ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,869
- 3,852
- Thread starter
- #161
Kama background yako haipo vizuri finacially, unahitaji uvumilivu mkubwa sanaasante sana,mim namaliza hio petroleum geology udsm,vp kujiajili na changamoto zake,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama background yako haipo vizuri finacially, unahitaji uvumilivu mkubwa sanaasante sana,mim namaliza hio petroleum geology udsm,vp kujiajili na changamoto zake,
soko la amethiest lipoje kwa tanzania
Kama background yako haipo vizuri finacially, unahitaji uvumilivu mkubwa sana
Woga wako ndiyo umasikini wakobackground na finacially ndo napokwama asee,mtaji na vifaa ttzo
Sawa pipi,.kwa ajili yako nitafanya😉I am trying to send to you pipi but your PM rejecting, unlock it please for a while pipi.
Mother Confessor
Confessor
Mkuu Ngai Moko asante kwa swali lako nitakujibu kama ifuatavyo.Kiongozi ninaomba kujua juu ya;
1. Njia za kutenganisha Dhahabu na Kopa katika gold leaching cyanidation kwa VAT Leaching.
2. Ni mambo gani husababisha dhahabu kutofautiana purity/ asilimia na ni njia gani zinaweza kutumika kuongeza purity/ asilimia?
2. Katika machimbo madogo huwa kuna utaratibu wa kuosha unga uliotokana na jiwe kusagwa kupitia kwenye gunia ili kukamata dhahabu, kuna dhahabu aina ya mwamba dhahabu yake haiwezi kukamatwa kwenye gunia wanaita dhahabu ya mlenda, je ni njia gani dhahabu hii inaweza kukamatwa kwa wachimbaji wadogo?
ndugu nina madini ya Silicoin nauza je soko lake lipo wapi hapa TZ mim niko mwanzaWoga wako ndiyo umasikini wako
Hapana sijawajua wateja wa haya madini, lakini nitajaribu kuulizia .ndugu nina madini ya Silicoin nauza je soko lake lipo wapi hapa TZ mim niko mwanza
Iko hivi Mkuu,Mkuu Ngai Moko asante kwa swali lako nitakujibu kama ifuatavyo.
1. Njia ya kutenganisha Dhahabu na kopa katika gold leaching cyanidation ni kutumia 50%Natric acidi ambayo inauwezo wa disolve(kuimengenya) copper pekee na siyo dhahabu. Hivyo copper itadisolve kwenye kimiminika cha acid hiyo na baada ya hapo inafyozwa (filter) na kubakiza dhahabu pekee. Baada ya hapo unaendelea na process zingine za kuisafisha dhahabu.
2. Purity katika dhahabu.
(A) Kwanza impurity katika dhahabu ni copper, silver, platinum, iron etc. Kitendo cha kupurify gold kinaitwa gold refining. Refining ndiyo hatua ya usafishaji wa dhahabu hadi kufikia 99.999%. Ni kifaa(mtambo) unaotumika ukisafishwa, mtambo huu unatumia melting and chemical reaction mbalimbali ili kuziondoa impurities hizo. Katika mtambo huo wa refinary plant kuna njia mbalimbali zinazotumika kulingana na mchanganyiko wa impurity hizo, mfano hapa Tanzania ACACIA anafanya refinary ya baadhi ya gold hasa ya north Mara lakini dhahabu ya mgodi ya bulyahnulu inamushinda ndiyo maana anaisafirisha kama makinikia kwa ajiri ya kwenda kufanyia simelting and refinary processes inayoweza kuzitenganisha michanganyiko ya madini yaliyomo. Mitambo hiyo ipo madukani inauzwa lakini inategemea na uchafu uliopo kwenye gold.
(B) Je impurity zinasababishwa na nini?. Mkuu, mashapo ya dhahabu( gold deposit) hujitengeneza kwenye miamba, miamba yote haifanani ndiyo maana mwamba wa dhahabu wa mgodi mmoja na mwingine siyo yote inafanana. Hivyo katika miamba kuna madini mbalimbali na kurigana na namna mashapo yalivyojitengeneza yanasababisha impurity za madini mengine yajichanganye na dhahabu. Hivyo wingi wa impurity unategemea na aina ya madini yaliyopo katika mwamba huo pamoja na namna ya mashapo yalivyojitengeneza. Ndiyo maana kuna dhahabu niza 60%-100%.
3. Namna ya kuchenjua dhahabu ya nyunga (mrenda, vumbi) au fine gold.
Kuna njia mbalimbali za uchenjuaji na moja wapo ya njia za asili ni kutumia magunia kwenye mbao ( sluice box method). Njiaa hii kiukweri haiwezi kukamata dhahabu za nyunga na ndiyo maana marudio (seneti) au tailing zinauzwa kwa watu wanaoenda kuozesha kwa acid ( VAT leaching). Sasa kiukweri njia inayoweza kusaidia wachimbaji wadogo ni kutumia hiyo njia ya VAT leaching ili kuipata. Hata hivyo njia Ya VAT leaching pia haiwezi maliza gold zote na ndiyo maana tailing zinaweza rudiwa mara mbili tatu bado dhahabu zinapatikana. Njia za uchenjuaji zipo nyingi na ni somo pana sana. Lakini kwa mazingira ya wachimbaji wadogo VAT leaching ndiyo njia bora ya kunusuru dhahabu inayoshindwa kukamatishwa na magunia.
Karibu kwa swali jingine kama sijajibu vizuri au sahihi.
Asante kwa swali lako mkuu
MkuuIko hivi Mkuu,
1. Katika vipimo vya mchanga (marudio) huwa kuna matokeo ya vipimo kuonesha madini yaliyopo, mfano yaweza kua hivi;
Au ppm 9.3
Cu ppm 7800
Swali langu ni kwamba, ikiwa natakiwa kuchenjua kwa VAT Leaching je ni njia gani au dawa zipi zinaweza kutumika kuitoa dhahabu katika mchanga walau kwa 80% bila kuvuna kopa na bila kutumia Urea au salfeti ya kopa? Maana matumizi ya Copper sulfate au Ammonium nitrate yanafanyika lakini bado kuna kiasi cha Copper hupita ambapo inapelekea dhahabu isivunwe kwa ufanisi katika udongo, mfano hiyo 9.3 ya Au inaweza kubaki 3.5 baada ya kuchenjuliwa.
Hii imesababisha wanunuzi wengi wa marudio kuogopa kununua marudio yenye wingi wa Copper
2. Kuhusu purity, nimekua nikiona dhahabu inaongezewa asilimia, mfano dhahabu inaweza ikapimwa uzito na purity yake, na bei ya dhahabu hutegemea sana asilimia yake, kuna watu hufanya ujanja wa kuongeza asilimia kwenye dhahabu je hutumia mbinu gani?
Mkuu
1. Kwa sample hio inamana copper nyingi sana kwaio ili kutumia cyanide inabidi upunguze kiasi icho bila ivo cyanide italika sana na utavuna copa nyingi badala ya gold.
Kwahiyo labla utafute njia mbadala za kuondoa copper kabla ya cynidation.
Ni testwork tu (metallurgical test) ndo itakupa ipi njia nzuri zaidi ya kuondoa copper.
Mana hata iyo copper kuna aina mbalimbali za copper katika mwamba yaani free au primary, secondary na complex copper, kwa hiyo treatment zake zinakua tofauti kulingana na aina ya kopper.
Mkuu mara nyingi waozeshaji wanafanya kazi kimazoea, hivyo hawafanyi tafiti ili wapate majibu. Kama unamarudio yanasumbua copper basi fanya metallurgical testing. Ndiyo maana acicia wanasafirisha sababu ni hiyo njia za kawaida walishindwa.
2. Kuna njia tatu za kuongeza purity ya gold. Eletrorefining, smelting na acidification. Mara nyingi wachimbaji wadogo huwa wanatumbukiza kwenye asidi ambayo hutafuna uchafu mwingine na haina reaction na gold hivyo husababisha purity iongezeke. Wachimbaji wengi hasa makota hutumia acidi hata kusibitisha kama kweri ni gold na diyo hiyo inasaidia kuongeza purity.
Kama sijakujibu vizuri unaweza uliza tena mkuu minamna nyingine
kaka uko vzr...! ntahitaji msaada wako dec..
Natamani nifanye hii biashara ya dhahabu kama mfanya biashara mdogo mwenye mtaji wa million tatu ila sina ABC kuhusiana na biashara hii ya dhahabu mkuuMaswali yanasubiliwa, karibuni muulize mjibiwe
Natamani nifanye hii biashara ya dhahabu kama mfanya biashara mdogo mwenye mtaji wa million tatu ila sina ABC kuhusiana na biashara hii ya dhahabu mkuu
Naomba msaada wako wa kimawazo na ushauri ji ya kipi nifanye kwa mtaji wangu huu wa million tatu ili niweze kutimiza azma yangu hii