Uliza ujibiwe kuhusu madini, gesi na mafuta

ASANTE KUSHUKULU MASAWALI YALIYO BAKI NITAKUJIBU NAYO PIA KESHO.
 
Ni dalili gani za asili zaweza kuonyesha kuwa eneo fulani lina dhahabu? Halafu, je ni kweli kuwa yale maeneo yanayotoka moshi chini baada ya mvua kunyesha huwa yana mafuta au yanaashiria nini?
 
mkuu kujenga huo mtambo ya kurifine natural gas ikatumika majumbani ni gharama sana. Imagine plant za madimba na songosongo kwa kuprocess gas cost ni almost 2.5Trilion wakati cost ya LNG plant zidisha hiyo cost mara 10
Mkuu kwa maana hiyo tuendelee kufyeka mapori kwa kuchoma mkaaa,ka Ni kuogopa kujenga mtambo huo Basi gesi hii haina maana kabisa.
 
Nadhani mkuu we umebobea sana kwenye hii fani hongera sana na asante kwa kutu toa ukoko,Nina kiji swali,je ni mawe gani hutumika kutengenezea cement? na ni kwanini yasiwe mawe mengineyo?
 
Ni dalili gani za asili zaweza kuonyesha kuwa eneo fulani lina dhahabu? Halafu, je ni kweli kuwa yale maeneo yanayotoka moshi chini baada ya mvua kunyesha huwa yana mafuta au yanaashiria nini?
katika utafiti wa dhahabu kuna vigezo vingi vinatumika vya awali. kama vile kunalamani za kijeolojia zinazoonesha wapi utapata madini ya aina gani na ramani hizi hutengenezwa na wajeolojia na kwa tanzania zinatengenezwa na kitego kinachoita geologiacal survey of tanzania zilizopo dodoma(GST). mfano katika leve ya dunia zipo na katika leve ya nchi zipo na kwa mfano katika ramani ya kijeolojia ya tanzania zinaonesha dhahabu zinapatikanika kwa wingi kanda ya ziwa, chunya mbeya, mpanda rukwa na ukifika katika maeneo hayo kunaramani za kilevo ya wilaya na hivyo utakuta kwa mfano wilaya ya geita siyo yote inadhahabu bali kunasehemu tu. kutokana na hayo ukifika unapaswa kutumia tafiti za geophyics, kikemia ambazo hutumika kurahisisha kupunguza aneo la kutafiti. na pia wachimbaji wadogowadogo wanatumika sana kuonesha wapi kunafaa kufanya utafiti. kwawachimbaji wadogowadogo dalili ni kupatikana kwa dhahabu za kuosha kutoka kwenye udongo hii inamaana kunamwamba karibu umesababisha dhahabu isambae kwenye udongo huo huko kanda ya ziwa wanaita sesa maana yake za kuchota mchanga na kuosha kwenye maji na kuziona. pia kwa wazoefu waliochimba siku nyingi wanaijua aina nyingi ya miamba hivyo wakiona tu aina ya miamba hiyo wanakuwa makini kuifatiria.

kuhusu mvuke
H
ii haina na mahusiano ya mafuta ila hii huwa kuwa ardh imechemuka juu na mvua inaponyesha inapoza kwa ghafula na hivyo husababisha ujoto uliokuwa ardhini utoke kwa njia mvuke. na huu mvuke waulize walima nyanya wanajua madhara yake kwani huwa unachoma majani ya miche ya nyanya na kuwa na mabaka ya rangi ya ugolo na huwahalibia mazao yao.


ASANTE KWA SWALI KARIBU TENA
 
1.Ntalitambuaje jiwe lenye dhahabu maana nilikaa geita kila siku naokota mawe ila wenyeji wananiambia bana haya hayana dhahabu ni ulanga tuuu

2.mchakato mzima wa gesi kwa tanzania tumefikia level gani
 
Nadhani mkuu we umebobea sana kwenye hii fani hongera sana na asante kwa kutu toa ukoko,Nina kiji swali,je ni mawe gani hutumika kutengenezea cement? na ni kwanini yasiwe mawe mengineyo?

Bwana last king

Cements inatengeneza na raw materia kuu tatu
1) Limestone (caco3) haya huchukua takribani 70-80% kwenye cement na haya mawe yanapatikana ukanda wote wa pwani ya tanzania kuanzia Tanga hadi Mtwara na ndiyo maana viwanda vyote vinajengwa ukanda wa pwani kuanzia kilichopo tanga, dar wazo hili, kunakingine kigamboni, mkulanga, lindi na mtwara mawe haya ndiyo yaliyo na rangi ya weupe na ugolo au mawe yanayovujwa kokoto kunduchi haya mawe ndiyo yanayotumia .kiwanda kimoja tu kipo mbali na pwani nacho ni mbeya cement ambacho kinatumia materia yanayoitwa Siderite(Feco3) ambayo yapo kwa wingi sana hapo songwe maji ya moto. na diyo maana kiwanda kimejengwa hapo.
2) Gypsum(Caso4). materia haya yanapatikanika makanya same, singida, dodoma na kilwa maeneo ya mandawa. lakini yanayopatikana mandawa diyo bora kuliko maeneo mengine na hivyo kufanya viwanda vingi vya cement vinanunua gypsum kutoka kilwa.
3) Irone ore (50Fe%) viwanda vingi vinapata kutoka tanga na lindi.

sasa mkuu kwa nini hawatumii mawe mengine?
.

jibu1`
kwamba cement inahitaji chemical composition frani na hivyo inahitaji raw material ambazo zikichanganywa zitaweza kuunda chemical composition hiyo. tofauti na hapo hakuna cement mkuu.
 

Nashukuru sana sana kwa kutumia muda wako kujibu maswali yangu na kunielimisha.. hakika nimeyasoma mara mbili mbili kuhakikisha naelewa vizuri.. I really would like to commend you.. natamani watu wengine wenye uelewa kwenye maeneo kadha wa kadha wachukue muda wao kutoa nafasi ya kuulizwa maswali na kutujibu hivi... Be blessed
 
Asante kwa kuelewa ,karibu tena.
 
1.Ntalitambuaje jiwe lenye dhahabu maana nilikaa geita kila siku naokota mawe ila wenyeji wananiambia bana haya hayana dhahabu ni ulanga tuuu

2.mchakato mzima wa gesi kwa tanzania tumefikia level gani
Majibu swali la 2

Kuhusu ni wapi tumefikia Juu ya mchakato wa gesi,, nikwamba uzalishaji ulishaanza mapema tangu mwaka 2004 huko songosongo Lindi na mnazi bay mtwara mwaka 2006 ...gas ya songosongo ililifika dsm nakuanza matumizi yakuzalisha umeme pamoja na viwanda vingine. Wakati gas ya mnazi bay mtwara ilianza kutumika kuzalisha umeme unaotumika mikoa ya kusini.

Kuanza mwaka 2012 ndipo ugunduzi mkubwa wa gesi katika kinakirefu cha bahari ulitokea ..nakumekuwa na mfululizo watafiti kuliko pelekea kupata jumla ya gesi yenye ujazo unaofikia 57 trillion cubic feet kwa data za mwaka Jana,, kufuatia ugunduzi huu mkubwa ndipo serikali ikaja nawazo lakujenga bomba kubwa la gesi kutoka mtwara na songosongo kuja dsm kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme ambao tayari pale kinyerezi umeme unazalishwa lakin pia gesi itatumika katika viwanda vingi vitakvyojengwa mwambao mwa bomba hilo lagesi.

Lakin pia kwa kuwa gesi hii ni nyingi sana ,,mpango uliopo sasa nikuuza nchi za nje..upo mpango wakujenga kiwanda cha kubadilisha gesi kwenda kwenye kimiminika (LNG) plant hii itawezesha kusafirisha kwa uraisi zaidi huu mchakato ulisha anza nabila shaka kufika miaka ya 2020-2025 huenda tukaona mradi ukikamilika.
 
Napenda kujua mafuta yanaagizwa nchi gn tunayotumia na kwa nn tusinunue kwny nchi km Sudan iliyopo ili kupata unafuu wa gharama z usafirishaji
 
Jibu swali na 11

Utofauti wa gesi tunayotumia nyumbani kwasasa na gesi asili tuliyo igundua nchini ni kwamba ..hii gesi tunayotumia nyumbani inajulikana kama liquified petroleum gas (LPG) ambayo nimoja ya zao linalotokana na kurifine mafuta(crude oil) ukichimba mafuta huwa yanapelekwa kwenye refinery plant ambayo hutenganisha product mbalimbali kulingana na boiling point ya product husika ambazo mojawapo nihii gesi inayotumika nyumbani LPG katika chemia inaitwa propane na butane ikiwa katika mitungi inakuwa katika form ya kimiminika.... harafu zinafata product nyingne kama kerosine,disel ,gasoline na mafuta mengine mazito.

Wakati gesi tuliyogundua Tanzania hii asilimia kubwa ni methane, haitokei katika mafuta yenyewe ni natural made as gas ndo mana ningumu kuibadilisha kuwa kimiminika nakuiweka katika mitungi kama ya LPG nakutumia nyumbani kumbe njia rahisi nikuisafirisha katika bomba mpaka nyumbani ..kama ilivyo bomba za maji au umeme unavotufikia nyumbani.... ingawa unaweza kuicompress katika mitungi maalumu (CNG) naikatumika kama fuel kuendeshea Gari ..pale ubungo kunakituo hicho
 
ni chuo gani duniani naweza kufanya Msc Oil and Gas Accounting, gharama zake na naweza vipi kupata sponsorship ama scholarship?
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120] asantee mkuu
 
1.Ntalitambuaje jiwe lenye dhahabu maana nilikaa geita kila siku naokota mawe ila wenyeji wananiambia bana haya hayana dhahabu ni ulanga tuuu

2.mchakato mzima wa gesi kwa tanzania tumefikia level gani


1.Ntalitambuaje jiwe lenye dhahabu maana nilikaa geita kila siku naokota mawe ila wenyeji wananiambia bana haya hayana dhahabu ni ulanga tuuu

jibu


LYNNE. Mimi pia nilikutana jambo kama hilo kwa muda sana nilifikia kuelewa.
ukweri ni kwamba miamba ya dhahabu ipo mingi sana hata ndani ya mgodi mmoja unakuta kunaaina zaidi ya moja miamba yenye dhahabu hivyo unahitaji udhoefu wa mwamba wa dhahabu maeneo ulipo. hii inamaana kuwa hakuna mwamba unaojulikana kuwa ni mwamba pekee unaokuwa na dhahabu. kumbuka kuwa ili kuiona dhahabu kwenye mwamba inahitajika huo mwamba uwe na dhahabu kubwa kubwa. yaani kunamiamba mingine dhahabu zake nindogondogo ambazo huwezi kuziona kwa macho wazi( very small grain of gold you can not see by necked eyes). hata hivyo kunamiamba mingine dhahabu yake ni kubwa kubwa hivyo inaonekana kwa majo tu. na ili uweze kuiona pia unapaswa kuijua rangi yake ambayo huwa golden yellow. lakini pia madini wanayoita ulanga kwa kitaalamu yanaitwa pyrite(FeS) Ambayo pia ni ya njano na kwa jina la mtaani yanajulikana kama foolish gold. pia kunamadini mengine kama arsenopyrite na chalcopyrite pia nayo ni njano(yellow) kwa ujumla unahitaji udhoefu wa mwamba wa mahala fulani ili uweze kuelewa huu ni mwamba wa dhahabu. vinginevyo kunajia za kujalibu kufanya ili kufikia maamuzi kuwa huo mwamba unadhahabu. ya haraka zaidi wachimbaji wadogowadogo wanaita kupiga sample maana yake kuchukua jiwe unalohofia kuwa linadhahabu na kulitwanga kisha kupiga kalai au bangala (kufanya panning) ili kuona kunadhahabu au hamna


ASANTE KWA SWALI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…