ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,869
- 3,852
- Thread starter
- #21
ASANTE KUSHUKULU MASAWALI YALIYO BAKI NITAKUJIBU NAYO PIA KESHO.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kwa maana hiyo tuendelee kufyeka mapori kwa kuchoma mkaaa,ka Ni kuogopa kujenga mtambo huo Basi gesi hii haina maana kabisa.mkuu kujenga huo mtambo ya kurifine natural gas ikatumika majumbani ni gharama sana. Imagine plant za madimba na songosongo kwa kuprocess gas cost ni almost 2.5Trilion wakati cost ya LNG plant zidisha hiyo cost mara 10
katika utafiti wa dhahabu kuna vigezo vingi vinatumika vya awali. kama vile kunalamani za kijeolojia zinazoonesha wapi utapata madini ya aina gani na ramani hizi hutengenezwa na wajeolojia na kwa tanzania zinatengenezwa na kitego kinachoita geologiacal survey of tanzania zilizopo dodoma(GST). mfano katika leve ya dunia zipo na katika leve ya nchi zipo na kwa mfano katika ramani ya kijeolojia ya tanzania zinaonesha dhahabu zinapatikanika kwa wingi kanda ya ziwa, chunya mbeya, mpanda rukwa na ukifika katika maeneo hayo kunaramani za kilevo ya wilaya na hivyo utakuta kwa mfano wilaya ya geita siyo yote inadhahabu bali kunasehemu tu. kutokana na hayo ukifika unapaswa kutumia tafiti za geophyics, kikemia ambazo hutumika kurahisisha kupunguza aneo la kutafiti. na pia wachimbaji wadogowadogo wanatumika sana kuonesha wapi kunafaa kufanya utafiti. kwawachimbaji wadogowadogo dalili ni kupatikana kwa dhahabu za kuosha kutoka kwenye udongo hii inamaana kunamwamba karibu umesababisha dhahabu isambae kwenye udongo huo huko kanda ya ziwa wanaita sesa maana yake za kuchota mchanga na kuosha kwenye maji na kuziona. pia kwa wazoefu waliochimba siku nyingi wanaijua aina nyingi ya miamba hivyo wakiona tu aina ya miamba hiyo wanakuwa makini kuifatiria.Ni dalili gani za asili zaweza kuonyesha kuwa eneo fulani lina dhahabu? Halafu, je ni kweli kuwa yale maeneo yanayotoka moshi chini baada ya mvua kunyesha huwa yana mafuta au yanaashiria nini?
Nadhani mkuu we umebobea sana kwenye hii fani hongera sana na asante kwa kutu toa ukoko,Nina kiji swali,je ni mawe gani hutumika kutengenezea cement? na ni kwanini yasiwe mawe mengineyo?
Naweza kukujibu kama ifuatavyo
1. Ni vitu gani hasa vinasababisha mafuta kujitengeneza huko chini ya ardhi?
Jibu
Mafuta hutengenezwa kutokana na mkusanyiko wa masalia ya viumbe hai na mimea ambavyo kwa pamoja hufukiwa na mchanga (sediments) kwa kipindi kirefu sana (millions of years) hasa katika maeneo ya mabonde, maziwa, bahari (basin area), mgandamizo na joto linalotokana na kinakirefu cha mchanga kilichofukia masalia ya viumbe na mimea ndicho kinachopelekea kuzalishwa kwa mafuta, gesi na makaa yam mawe (fossil fuels).
2. Na ni kwa nini kuna baadhi ya maeneo mafuta yako kwa wingi sana tofauti na pengine? mfano huko uarabuni toka enzi na enzi uchumi wao ni mafuta tu.
Jibu
Kiwango cha masalia ya viumbe na mimea kinachofukiwa huchagiza kiasi cha mafuta kitachotengenezwa ingawa kiwango kinaweza kikawa sawa lakin kiasi cha oxygeni kikizidi hupelekea decomposition kuwa kubwa na hivyo kuharibu bond ya hydrogen na carbon ambazo ndizo hupelekea mafuta kutengenezwa.
3. ..itatokea hizo reserves ziishe?
Jibu
Hii ni aina ya nishati ambayo hupungua kadiri unavyo izalisha kwaiyo ukianza kuzalisha lazima itafika siku itaisha
4. huku kwetu je kiasi kilichogundulika kinaweza kufikia kiwango walicho nacho?
Jibu
Huku kwetu mafuta bado hayajagunduliwa ingawa serikali kupitia shirika la maendelea Tanzania (TPDC) zinafanya jitihada yakuendelea kutafuta katika maeneo mbalinmbali nchini
Ni Gesi asilia ndio tumefanikiwa kugundua katika maeneo ya mwambao wa pwani na bahari ya hindi ambayo imefikia kiasi cha 57 Trillion Cubic feet (TCF) (data za mwaka 2016 TPDC) hiki kiasi ni sawa na mapipa ya mafuta (equivalent oil amount in barrel) 9,826,499,031, kiasi hiki cha gesi tuliyo nayo ni asilimia 0.86 ya gesi yote ambayo tayali imeshagunduliwa duniani, bado jitihada zakuitafuta zinaendelea.
5. Kuna tofauti ya mafuta yanayopatikana baharini na yale yanayopatikana kwenye maziwa?
Jibu
Katika maana ya utengenezwaji wake unafanana kote baharini (offshore) na nchi kavu (onshore) kote hutenezwa kwa namna moja kama ilivyo elezwa katika jibu la swali la kwanza, kinachoweza kutofautisha reserve moja na nyingine ni viambata vilivyomo katika mafuta (chemical composition of crude oil or gas).
6. Inawezekana kupata mafuta au gas eneo la nchi kavu? mfano pale Ruvu naona kuna shughuli inayoendelea nikaambiwa ni utafiti wa mafuta na gas?
Jibu
Uwezekano upo kama nilivo eleza katika jibu la swali la kwanza kwa mafuta au gesi vinatengenezwa katika maeneo ya mabonde (basin)ambapo uwezekano wa masalia ya viumbe hai na mimea kufukiwa na mchanga (sediments), kwa hiyo Ruvu ni moja ya mabonde (basin) ndo maana uliona tafiti zinaendelea.
7. kuna viashiria gani vinavyoonesha kuwa hapa kuna mafuta na gas?
Jibu
Namna raisi yakujua kama eneo fulan kuna gesi au mafuta, unaweza kuona gas/oil seep hii inamaana mafuta au gesi ambayo imepenya miamba nakutokezea juu ya ardhi pasipo kuchibwa kunabaadhi ya maeneo Tanzania kuna izi seeps Kunasehemu inaitwa wingayongo maeneo ya rufiji na sehemu fulani kule mtwara karibu na mnazibay.
Zipo namna nyingine nyingi zakitaalammu zinazotumika kutafuta mafuta au gesi lakin namna pekee ambayo unaweza kujua kama kweli kuna mafuta au gesi nikuchimba kisima nakufanya upembuzi yakinifu.
Asante kwa kuelewa ,karibu tena.Nashukuru sana sana kwa kutumia muda wako kujibu maswali yangu na kunielimisha.. hakika nimeyasoma mara mbili mbili kuhakikisha naelewa vizuri.. I really would like to commend you.. natamani watu wengine wenye uelewa kwenye maeneo kadha wa kadha wachukue muda wao kutoa nafasi ya kuulizwa maswali na kutujibu hivi... Be blessed
Majibu swali la 21.Ntalitambuaje jiwe lenye dhahabu maana nilikaa geita kila siku naokota mawe ila wenyeji wananiambia bana haya hayana dhahabu ni ulanga tuuu
2.mchakato mzima wa gesi kwa tanzania tumefikia level gani
Jibu swali na 111: Zamani enzi za mababu zetu walikuwa wanaokota dhahabu juu ya ardhi kwanini isiwe sasa au madini yaliyopo juu ya ardhi yaliisha na kama yaliisha ilikuwaje wakae juu ya ardhi kipindi hicho?
2:Mafuta ni bidhaa muhimu sana kwa dunia ya sasa ni vipi mafuta hutokea?
3: Nasikia Mchanga wa Madini una tabia ya kuzaliana na baadae kuwa madini je kuna ukweli juu ya hili na kama ni kweli kwanini?
4:Kuna aina ngapi za Madini duniani na ni madini gani ni ghali kuliko yote.
5:Je hapa duniani kuna (nchi) ukanda ambao hauna madini yeyote yale ?.
6:Je Kuna Mahusiano gani kati ya madini na Miamba?
7: Gesi na Mafuta hutofautiana nini?
8: Kwanini Nchi nyingi za Uarabuni zina Mafuta sana?
9:Kipi kati ya Gesi, Mafuta na Madini kina gharama kubwa katika uzalishaji?.
10:Ni dalili zipi za awali huonekana katika ardhi yenye Madini,Mafuta na Gesi kabla ya utafiti kufanyika(huwa kuna dalili zipi).
11:Naomba kujua hii gasi ya kupikia ina tofauti gani na hii gasi iliyopo hapa Nchini (Mtwara).
12: Mafuta ya Ndege Gari na vyombo vingine huwa yanatofautiana nini?
Check link hii.ni chuo gani duniani naweza kufanya Msc Oil and Gas Accounting, gharama zake na naweza vipi kupata sponsorship ama scholarship?
sio hakili lakini mkuuBwana lazaro
madini ni vitu vya thamani. teacher anapokuambia una madini anamaanisha unahakili . "hakili ni mali"
[emoji120] [emoji120] [emoji120] asantee mkuuMajibu swali la 2
Kuhusu ni wapi tumefikia Juu ya mchakato wa gesi,, nikwamba uzalishaji ulishaanza mapema tangu mwaka 2004 huko songosongo Lindi na mnazi bay mtwara mwaka 2006 ...gas ya songosongo ililifika dsm nakuanza matumizi yakuzalisha umeme pamoja na viwanda vingine. Wakati gas ya mnazi bay mtwara ilianza kutumika kuzalisha umeme unaotumika mikoa ya kusini.
Kuanza mwaka 2012 ndipo ugunduzi mkubwa wa gesi katika kinakirefu cha bahari ulitokea ..nakumekuwa na mfululizo watafiti kuliko pelekea kupata jumla ya gesi yenye ujazo unaofikia 57 trillion cubic feet kwa data za mwaka Jana,, kufuatia ugunduzi huu mkubwa ndipo serikali ikaja nawazo lakujenga bomba kubwa la gesi kutoka mtwara na songosongo kuja dsm kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme ambao tayari pale kinyerezi umeme unazalishwa lakin pia gesi itatumika katika viwanda vingi vitakvyojengwa mwambao mwa bomba hilo lagesi.
Lakin pia kwa kuwa gesi hii ni nyingi sana ,,mpango uliopo sasa nikuuza nchi za nje..upo mpango wakujenga kiwanda cha kubadilisha gesi kwenda kwenye kimiminika (LNG) plant hii itawezesha kusafirisha kwa uraisi zaidi huu mchakato ulisha anza nabila shaka kufika miaka ya 2020-2025 huenda tukaona mradi ukikamilika.
robert gordon nilijaribu kuomba ila ada yao sio kitoto aisee na pia uingereza sipafagilii kabisa ingawa sijawahi kufika.. hakunaga chuo kingine cha hiyo? au hata makampuni yanayosaidia watu kutafuta vyuo na sponsorship kwa malipo kidogo?
Jaribu kuwatumia hawa jamaarobert gordon nilijaribu kuomba ila ada yao sio kitoto aisee na pia uingereza sipafagilii kabisa ingawa sijawahi kufika.. hakunaga chuo kingine cha hiyo? au hata makampuni yanayosaidia watu kutafuta vyuo na sponsorship kwa malipo kidogo?
1.Ntalitambuaje jiwe lenye dhahabu maana nilikaa geita kila siku naokota mawe ila wenyeji wananiambia bana haya hayana dhahabu ni ulanga tuuu
2.mchakato mzima wa gesi kwa tanzania tumefikia level gani