Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Bwana nzalendo jibu lako linajibiwa vizuri sana na NATURAL GAS UTILIZATION MASTER PLAN 2016-2045. Hii ni plan ya serikali ya Tanzania itakavyotumia gas. unaweza kuisoma hasa ukurasa wa 15 hadi 31. . ila pia kumbuka gas haifanyiwi utafiti na TPDC. Bali ni makampuni binafisi hupewa vitalu na kufanya utafiti na kulingana na sheria serikali inamiliki 20% na hivyo mipango ya uanzaji wa udhalishaji gas na mafuta inategemea mipango ya mabwana wakubwa wanaomiliki hisa kubwa pia pesa za kuendeleza miladi.
Pipi,.naomba kijitabu basi hata kidogo juu ya hili,tafadhali
 
vp ajira kwa watu wa petroleum geologist na geologist kwa ujumla hpa Tanzania??
Mkuu cheguvala asante kwa swali lako.

Ajira za Petroleum geologist na geologist zinategemea na shuguli za utafiti pamoja na uchimbaji wa madini na mafuta.
Kiukweri kabisa ajira katika sekta hii zimeyumba sana kwa sababu zifuatazo na baadhi ni sababu za kidunia na zingine za hapa Tanzania pekee.

1. Baadhi ya madini, Mafuta na gas yaliporomoka sana bei miaka ya 2013, mfano miradi mingi ya utafiti ya mafuta na gas ilianza kusimama mwaka huo.

(a) Gas na mafuta
Kutokana na takwa la sheria ya mafuta na gas linalazimisha makampuni kusomesha wataalamu wazawa. Kutokana na takwa la sheria hiyo wanafuzi wengi wa masters walipata scholaship kwa garama za makampuni hayo pia course nyingi za mafuta na gas zilianzishwa chuo cha UDOM pamoja na UDSM, haya yote yalifanyika bila kuona mbele kuwa soko la wataalamu hao lishashuka.
Bei ya mafuta ilishuka kutokana na kuvumbuliwa technology mpya uchimbaji wa Oil sand na kuifanya Canada, Venezuela pamoja na marekani kuwa kwenye ramani ya reserve kubwa ya mafuta. Pia mizozo ya waarabu katika cartel yao ya OPEC nayo ni sababu ya kuyumba kwa bei ya mafuta. Hivyo kwa sasa wataalu wa mafuta na gas wengi wapo mtaani na hawajui waitumie wapi hiyo elimu.

(b)kuporomoka bei ya madini
Tukianza na Uranium, Fukushima Tsunami 2011 ilisababisha kuharibika mitaambo ya kufua umeme Japani ambaye ndiye alikuwa mnunuzi mkubwa pamoja na hilo pia mataifa mengi ya ulaya yalianza kutafakari namna nyingine ya kuzalisha umeme tofauti na kutumia Uranium, kabla ya tukio hilo tanzania kulikuwa na miradi mingi ilikuwa inapigiwa kerere sana ambayo ilikuwa imeajiri geologist wengi sana ambayo miradi mingi ilikuwa singinda, dodoma na ruvuma, miladi hiyo yote ilisimama kutokana na soko hivyo wataalamu wengi walirudi mtaani
Mbali na uranium, makaa ya mawe, chuma, gold, nikel etc ziliporomoka bei miaka ya 2013 kwa sababu mbalimbali nazo zilisababisha kampuni nyingi kusimamisha tafiti na migango ya kuchimba mfano kama miradi ya kabanga nikel, namtumbo uranium one na kufanya wataalamu wengi waludi mtaaani.

2. Sheria mpya ya kizalendo ya mwaka 2017 nayo inaonekana ni mwiba kwa makampuni mengi kwa maana inaonesha kampuni nyingi zilikuwa ya kitapeli au sheria ndiyo ngumu kwao kuitekeleza. Hii sheria mpya imesababisha kampuni nyingi kufunga virago na kuwaacha wataalamu mtaani

Kwa ujumla wake soko la wataalamu wa madini na mafuta ni gumu kwa hapa Tanzania na sijui lini litakaa vizuri but kwa ushauri wangu kwa sasa watalaamu ni wengi mtaani hivyo ni bora kujichanganya na small scale ili tutengeneze ajira wenyewe na kukuza industry yetu wenyewe.

Asante kwa swali kama haujanielewa unaeza uriza kivingine tena.
 
mim nilikua nimetazamia hasa maswala ya maji(hydrogeology),lkn kupitia hii mada naweza pata changamoto zakujiajil upande wa madin,mafuta,gas na maji kwa ujumla
asante sana,mim namaliza hio petroleum geology udsm,vp kujiajili na changamoto zake,
 
mim nilikua nimetazamia hasa maswala ya maji(hydrogeology),lkn kupitia hii mada naweza pata changamoto zakujiajil upande wa madin,mafuta,gas na maji kwa ujumla
Madini unajiajiri, fursa zipo za kutosha
 
Back
Top Bottom