE KWA HAYA HAWANA HATIA KABISA.

mwenye hoja za haya maswali anijibu kama huna kaa silent usubili majibu yangu ndiyo utajua tatizo liko wapi wabongo kuondoka mikono mitupu kwenye madini yetu.
 
Bwana last king

Cements inatengeneza na raw materia kuu tatu
1) Limestone (caco3) haya huchukua takribani 70-80% kwenye cement na haya mawe yanapatikana ukanda wote wa pwani ya tanzania kuanzia Tanga hadi Mtwara na ndiyo maana viwanda vyote vinajengwa ukanda wa pwani kuanzia kilichopo tanga, dar wazo hili, kunakingine kigamboni, mkulanga, lindi na mtwara mawe haya ndiyo yaliyo na rangi ya weupe na ugolo au mawe yanayovujwa kokoto kunduchi haya mawe ndiyo yanayotumia .kiwanda kimoja tu kipo mbali na pwani nacho ni mbeya cement ambacho kinatumia materia yanayoitwa Siderite(Feco3) ambayo yapo kwa wingi sana hapo songwe maji ya moto. na diyo maana kiwanda kimejengwa hapo.
2) Gypsum(Caso4). materia haya yanapatikanika makanya same, singida, dodoma na kilwa maeneo ya mandawa. lakini yanayopatikana mandawa diyo bora kuliko maeneo mengine na hivyo kufanya viwanda vingi vya cement vinanunua gypsum kutoka kilwa.
3) Irone ore (50Fe%) viwanda vingi vinapata kutoka tanga na lindi.

sasa mkuu kwa nini hawatumii mawe mengine?
.

jibu1`
kwamba cement inahitaji chemical composition frani na hivyo inahitaji raw material ambazo zikichanganywa zitaweza kuunda chemical composition hiyo. tofauti na hapo hakuna cement mkuu.
Asante sana mkuu
 
Naomba kujua baadhi ya plants ambazo zinaweza kutumika 4 prospecting mineral deposits! Nikipata na vivid examples za Tanzania ningefurahi zaidi [emoji4]
 
mkuu kujenga huo mtambo ya kurifine natural gas ikatumika majumbani ni gharama sana. Imagine plant za madimba na songosongo kwa kuprocess gas cost ni almost 2.5Trilion wakati cost ya LNG plant zidisha hiyo cost mara 10
Correction mkuu Oil ndo inakua refines, Gas/Natural Gas inachakatwa (Processing).

Natura Gas ni Dry gas (mainly Methane) ambayo inasambazwa kwa pipe kwenda majumbani sio kwenye mitungi na inayowekwa kwenye mitungi ni LPG (Liquefied Petroleum Gas) mainly Propane ambayo Tanzania hatuna hii inapatikana baada ya Oil kuwa refined.
 
Naomba kujua baadhi ya plants ambazo zinaweza kutumika 4 prospecting mineral deposits! Nikipata na vivid examples za Tanzania ningefurahi zaidi [emoji4]

Kimberlite.
naomba kidogo ufafanuzi huu. unaamanisha plants 4-processing mineral deposite au 4 prospecting mineral deposit. vile vile naomba uniambie aina ya madini gani unataka nikufafanulie?. na kama ni prospecting hakuna plant inayohitajika ila methods for prospecting mineral deposit. nakuomba unifafanulie vizuri ili niweze kukujibu.
 
usiwe mbishi natural gas pia inaweza kuwekwa kwenye cylinders na ikatumika majumbani ukiacha hiyo njia ya kutumia pipe kwan huwez peleka pipe kwa kila mtu kutokaba na mpangilio mbovu wa miji yetu. mkuu nafanya kazi kwenye natural gas processing facility (sio hapa bongo) so i know what im sayin
 
Endelea kurefine gas mkuu.

Maana inaonekana hili la gas hulijui vizuri.

Norway wana Miundo mbinu mizuri ila hawaweki natural Gas kwenye mitungi unayofikria ww
 
Endelea kurefine gas mkuu.

Maana inaonekana hili la gas hulijui vizuri.

Norway wana Miundo mbinu mizuri ila hawaweki natural Gas kwenye mitungi unayofikria ww
nakubali kuwa gas ndio inafanyiwa processing na oil huwa refined BUT still CH4 inaweza kuwekwa kwenye cylinders.... ule mradi unaosua sua kusini wa LNG unadhani ni kwa ajili ya nini???? sawa CH4 ni dry gas but you can liquify it na ukaiweka kwenye mitungi
 
Baadhi ya watu husema miamba ya Dhahabu huwa na ulalo wa kutoka mashariki kwenda magaribi ,ikimaanisha nikikuta dhahabu ya mwamba inachimbwa nyuzi tatu kusini mwa ikweta shinyanga na nikienda nyuzi tatu kusini mwa ikweta manyara nitapata pia?
 
Kimberlite.
naomba kidogo ufafanuzi huu. unaamanisha plants 4-processing mineral deposite au 4 prospecting mineral deposit. vile vile naomba uniambie aina ya madini gani unataka nikufafanulie?. na kama ni prospecting hakuna plant inayohitajika ila methods for prospecting mineral deposit. nakuomba unifafanulie vizuri ili niweze kukujibu.
Mkuu sijaelewa wapi hujaelewa swali langu! Labda niulize kwa kiswahili.. nataka kujua mimea (plants) ianayoweza kutumika kusaidia kutambua uwepo wa madini fulani. that is niambie mfano... mmea huu..... unatumika ku prospect presence ya gold labda nk?
 
Mkuu sijaelewa wapi hujaelewa swali langu! Labda niulize kwa kiswahili.. nataka kujua mimea (plants) ianayoweza kutumika kusaidia kutambua uwepo wa madini fulani. that is niambie mfano... mmea huu..... unatumika ku prospect presence ya gold labda nk?
Naomba kujua baadhi ya plants ambazo zinaweza kutumika 4 prospecting mineral deposits! Nikipata na vivid examples za Tanzania ningefurahi zaidi [emoji4]

Kimberlite nimekuelewa.
kwanza ni kweri kwamba mimea hutumika katika utafiti wa madini na hii hutumika kutokana na sababu kuu mbili
1)wingi wa madini eneo fulani unaweza kuingia kwenye sehemu mbalimbali za mmea ulioota hapo kutoka kwenye udongo.(Plant material can be enriched in metals taken up from soils that are enriched in the metals.)
2) wingi wa madini sehemu flani unaasili uoto wa mimea wa pale kutoka na kuwa udongo wake hujaa madini ya namna flani hivyo mimea inayowezakusitahimili udongo wa namna hiyo ndiyo itaota hapo.(Effects of elevated metal concentrations may lead to visible differences in plant characteristics or distribution)
kutokana na sababu hizo mimea hutumika katika utafiti. lakini mimea kutumika katika utafiti haiwi (universal)kwa ujumla kuwa kama mmea flani umetumika kwenye utafiti wa dhahabu Ghana basi na tanzania utatumika. hii husababishwa na hali ya hewa kutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine(climate differrent from one area to another)
kutokana na sababu hii utafiti wa kina wa kila mahala unahitajika kujua mimea inayofaa kutumika katika eneo hili. mkuu niliwahi kufanya tafiti za dhahabu GEITA NA MUSOMA .kiukweri kulikuwa na miti kila kila walipo wachimbaji wadogo wadogo tuliona lakini hatukufatilia kwa kina kufikia maamuzi ya kuwa hiyo miti inaonesha kuwepo kwa dhahabu.

Kimbarlite kwa hapa tanzania sina mifano , bali nitakupa mifano sehemu zingine duniani lakini pia hii ni changamoto kwa tanzania nitajitahidi kufatilia au hata kufanya tafiti baazi ya sehemu nitakazoweza na nitakujuza na kama unafahamu unao waweza kutusaidiapia katika hili.

upload_2017-4-17_20-59-12.png

Bacium Homblei is a copper and Chromium indicator plant in Zambia and DRC.

upload_2017-4-17_21-1-36.png
 
Baadhi ya watu husema miamba ya Dhahabu huwa na ulalo wa kutoka mashariki kwenda magaribi ,ikimaanisha nikikuta dhahabu ya mwamba inachimbwa nyuzi tatu kusini mwa ikweta shinyanga na nikienda nyuzi tatu kusini mwa ikweta manyara nitapata pia?

Hishakiye.
Siyo kweri mkuu.
Tena siyomiamba ya dhahabu yote inaulalo(strike) wa kutoka mashariki kwenda magaribi ulalo wa miamba inategemea na mahala husika mfano ulalo wa mwamba wa dhahabu sehemu nyingi mkoa wa lindi ni kasikazini mashariki(NE) Kwenda kusini magharibi(SW). Pamoja na hayo ulolo wa mwamba unamwazo na mwisho. unaweza kuwa ulalo wake ni 1metre tu na mwingine unaweza kuwa hadi 15000metre. tena napenda nikufahamishe kuwa madini hayanauhusiano na ulalo kabisa ila kila ilipo dhahabu lazima iwe kwenye ulalo flani. hii inamaana kuwa kunasababu mbalimbali kusababisha madini ya dhahabu yatokee ila siyo ulalo.
Unaposema nyuzi tatu kusini mwa ikweta shinyanga na nikienda nyuzi tatu kusini mwa ikweta Manyara utapata pia? siyo kweri na hautapata hata ndani ya shinyanga yenyewe siyo kila ilipo nyuzi tatu utapata dhahabu.

asante kwa swali kama hujaelewa unaweza niuliza tena kwa namuna nyingine.
 
Kimberlite nimekuelewa.
kwanza ni kweri kwamba mimea hutumika katika utafiti wa madini na hii hutumika kutokana na sababu kuu mbili
1)wingi wa madini eneo fulani unaweza kuingia kwenye sehemu mbalimbali za mmea ulioota hapo kutoka kwenye udongo.(Plant material can be enriched in metals taken up from soils that are enriched in the metals.)
2) wingi wa madini sehemu flani unaasili uoto wa mimea wa pale kutoka na kuwa udongo wake hujaa madini ya namna flani hivyo mimea inayowezakusitahimili udongo wa namna hiyo ndiyo itaota hapo.(Effects of elevated metal concentrations may lead to visible differences in plant characteristics or distribution)
kutokana na sababu hizo mimea hutumika katika utafiti. lakini mimea kutumika katika utafiti haiwi (universal)kwa ujumla kuwa kama mmea flani umetumika kwenye utafiti wa dhahabu Ghana basi na tanzania utatumika. hii husababishwa na hali ya hewa kutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine(climate differrent from one area to another)
kutokana na sababu hii utafiti wa kina wa kila mahala unahitajika kujua mimea inayofaa kutumika katika eneo hili. mkuu niliwahi kufanya tafiti za dhahabu GEITA NA MUSOMA .kiukweri kulikuwa na miti kila kila walipo wachimbaji wadogo wadogo tuliona lakini hatukufatilia kwa kina kufikia maamuzi ya kuwa hiyo miti inaonesha kuwepo kwa dhahabu.

Kimbarlite kwa hapa tanzania sina mifano , bali nitakupa mifano sehemu zingine duniani lakini pia hii ni changamoto kwa tanzania nitajitahidi kufatilia au hata kufanya tafiti baazi ya sehemu nitakazoweza na nitakujuza na kama unafahamu unao waweza kutusaidiapia katika hili.

View attachment 497541
Bacium Homblei is a copper and Chromium indicator plant in Zambia and DRC.

View attachment 497544
Shukrani mkuu
 
1.ni vifaa gani vyenye bei nafuu ambavyo mchimbaji mdogo anaweza kuvitumia kugundua madini yaliyopo aridhini? 2.katika machimbo madogo madogo mule ndani ya mashimo kunawakati huwa kunazuka gas hatari ambayo huua na kukausha.je[a]gas hii husababishwa na nn? je kama watalaamu na watafiti hamuoni kuwa geita inapaswa kufanyiwa utafiti wa gesi kutokana na kiashiria hicho?[nipo tayari kuwapeleka ktk eneo husika] 3.katika uchenjuaji wa dhahabu wa wachimbaji wadogo,kemikali ya zebaki/mecury hutumika kukamatisha dhahabu iliyopo katika mchanga ulioragwa karashani.kwa bahati mbaya kemikali hii imeonekana kuwa na madhara ya kiafya na pia kuacha dhahabu nyingi kwenye mcianga.je, hakuna njia nyingine nzuri ya kukamatisha dahabu? 4.OMBI:HUKU GEITA ndani ndani kata ya lwamgasa kunasehemu kunamawe yenye shaba nyingi sana.yaani nyingi kweli kweli.kama kunanamna ningependa kuwakaribisha ktk utafiti wa shaba.ahsanteni.
 
Nimesikiliiza .video ya CAG akieleza kuhusu ushuru wa madini takiribani mara 10.
kaniacha na maswali haya na nikiwa na mashaka mengi kama alichokuwa anaongea anakijua au anakifahamu.
1)kutokulipa ushuru wa usafilishaji wa madini nje ya nchi (tax export and VAT for export of mineral). najiuliza
a) anajua sababu za msingi kwa nini hawalipi?
b) je! sababu nizakibiashara au za kisheria ya mkataba walioingia?
c) anamifano ya nchi zingine hasa zilizoendelea wanafanyaje kwenye eneo hili?

2) kuhusu kutokulipa ushuru wa makampuni ya madini zaidi ya miaka 10.( corparate icome tax)
a) kwa nini hawalipi?
b)je! sheria imewakataza kulipa?
c) je! anamifano ya nchi zilizoendelea kuhusu ushuru wa namna hii njisi unavyotozwa?

3} je! hatupati faida kwenye madini kwa sababu ya ubovu wa mikata yasheria yetu ya madini au kwa sababu ya usimazi na wapiga shesabu wetu wabovu?.

CAG HUWEZI KUSHAURI VIZURI NJAMBO USILOLIJUA

W
AZEE WETU MKAPA NA KIKWETE WASILAUMIWE KWA HAYA HAWANA HATIA KABISA.

mwenye hoja za haya maswali anijibu kama huna kaa silent usubili majibu yangu ndiyo utajua tatizo liko wapi wabongo kuondoka mikono mitupu kwenye madini yetu.

UCHAMBUZI HUU
Ni
taufanya katika vipengele vitatu
1)sheria ya madini ya tanzania inavyoelekeza njisi ya kutoza shuru mbalimbali za madini
2)sheria za madini za baadhi ya nchi zilizoendelea na tunatofautiana nao kinamuna gani
3) nini tufanye ili tuweze kufaidi madini yetu.
Lengo kuu la uchambuzi wangu nikutaka kuelimishana pale nitakapokuwa ninauelewa potofu niweze kuelimishwa nami kwani kunawataaramu wengi kutoka wizara ya nishati na madini pia wapo wakala wetu Tanzania Mineral Audit Agency (TMAA) na dio wanahusika na mambo haya.. Lakini kunajambo huwa linaniuma sana nalo ni kuona wananchi wanalalamiaka, wabunge wanalalamika, mawaziri wanalalamika na Rais wetu sote tunalalamika kuwa tunaibiwa. lakini huwa sioni walalamikaji wakitoa sababu za kitaalamu jinsi tunavyoibiwa.

UCHAMBUZI KIPENGELE 1
1)SHERIA ya madini ya tanzania na inavyoelekeza njisi ya kutoza shuru mbalimbali za madini

TANZANIA MINING ACT 2010

CORPORATE INCOME TAXES (CIT) MINING ROYALTIES AND OTHER MINING TAXES

upload_2017-4-18_7-38-35.png

upload_2017-4-18_7-59-36.png

upload_2017-4-18_7-49-0.png

upload_2017-4-18_7-49-33.png

upload_2017-4-18_7-50-10.png

upload_2017-4-18_7-50-41.png

Kutokana na sheria hii ya 2010
uchambuzi wangu njisi ya mahesabu ya kukokotoa ushuru migodini ni kama ifuatavyo nitaelezea kuhusu madini ya dhahabu.

GROSS GOLD REVENUE(MAPATO GAFI YA DHAHABU
a) hapa tunatoza 4% kama mrahaba(4% royalt) kwa bei ya sokoni ya dhahabu
kilichobaki baada ya mrahaba kukatwa hukatwa garama zifuatazo

b)garama za uendeshaji hutolea na wenye mgodi(oporationing cost) hukatwa 100%
c)garama za ununuzi wa asset au utafiti wa mgodi hadi kuupata hukatwa kwa 100%(ore assets)
d)garama za ulipaji fidia wa ardhi pamoja na uendelezaji (land/ improvents) hukatwa kwa 100%
e)garama za majengo mgodini na nje ya magodi kukatwa kwa 100%
f)garama ya mitambo wa kuchakachua na mitambo(plant and machinery) hukatwa kwa 12.5/25/37.7%
g)garama ya kutengeza matunzio ya marudio(sanate) (tailing liners) hukatwa kwa 100%
h)garama za kazi/ujenzi unaoendela mgodini(work/construction in progress hukatwa kwa 100%

baada ya makato ya kipengele b hadi h kinachobaki ndiyo faida kabula ushuru wa kampuni(profit without corparate income tax)
hiki dicho kinatakiwa kitozwe 30% kama corparate income tax
kile kinachobaki baada makato hayo
ndiyo faida ya kampuni inayochimba madini.

wakuu kipengele cha b,c,d,e,f,g,h, katika utozaji ndicho kama kinasimama mtaji wa mwekezaji(investment capital for mining develompment) na hiki ndicho kinaleta utata sana kwani garama hizi huwa zinahitajika hata miaka kadhaa kuludisha kwa mwekezaji. kutokana na sheria yetu ya madini mwekezaji amepewa ruhusa ya kukata pesa zake zote alizowekeza ili aanze kulipa ushuru.na kihi ndicho kilikuwa kinaelezwa na CAG Kuwa tax allowance anayopewa mwekezaji ni kubwa mno. na kiukweri hata mimi nasema garama hizi nikubwa mno na ndinyo mkataba wa madini ulivyo na diyo upo hivyo na haubadiliki kama alivyosema CAG na hii siyo Tanzania tu hata austial, usa, canada china, chile ect mkataba huu upo hivyo ila tofauti ni kuwa wao garama kama hizo huzigawanya kwa idadi ya miaka ya uhai wa mgodi hivyo wawekezaji hukata kidogodogo hivyo hutoa nafasi ya mapato ya ushuru kupatikanika kila mwaka , kwetu ni tofauti ila inamaana ileile kwani wakikata garama zao zikiisha tutapata ushuru mkubwa sana kwa mwaka. tatizo mbona garama za uwekezaji wao haziishi takribani sasa miaka 15?. CAG NA SERIKALI KABLA YA KULALAMIKA TUNAIBIWA FATILENI HAYA.
1) Oporation cost zao mfatilie kwa makini ninahisi huwa mnaongezewa utumbo hapa tena mwe makini na garama hizi kwa kuwa na monitaring system ili mjilizishe garama hizi daya to day
2)fatilieni uzalishaji wa dhahabu kuanzia tone za mawe zinazochimbwa hadi uchenjuaji wake wanapata kiasi gani day to day (dama kwa dama) hapa napo kunanafasi ya wizi.

kwa mtazamo wangu naona miaka 15 inapita garama zao haziishi kwa sababu tunaibiwa kupitia garama hizi na uzalishaji kudanganywa.

CAG
K
uhusu EXPORT TAX FOR MINERAL
Nimefatilia nchi 22 ikewo, austrial, china, tanzania, ghana usa chile , peru, canada mexico congo, brazil etc
hazina export tax for mineral. kwa kufikri kwangu ni kwasababu ya mahesabu yote ya madini kuanzia mrahaba (royalty) hufanyika kwa bei ya soko la dunia hivyo hakuna faida wanayopata kutokana na export kulinganisha na bei ya mahesabu ya utozaji wa ushuru yanavyofanyika. sasa huwezi kumutoza royalty kwa bei ya soko la dunia tena unaenda kumusubili akulipe ushulu wa export . ila kuna baazi ya nch zimeweka tena kwa kiwango kikubwa kwa ajiri ya kukatisha tamaa wasiende kuuza nje ya nchi ili wawauzie wao kwa bei hiyo hiyo ya soko la dunia. sasa CAG tanzania wakisema watuuzie ili wasisafirishe tutaweza kununua?.

HUU NI UJAMBUZI WANGU NIPO TIARI KUKOSOLEWA ILI NIJIFUNZE ZAIDI

Nitaendeal na sehemu ya 2........................
 
Attachments

  • upload_2017-4-18_7-39-33.png
    upload_2017-4-18_7-39-33.png
    11.7 KB · Views: 131
  • upload_2017-4-18_7-42-1.png
    upload_2017-4-18_7-42-1.png
    44.1 KB · Views: 131
Mkuu unajibu maswal vzur sana, ntafurah ukinisaidia kujibu haya maswal yang machache

1. Gas inayotumika sa hv for domestic use ni nyumba ngap exactly znazotumia?

2. Kwann tangu 2009 walivyoanza mpaka leo haijasambazwa kwa nyumba nyngne nying zaid na kuna mpango gan so far and how is going to be implemented?

3. Pia kuitumia gas for transport kuna mpango gani endelevu (is there a plan to increase CNG filling stations?) na kama haupo ww unashaur nin kifanyike kwa experience yako ili tui-utilize gas yetu zaid?

4. Na kama utaweza kunisaidia kujua kias kinachotumika kwa mwaka kwa ajil ya kuitumia gas for domestic use and transport ntakushukuru sana. (Kila moja kivyake)
 
Back
Top Bottom