Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

nakubali kuwa gas ndio inafanyiwa processing na oil huwa refined BUT still CH4 inaweza kuwekwa kwenye cylinders.... ule mradi unaosua sua kusini wa LNG unadhani ni kwa ajili ya nini???? sawa CH4 ni dry gas but you can liquify it na ukaiweka kwenye mitungi
hiyo ni kweli hakuna ubishi naona unanirudisha shule hapa
 
kuna njia yoyote ya asili ya utafiti wa madini kama dhahabu n.k,?
 
kuna njia yoyote ya asili ya utafiti wa madini kama dhahabu n.k,?
yaaa. zipo. but kitaalamu tuseme hizi zinaitwa njia za kijeolojia na kikemia( uzoefu wa miamba ya madini na utaalamu wa kuangalia sample bila kwenda mabara). yaani. unaenda site ambapo unaona panaudongo ambao unafanana na sehemu zinapopatikana dhahabu. kisha unauchota na kwenda kupiga bangala, chabo au kwa kimobo panning . kama kunazahabu utaziona. ukiziona kwenye udongo huo au mchanga unaweza anza kutafuta sehemu zilikotokea. kama unauzoefu na knowledge ya miamba utafanikiwa kugundua sehemu mwamba zilipo. hii njia nisiseme ya asili bali ni local methodi. na machimbo mengi madogomdogo ya gundulika kwa njia hii. lakini tofauti kubwa wachimbaji wadogo wadogo huwa hawana mission ya kuwa na mikakati ya kutafuta miamba. mala nyingi huwatokea tu na ndiyo maana inabaki kuwa madini ni bahati nasibu.
download.jpg

hii picha inaonyesha njisi ya kutazama sample ya madini bila kwenda mabala.
kwa kifupi ipo njia za local na siyo ya asili. na inahitaji uzoefu na uelewa wa madini hayo. lakini hii njia inamipaka yake kulingana na mtaji unaohitajika kuwekwa hapo. kama ni mtaji mkubwa ha utafiti wake unahitajika uwe mkubwa .

asant kwa swali nafikri nimekujibu sahihi. kama sijakujibu sahihi unaweza niuliza tena.
 
Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    11.5 KB · Views: 113
Una chimba Madini gani na sehemu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
nachimba madini ya dhahaku mkoani lindi. pia niaviwanja vywa jipsum. si hayo tu pia ninaviwanja vya dhahabu geita ambavyo sijaanza kuvifanyia kazi ambako ni nyumbani twetu. pia nilikuwa na chimba gemstoni aina ya malaya garnet huku lindi. na nilikuwa naendesha mladi wangu wa uzalishaji kokoto huku huku lindi. kwa bahati nzuri au mbaya nimeuuza.
nafikri nimekujibu. NB sijawahi kuajiliwa toka nihitimu wala sijawahi kupanga kuomba kazi za kuajili. hivyo sina profile ya kwenye migodi mikubwa.
 
Hongera mkuu! Mm nimemaliza mining hapa udsm. Mpango wangu ni kuanzisha crusher na ball mill nyarugusu geita. Unanishauri vipi katika hilo maana una uzoefu wa kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bentonite nitapata wapi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu French.

download (1).jpg
bent.jpg
download (2).jpg
download (3).jpg

picha za miamba mbali mbali za bentonita
Bentonite naomba nikukumbushe kuwa ni madini yatokanayo na mabadiliko ya mavumbi au macjivu ya volcano endapo italipuka na kutua kwenye maji na hasa maji ya chumvi( sea water). kutokana na halii inaamanisha mara nyingi bentonite inapatikana maeneo ambapo volkano imetokea na ikatua kwenye maji ya chumvi.
kwa tanznia yetu maeno haya ni ya ukanda wa bonde la ufa. hasa la upande wa mashariki. yaani ARUSHA-MOSHI-MANYARA-SINGINDA-KIDOGO NA DODOMA. ukiangalia ukanda huu maji yake ni ya chumvi sana hata maziwa yake kama manyara na natroni.
French
Bentonite inakazi nyingi sana kama kama kufyoza uchafu au langi fulani kutoka sehemu flani, inatumika kwenye petroleum refining as catalysis , kutengeneza plastic na paper etc zipo nyingi sana. but swali lako halijalenga huku.

.Sasa hasa hasa wapi utaipata BENTONITE KATIKA UKANDA HUU?.

French

1. minjingu karibu na ziwa manyara
2.Gelai karibu na ziwa Ntroni
3.Arusha karibu na lake Amboseli
4.Iramba siginda ndani ya bonde lawembere-manonga

mkuu French usitoke mbio kwenda kuanza kuchimba ukapata hasara ukanilaumu bureeeeeeeeee et nimekudanganya. mambo ya madini hatakama ukiambia kuwa ndani ya uwanja wa mpira ule kunamadini. usibebe vifaa ukaanza kuchimba.
unahitaji detail nyingi sana ili kujilizisha mahali exactly yalipo na kina pamoja na kujua ubora wake. kwa kifupi maeneo niliyokutajia huwezi kukosa bentonite.

asante kwa swali kama sijakujibu vizuri unaweza kuniuliza kwa upya tena mkuuu.
 
mkuu French.

View attachment 582689 View attachment 582692 View attachment 582693 View attachment 582694

kwani hii ni tofauti na bentonite clay? alafu kama kuna mtu anauza au ana mgodi aniambie, maana kuna sehem nimepata order. kama yupo ani PM nimpe specification ili tufanye biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mkuu! Mm nimemaliza mining hapa udsm. Mpango wangu ni kuanzisha crusher na ball mill nyarugusu geita. Unanishauri vipi katika hilo maana una uzoefu wa kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
WP_20161205_005.jpg

yaaa. nivizuri sana mimi pia ninaviwanja vya gold hapo nyarugusu na kunamdogo wangu anasoma diploma ya maining kutoka madini insititute dodoma alikuwa hapo akipata mafunzo kwenye mgodi wa sagano wa wachimbaji wadogo wadogo kwa lengo akihitimu tuchape kazi haswa kwa pamoja. but viwanja nilivyonavyo toka nyarugusu bado sijavifanyia kazi kabisa, mipango yangu ni mwaka kesho kurudisha kazi zangu kanda ya ziwa. changamoto iliyopo ni kuwa kutafuta eneo ambalo litakuwa potential na utalifanyia kazi huku likiwa lako hivyo utakuwa unatengeneza asset hata kama ukiwa unapoteza pesa itafika wakati unaweza uza hata eneo lako na ukatafuta jingine. tatizo kwa sasa watu kanda ya ziwa wanakimbilia kusanga na kuuza tail(seneti luga ya kichimbaji). kazi hii huwa aisaidii kwa mhusika kujenga asset. but ukiwa unafanyia kazi eneo lako hata kama unazalisha kidogo kidogo inafaida. mara nyingi mfumo ambao unasumbua huko ni kununua mawe kwa ajili ya kusaga badae uuze tailing. sasa watu wengi wanapoteza pesa kwa kudanganywa kuwa mawe yanakitu but hayana. wengi sana wanaua pesa kwa uongo huu. kama unaeneo lako unaweza azisha shimo lako na unakuwa nataratibu zako mchimbaji akiuza mawe yake shariti yasangwe kwenye ball mill yako na yaachwe hapo kama mali yako. badae unaweza amua kuuza au kuozesha mwenyewe. kazi hii utakuwa unajenga asset zako. na siyo kukimbia kimbia mara huku mara kule. yaani naamanisha ukiwa na ball mill harafu unaenda kuweka sehemu na kununua mawe ili ukusanye seniti risk yake ni kubwa sana ya kupoteza pesa harafu hata asset hutengenezi.
kama utapata eneo lako wakati mwingine kama wewe mtaalamu wa mining unaweza pata wawekezaji na ukadizaini mining shafiti yako vizuri na ukaendesha shuguli zako.
kwa ushauri mkubwa hata kama hauna crusher na ball mill unaweza enda ukaanza kujichanganya ukajifunza na unaweza pata marafiki wenye migodi huko ukapewa kusimamia kwa kuwa unataluma yako na ukatengeneza pesa na badae ukawa ACACIA.
MIMI NAKUMBUKA NILIKUJA ANZA BAADA YA KUHITIMU NILIKUWA 100000 TU. NA NILIISHI mazingira ya wachimbaji wadogo kula na kula huko .NA HADI LEO NIPO NA NINA BALL MIIL YANGU NA PML NYINGI japokuwa kifedha bado sijaimalika. mimi nilichagua huku kwa kuwa kunaina nyingi za madini. sasa my plani kuludi kanda ya ziwa nikiwa na uzoefu na uelewa wa kucheza kila aina ya vulugu na utulivu katika sekta hii.

usikate tamaaaa. no alternative burn the ship ili usifikiri kurudi ulikotoka

asante kwa kuniomba ushauri kama nitakuwa sijakushauli vizuri unaweza omba kwa vingine tena
 
kwani hii ni tofauti na bentonite clay? alafu kama kuna mtu anauza au ana mgodi aniambie, maana kuna sehem nimepata order. kama yupo ani PM nimpe specification ili tufanye biashara

Sent using Jamii Forums mobile app

bentonite ni mtoto wa clay au clay ni mzazi wa bentonite. kwa lugha nzuri bentonite ni jamii ya clay.
kwa kifupi sifahamu mwenye mgodi au mwenye nayo.
download (5).jpg

soko lake vipi?

kama soko lipo la kutosha sema watu watafute fulsa hii. unajua bentonite ni madini ambayo katika mazingila ya kawaida soko lake halipaatikaniki. hivyo madini haya yanahitaji ufatiliaji sana ili uanze kuchimba. i mean siyo kama gemstone au gold unaweza weka mfukoni na kuenda kuuza. bentonite ni industry mineral unahitaji kujaza kwenye gari loli zima na kupeleka sokoni. kwa hiyo mtu hawezi chimba bila kujua ataenda uza wapi. kama soko lipo la uhakika na log term inawezekana watu wakatafuta kwa utulivu na kuanza kuchima.
funguka mkuu kuhusu soko.
 
Wana JR uliza swali lako lolote kuhusu madini, mafuta na gas, kuanzia njisi yanavyojitengeneza ardhini, kufanyiwa utafiti, kuchibwa hadi kuuzwa nawe utajibiwa na mtaalamu wako hapo.

Nipe formation ya dhahabu inakuwaje had I kujitengeneza ardhini, na kwanini dhahabu ya njombe inatofautiana process take ya upatikanaji na ya mbeya,kahama etc.
 
Uliza ujibiwe
Mkuu Mimi swali langu ni hivi kwa mtu ambaye hajui kabisa kuhusu madini je inachukua muda gani kujifunza hayo mambo ya madini na kuanza kufanya hizo kazi?na je anatakiwa awe na mtaji kiasi gani ili aingie porini na kufanya hizo projects Kama unazozifanya wewe(uchimbaji mdogo)?
 
Mkuu asante sana kwa swali lako.

Kwanza kujihusisha na project za madini siyo lazima uyafahamu kwa kitaalamu. Kwa maana hii unatakiwa kujua soko na aina ya madini yanayohitajika. Kwa maana hii unahitaji kuwa na mzoefu au mtaalamu atakayekuongoza katika biashara hii. Wapo wataalamu wa uzoefu na wa kusomea kisha wakapata na uzoefu katika madini hayo. Mkuu wataalamu wakusomea wako katika ngazi za cheti (miezi 3-mwaka1), diploma (miaka 2-3)na degree (miaka 4) na vyuo vipo hapa tanzania na nje ya hapa. Elimu ya madini imegawanyika katika vitengo vitatu
1. Utafiti (exploration)
2. Uchimbaji (mining)
3. Uchenjuaji (processing)

Napenda kukujuza kuna aina za madini zaidi ya 2000, ambayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali (hili ni somo kubwa sana) lakini unaweza chimba aina moja ya madini na ukatajirika.

Pili swala la mtaji
Biashara ya madini ni biashara yenye highest risk sana, ndiyo maana unasikia alienda hana mtaji na karudi na mamilioni na wengine wanaenda na mtaji wanarudi mikono mitupu, hii inatehemea mtaalamu wako au uzoefu wako katika namna ya kuwekeza. Hivyo kama wewe ni mgeni kabisa unahitaji kukaa na mzoefu kisha umwambie unakiasi gani na yeye akueleze kulingana na mtaji wako utawekeza katika namna ngani, ukiona mtaalamu wako amekueleza vizuri then unaamua. Kama wewe ni mgeni ukiingia kichwakichwa utapoteza pesa zako bure.

Madini ni yetu tuyachine yatunufaishe,

Kama unashauku ya kujua zaidi karibu uulize tena mkuu.
 
Nipe formation ya dhahabu inakuwaje had I kujitengeneza ardhini, na kwanini dhahabu ya njombe inatofautiana process take ya upatikanaji na ya mbeya,kahama etc.
Mkuu asante kwa swali lako ila maomba unifafanulie swali lako vizuri.

Kwa maana gold zipo naturally ardhini( in the earth) lakini zipo kwa wastani mdogo sana kiasi kwamba huwezi kwenda sehemu yeyote na kuanza kuchimba, hivyo kuna processes ambanzo huzifanya zijikusanye katika sehemu moja na kuwa kwa wingi hivyo huwa na tija kiuchimu ukizichimba. Sasa kuna processes za aina mbalimbali ambazo huzifanya zijikusanye katika mahara furani. Mojawapo wa njia ni 1. volcano huweza kukusanya zahabu
2. Hydrothermal movement
3. Mmomonyoko wa ardhi ( soil erosion)
Etc

Nahitaji ufafanuzi wa swali lako ,Je unahitaji hizi njia (processes) zinazosababisha dhahabu zijkusanye sehemu moja au swali lako linalenga nini?
Karibu mkuu.
 
Mkuu asante sana kwa swali lako.

Kwanza kujihusisha na project za madini siyo lazima uyafahamu kwa kitaalamu. Kwa maana hii unatakiwa kujua soko na aina ya madini yanayohitajika. Kwa maana hii unahitaji kuwa na mzoefu au mtaalamu atakayekuongoza katika biashara hii. Wapo wataalamu wa uzoefu na wa kusomea kisha wakapata na uzoefu katika madini hayo. Mkuu wataalamu wakusomea wako katika ngazi za cheti (miezi 3-mwaka1), diploma (miaka 2-3)na degree (miaka 4) na vyuo vipo hapa tanzania na nje ya hapa. Elimu ya madini imegawanyika katika vitengo vitatu
1. Utafiti (exploration)
2. Uchimbaji (mining)
3. Uchenjuaji (processing)

Napenda kukujuza kuna aina za madini zaidi ya 2000, ambayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali (hili ni somo kubwa sana) lakini unaweza chimba aina moja ya madini na ukatajirika.

Pili swala la mtaji
Biashara ya madini ni biashara yenye highest risk sana, ndiyo maana unasikia alienda hana mtaji na karudi na mamilioni na wengine wanaenda na mtaji wanarudi mikono mitupu, hii inatehemea mtaalamu wako au uzoefu wako katika namna ya kuwekeza. Hivyo kama wewe ni mgeni kabisa unahitaji kukaa na mzoefu kisha umwambie unakiasi gani na yeye akueleze kulingana na mtaji wako utawekeza katika namna ngani, ukiona mtaalamu wako amekueleza vizuri then unaamua. Kama wewe ni mgeni ukiingia kichwakichwa utapoteza pesa zako bure.

Madini ni yetu tuyachine yatunufaishe,

Kama unashauku ya kujua zaidi karibu uulize tena mkuu.
Mkuu nashukuru sana na nakupongeza kwa kujibu maswali kwa uweledi wa hali juu.
Nimefurah umenieleza ukweli bila ushabiki wa aina yoyote wala kuegemea upande mmoja.
 
Back
Top Bottom