Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

View attachment 582707

yaaa. nivizuri sana mimi pia ninaviwanja vya gold hapo nyarugusu na kunamdogo wangu anasoma diploma ya maining kutoka madini insititute dodoma alikuwa hapo akipata mafunzo kwenye mgodi wa sagano wa wachimbaji wadogo wadogo kwa lengo akihitimu tuchape kazi haswa kwa pamoja. but viwanja nilivyonavyo toka nyarugusu bado sijavifanyia kazi kabisa, mipango yangu ni mwaka kesho kurudisha kazi zangu kanda ya ziwa. changamoto iliyopo ni kuwa kutafuta eneo ambalo litakuwa potential na utalifanyia kazi huku likiwa lako hivyo utakuwa unatengeneza asset hata kama ukiwa unapoteza pesa itafika wakati unaweza uza hata eneo lako na ukatafuta jingine. tatizo kwa sasa watu kanda ya ziwa wanakimbilia kusanga na kuuza tail(seneti luga ya kichimbaji). kazi hii huwa aisaidii kwa mhusika kujenga asset. but ukiwa unafanyia kazi eneo lako hata kama unazalisha kidogo kidogo inafaida. mara nyingi mfumo ambao unasumbua huko ni kununua mawe kwa ajili ya kusaga badae uuze tailing. sasa watu wengi wanapoteza pesa kwa kudanganywa kuwa mawe yanakitu but hayana. wengi sana wanaua pesa kwa uongo huu. kama unaeneo lako unaweza azisha shimo lako na unakuwa nataratibu zako mchimbaji akiuza mawe yake shariti yasangwe kwenye ball mill yako na yaachwe hapo kama mali yako. badae unaweza amua kuuza au kuozesha mwenyewe. kazi hii utakuwa unajenga asset zako. na siyo kukimbia kimbia mara huku mara kule. yaani naamanisha ukiwa na ball mill harafu unaenda kuweka sehemu na kununua mawe ili ukusanye seniti risk yake ni kubwa sana ya kupoteza pesa harafu hata asset hutengenezi.
kama utapata eneo lako wakati mwingine kama wewe mtaalamu wa mining unaweza pata wawekezaji na ukadizaini mining shafiti yako vizuri na ukaendesha shuguli zako.
kwa ushauri mkubwa hata kama hauna crusher na ball mill unaweza enda ukaanza kujichanganya ukajifunza na unaweza pata marafiki wenye migodi huko ukapewa kusimamia kwa kuwa unataluma yako na ukatengeneza pesa na badae ukawa ACACIA.
MIMI NAKUMBUKA NILIKUJA ANZA BAADA YA KUHITIMU NILIKUWA 100000 TU. NA NILIISHI mazingira ya wachimbaji wadogo kula na kula huko .NA HADI LEO NIPO NA NINA BALL MIIL YANGU NA PML NYINGI japokuwa kifedha bado sijaimalika. mimi nilichagua huku kwa kuwa kunaina nyingi za madini. sasa my plani kuludi kanda ya ziwa nikiwa na uzoefu na uelewa wa kucheza kila aina ya vulugu na utulivu katika sekta hii.

usikate tamaaaa. no alternative burn the ship ili usifikiri kurudi ulikotoka

asante kwa kuniomba ushauri kama nitakuwa sijakushauli vizuri unaweza omba kwa vingine tena
Huu ushauri umenifumbua mengi, nimetoka kupigwa mzigo kwa kuingia kichwakichwa kwenye hii biashara bila kuijua kiundani, hii biashara inataka kuijua na kuwa mvumilivu ndio utaona matunda yake
 
Mafuta na gas za Sasa zimejitengeneza zaidi ya 16million years ago hasa Kati ya 100-250 million years ago. Hivyo siyo swala la muda mfupi. Pia Kuna mazingira yanayohitajima mmea au mnyama kufunikwa na udongo Kisha akaweze Kuwa mafuta ama gasi. Mazingira haya yanahitajika kwenye maji au mazingira yenye majimaji kwa muda mrefu Kama vile bahari, ziwa ama sehemu za chemichemi za maji nyingi Sana
Hata 2million inatisha kuanza kwa kuishi Kama ndege ukiwa site unanunua but kuanzia 5million ni nzuri zaidi

Screenshot_20220316-134933.png
 
Msaada



Naskia kunakiwango kidogo cha dhahabu ndani yake napia ukipata tani moja unaweza tengeneza dhahabu nyingi
Peleka sample maabaraa upate majibu. Siyo dhahabu zote huonekana kwa macho mtupu.
 
Soko la white pebbles quartz limekaaje hapa Tanzania anaefaham msaada plz..

IMG_20220403_123326_566.jpg
 
Naweza kujibu kama ifuatavyo Mr Mreno

2:Mafuta ni bidhaa muhimu sana kwa dunia ya sasa ni vipi mafuta hutokea?

Jibu


Mafuta hutengenezwa kutokana na mkusanyiko wa masalia ya viumbe hai na mimea ambavyo kwa pamoja hufukiwa na mchanga (sediments) kwa kipindi kirefu sana (millions of years) hasa katika maeneo ya mabonde, maziwa, bahari (basin area), mgandamizo na joto linalotokana na kinakirefu cha mchanga kilichofukia masalia ya viumbe na mimea ndicho kinachopelekea kuzalishwa kwa mafuta, gesi na makaa yam mawe (fossil fuels).


7.Gesi na Mafuta hutofautiana nini?

Jibu


Gesi na mafuta vyote hutengenezwa katika namna inayofanana kamailivoelezwa katika swali na 2 kinacholeta utofauti ni joto na mkandamizo unaotumika kutengeza,

Mafuta yenyewe hutengezwa katika joto kati ya (65'C na 150'C) joto hili hupatikana kutika kina 2000m mpaka 5500 meter, Joto likizidi 150'C basi hizo organic compounds ambazo zingekuwa mafuta sasa zitakuwa gesi asilia na likizidi 250'C basi izo organic compounds zitabadilika nakuwa graphite. (kumbuka Joto na mgandamizo huongezeka kadiri kina kinavyo ongezeka.

9. Kipi kati ya Gesi, Mafuta na Madini kina gharama kubwa katika uzalishaji?

Jibu

Napenda kuelezea kuhusiana na gaharama za gesi na mafuta pekee.

Kwanza gharama zinaanzia katika utafutaji na badae tutaona katika uzalishaji, ntaelezea katika mukitadha wa kitu kinaitwa oil and natural gas life cycle.

1. Gharama za kupata access (gaining Access)

Hizi ni gharama zitakazo husiana na kupata vibali katika mamlaka mbalimbali lakini pia kupata documents au taarifa za awali (data) kuhusiana na eneo amabalo unapanga kufanya utafiki ( gharama hizi zitategemea sana sheria na aina ya mikataba katika nchi husika lakin wastani ni dola za kimarekani 20 million na hutumia kati ya miaka 0 mpaka 2 kukamilisha taratibu katika kipengele hiki.

2. Gharama ya kufanya utafiti (exploration cost)

Gharama hizi zitahusisha tafti mbalimbali za awali utakazo zifanya kama aerial survey, seismic ( ambazo unaweza kuzifanya kwakutumia meli kama ni baharini au tracks kama ni nchi kavu) lakin pia gharama za kuchimba kisima kama tafiti za awali zitaonesha dalili njema za kuwepo mafuta au gesi na gharama za kufanyia analysis sample mbalimbali ambazo utazitoa kwenye kisima (gharama zake zitategemea eneo unalofanyia utafiti kama ni kinakirefu cha bahari au kifupi au nchi kavu) wastani wa gharama za kuchimba kisima kimoja katika nchi kavu (onshore) ni dola za kimarekani million 1 mpaka million 15 kutokana na urefu na complication za mahari kilipo wakati kuchimba kisima kimoja katika kina kirefu cha bahari (offshore) (1000 meta na kuendelea) ni dollar za marekani kuanzia million 100 nakuendelea ,so hapo utajumlisha na gharama nyingne za tafiti za awali ambazo zitategemeana na watoa huduma. Unaweza tumia miaka 4 au zaidi katika kipindi hiki cha exploration.

3. Gharama za kuchimba visima vingne zaidi kwa ajili yakujiridhisha kiasi kilichopo katika eneo (appraisal phase cost)

Katika hatua hii utalazimika kuingia gharama za kuchimba visima vingine kadhaa kama kisima ulicho chimba awali kimeonesha matumaini ya kuwepo mafuta au gesi, katika hatua hii visima vinaweza kuwa vitatu au zaidi kwa gharama zile zile nilizo zioredhesha katika point no 2, umhimu wa hatua hii nkutaka kujua jumla ya kiasi kilichopo katika eneo lako atachoweza kuzalisha, unaweza tumia miaka 2 au zaidi

4. Gharama za kuandaa miundo mbinu ya uzalishaji

Katika hatua hii sasa utakuwa tayari umejua kama kitaru chako kina mafuta au gesi au vyote kwa pamoja hivyo utatikiwa kuandaa mazingira ya uzalishaji kulingana na aina ya product iliyopo.

Kama ni gesi asilia ndo ipo

Itakulazimu kuandaa mazingira ya uzalishaji kutoka na soko lilipo kwanza itabidi kujenga kisima kiwe nahadhi ya uzalishaji na sio utafiti tena, hapa utaweka mabomba ya kuzalishia kuanzia chini ya kisima mpaka kwene well head na kisha utajenga kiwanda cha kuisaficha gesi kwani huwa inazalishwa ikiwa na viambata mbalimbali ambavyo hupunguza efficiency ya gesi lakin pia husababisha ugumu wa kuisafirisha.. gharama zake zitategemeana na wingi wa gesi unayo zalisha lakin pia aina na kiasi cha viambata ambavyo unataka kuvitoa kwani kuniaviambata vingine ambavyo ni complex kuviondoa kama hydrogen sulfide, but Tanzania hatuna gesi yenye sulfur gharama za kujenga plant hii ya kasafisha inaweza kurange kati ya dola million 100-200 million kwa kiwanda chenye uwezo wakuzalisha wastani wa 80-180MMcft per day , harafu utatandaza mabomba kutoka kiwanda cha kuchakata kilipo mpaka kwa wateja wako kama watakuwa hawapo mbali sana ( kama ndani ya nchi au nchi jirani ) gharama zake ni umbali wa kutoka mtwara mpaka somanga fungu, songosongo mpaka somangafungu harafu somanga fungu dsm imecost kama pesa za Tanzania zadi ya 1 tillion.

Lakin kama wateja wako wapo nchi za mbali lets say Tanzania to china hutoweza kujenga mambomba kwa umbali huo itakulazimu kujenga LNG plant ambapo itakuwezesha kubadilisha gesi yako kutoka kwenye gesi form kwenda katika liquid form hivyo basi mbali nakujenga kiwanda cha kusafisha gesi itakulazimu kujenga pia LNG plant kwa gharama zake zitategemia nakiasi utakacho safirisha kwa mwaka kam itakuwa ni tani million 1 kwa mwaka kiwanda chako kitagarimu takiribani dola za marekani 1.5bilion hii nikwenye plant ya kupabadilishia gesi kwenda kwenye liquid form lakin ikifika sokoni itabidi kujenga plant itakayo badilisha kuirudisha kwenye gesi form kiwanda hiki kitagharimu takribani dola za marekani 1 bilion uwezo wake itakuwa nikubadilisha kiasi cha gesi yenye ujazo wa 1billion cubic feet per day.

Kuhusu gharama za uzalishaji wa mafuta

Hapa itakulazimu kwanza kuchimba kisima cha uzalishaji au kubadilisha kisima kilicho chibwa kwaajili ya utafiti kiwe cha uzalishaji hivyo utaweka mabomba maalum kwa ajili kutoka chini mpaka juu kwenye well head baada ya hapo utaweka mabomba kutoka kwenye well head mpaka kwenye refinery plant ambayo utaijenga kulingana na wing I wa mafuta unayo zalisha, mfano Uganda wanataka kujenga refinery plant yenye uwezo wakuzalisha mapipa 60000 kwa siku kwa bei ya 2.5 billion dollar unawezakupata picha ya gharama zake lakin wakati huo huo kunakiasi cha mafuta kama 200000 ivi watapitisha Tanzania mpaka bandari ya Tanga kupitia kwenye bomba litakalo jengwa kwa gharama za shilingi 4 billion usa dollar so unaweza kuona how this iverstment cost a lot

So issue nkwamba ni ngumu kujua nkipi kinagharama kubwa kuliko kingne kutokana na mazingir za hiyo product ilipo, composition zake na soko lako
Duh ndio maana Prof Muhongo alisema hawa matajiri wetu hawana hela ya kuwekeza huko. Tukamind kumbe ni biashara nzito hivi katika uwekezaji
 
Mkuu ngoja nikubali kuwa mjinga nipate kitu juz Kun habar ilikua trend Kun dini aina ya ruby walikua wanapiga mnada huko Dubai ambapo samani yake inafika more than 100 us dollars ni pesa nyingi sana hii kitu nacho jiuliza hayo madini wanatumika kutengenezea kitu gani ambayo kinaweza kurudisha thamani ya hiyo hela na mfano wa hivo vitu ni vitu gani
 
mkuu French.

View attachment 582689 View attachment 582692 View attachment 582693 View attachment 582694
picha za miamba mbali mbali za bentonita
Bentonite naomba nikukumbushe kuwa ni madini yatokanayo na mabadiliko ya mavumbi au macjivu ya volcano endapo italipuka na kutua kwenye maji na hasa maji ya chumvi( sea water). kutokana na halii inaamanisha mara nyingi bentonite inapatikana maeneo ambapo volkano imetokea na ikatua kwenye maji ya chumvi.
kwa tanznia yetu maeno haya ni ya ukanda wa bonde la ufa. hasa la upande wa mashariki. yaani ARUSHA-MOSHI-MANYARA-SINGINDA-KIDOGO NA DODOMA. ukiangalia ukanda huu maji yake ni ya chumvi sana hata maziwa yake kama manyara na natroni.
French
Bentonite inakazi nyingi sana kama kama kufyoza uchafu au langi fulani kutoka sehemu flani, inatumika kwenye petroleum refining as catalysis , kutengeneza plastic na paper etc zipo nyingi sana. but swali lako halijalenga huku.

.Sasa hasa hasa wapi utaipata BENTONITE KATIKA UKANDA HUU?.

French

1. minjingu karibu na ziwa manyara
2.Gelai karibu na ziwa Ntroni
3.Arusha karibu na lake Amboseli
4.Iramba siginda ndani ya bonde lawembere-manonga

mkuu French usitoke mbio kwenda kuanza kuchimba ukapata hasara ukanilaumu bureeeeeeeeee et nimekudanganya. mambo ya madini hatakama ukiambia kuwa ndani ya uwanja wa mpira ule kunamadini. usibebe vifaa ukaanza kuchimba.
unahitaji detail nyingi sana ili kujilizisha mahali exactly yalipo na kina pamoja na kujua ubora wake. kwa kifupi maeneo niliyokutajia huwezi kukosa bentonite.


asante kwa swali kama sijakujibu vizuri unaweza kuniuliza kwa upya tena mkuuu.
Kwanza ninashukuru kwa kupata nafasi ya kusoma taarifa MBALI MBALI za madini,na kiujumla nimepata elimu kidogo ya kuanzia.
Anyway kwetu tarime katika shamba letu,nilikuta kwa juu juu kuna mawe flani ya kijani, nadhani kwenye picha ya mwanzo hapo juu,nikachukua na kuja nayo dar na kwenda kupima. Yakakutwa na dhahabu,iron,fe,na madini mengine zaidi ya 7.
Kwa kuwa lilipatikana usawa wa sehemu ambayo hata ukiingiza mguu hufiki kwenye goti,nikaambiwa nichimbe walau futi kadhaa chini,nilete mchanga upimwe na wao wanaweza kuniambia kuhusu usawa wa mwamba,aina za madini,wingi wake na wao huita hayo mawe ya kijani sana kuwa ndo makinikia.
Pia wakasema kwa aina ya hayo mawe, unaweza chimba chini then ukakutana na mawe meusi na ndipo unaweza pata dhahabu katika mawe hayo hasa kwenye kichuguu. Maana yake unakuta mawe meusi makubw,na hapo ndani ya hayo mawe magumu, ndani yake kunakuwa na dhahabu nyingi.
Naweza kupata utaalam kidogo? eneo hilo halijapimwa kwa Sasa hivyo nafanyia process za kupata eneo hilo kwa njia ya hati za kimila
 
Back
Top Bottom