Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

Hakuna leseni ya madini inaitwa hati za kimila. Chukua coordinate Kisha nenda office za madini utaambiwa Kama pako wazi utamiluki. Hati ya kimila ni kumiliki shamba tu. Juu ya madini, inategemea Kama yapo au hayapo. Inahitaji kutafiti. Kama yapo utayapata na siyo sahihi ukichimba chini zaidi ndiyo unayapata. Inategemea na menyewe yapo wapi. Kuna sehemu dhahabu unaikuta juuu kabisa ya aridhi na kazi yako ni kuchota tu.
 
Naomba kujua soko la chrome na pink tourmaline kwa sasa bei ipoje hapa tz
 
Naomba kujua soko la chrome na pink tourmaline kwa sasa bei ipoje hapa tz
Pink tourmaline inategemea imekaaje. I mean ubora wake rangi pamoja na ukubwa. Unapaswa kuchukua chache na kwenda nazo sokoni. Angalia solo lililopo karibu nawe au mabroker walio karibu nawe. Chrome ni metal inahitajika mchakato mkubwa, vizuri ikiwa imechenjuliwa Sasa Kama bado ipo aridhini labda uwekezaji wa kuchimba na kuchenjua Kisha sokoni. But huwa kunaviwanda china wananunua ore yake Ila kwa Sasa sijui zaidi mpaka kufatilia
 
Mkuu ule unga wa mercury nyeusi na nyekundu bei yake ikoje
 
Ruby naomba tuwasiliane please, nina jambo langu la gypsum kule kilwa.

Sent from my MRD-LX1F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu baada ya kuhitimu degree miaka minne iliyopita bila ajira kuna jamaa kanishauri nikasome certificate ya mining processing kwa uzoefu wako baadae ya kuhitimu naweza kupata pa kujishikiza au ndo nitasungua benchi tu?
 
Mkuu Binafsi Mimi nipo interested Sana kujua....I'm passionately curious, napenda Sana kujua regardless nitakifanyia kitu kazi au laah..umesema hapo juu [emoji115] kuwa dhahabu inapatikana kwa uwiano wa 0.004g/tonne, which means that in every 1000kg of stones we have 0.004g of gold...swali langu ni hayo yanakuwa ni mawe ya mwamba wa dhahabu kama ulivosema kuwa always dhahabu inakaa katika mwamba na ikitokea rock weathering ndio tunaipata dhahabu juu ya ardhi kirahisi(placer deposit) au ni mawe yeyote yale yakiwa 1000kg(1T) ndani yake kuna dhahabu kiwango cha 0.004g?
 
ruby garnet kaka habari, haya mawe naomba kujua jinsi ya kufaidika nayo, kwenye eneo langu yapo
 

Attachments

  • IMG_20220826_120636_HDR.jpg
    104.1 KB · Views: 33
Naomba msaada wa kupata leseni ya uchimbaji mdogo na gharama zake.
 
Nenda ofisi za madini za wilaya ulipo mgodi kama una gps chukua cordinates za eneo unalotaka kupata leseni,hapo wataangalia kwenye database kama eneo halina mtu(halina mmiliki),kama halipo katika makazi ya watu,halipo katika hifadhi,halipo katika chanzo cha maji & the same;kama limekizi vigezo hivyo watakwambia uandike barua ya maombi ya kuomba leseni ya eneo hilo na kamati itakaa kujadili umilikishwe leseni...process hii kawaida huchukua wiki mbili na utapatiwa majibu,gharama za maombi ni ilikuwa ni elfu 50 mpk mwaka jana na malipo ya leseni ni laki na 80 kwa kiwanja kwa kila mwaka by the time,hata kama imepanda haitakuwa zimepishana sana
 
ruby garnet Mkuu gharama za kujenga VAT leaching zipoje kwa tank la tone 50 na taratibu zake zipoje?

Naomba uelezee tofali za kuchoma na block na zipi nzuri zadi,natanguliza shukrani.
 
ruby garnet pia Kuna uhusiano gani Kati ya dhahabu na mnyama kakakuona.

Je umewahi kuzisikia tuhuma za wachimbaji kule maduarani kuhusu kakakuona.
 
Mkuu Asante kwa fafanuzi hizi zenye mantiki. Mimi naomba kujua Bei ya madini ya white quartz. Je yanuzwaje, kwa kilo au kwa Tani? Na Bei zake zikoje?.
 
Nina mtaji wa 25M naomba ushauri, ni kipi nifanye kati ya hivi (biashara ya dhahabu)

-kununua karasha na kusaga mawe kisha kutunza rundo (ludio)

-kununua rudio moja kwa moja na kupeleka plant?
 
Nina mtaji wa 25M naomba ushauri, ni kipi nifanye kati ya hivi (biashara ya dhahabu)

-kununua karasha na kusaga mawe kisha kutunza rundo (ludio)

-kununua rudio moja kwa moja na kupeleka plant?
Zote mbili zinalipa na zote zinakata mtaji , inategemea wewe ipi unaipenda. Chagua uipendayo uchape kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…