Mkuu asante sana kwa swali lako.
Kwanza kujihusisha na project za madini siyo lazima uyafahamu kwa kitaalamu. Kwa maana hii unatakiwa kujua soko na aina ya madini yanayohitajika. Kwa maana hii unahitaji kuwa na mzoefu au mtaalamu atakayekuongoza katika biashara hii. Wapo wataalamu wa uzoefu na wa kusomea kisha wakapata na uzoefu katika madini hayo. Mkuu wataalamu wakusomea wako katika ngazi za cheti (miezi 3-mwaka1), diploma (miaka 2-3)na degree (miaka 4) na vyuo vipo hapa tanzania na nje ya hapa. Elimu ya madini imegawanyika katika vitengo vitatu
1. Utafiti (exploration)
2. Uchimbaji (mining)
3. Uchenjuaji (processing)
Napenda kukujuza kuna aina za madini zaidi ya 2000, ambayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali (hili ni somo kubwa sana) lakini unaweza chimba aina moja ya madini na ukatajirika.
Pili swala la mtaji
Biashara ya madini ni biashara yenye highest risk sana, ndiyo maana unasikia alienda hana mtaji na karudi na mamilioni na wengine wanaenda na mtaji wanarudi mikono mitupu, hii inatehemea mtaalamu wako au uzoefu wako katika namna ya kuwekeza. Hivyo kama wewe ni mgeni kabisa unahitaji kukaa na mzoefu kisha umwambie unakiasi gani na yeye akueleze kulingana na mtaji wako utawekeza katika namna ngani, ukiona mtaalamu wako amekueleza vizuri then unaamua. Kama wewe ni mgeni ukiingia kichwakichwa utapoteza pesa zako bure.
Madini ni yetu tuyachine yatunufaishe,
Kama unashauku ya kujua zaidi karibu uulize tena mkuu.