Tetesi: Umakamo wa Urais Zanzibar ni Joto

Mjomba umerudia rudia sana hoja kiasi umefanya andiko lko liwe refu bila ya sababu za msingi.
Hayo yote uliyoandika yangetosha kwa mistari michache tu na ungeeleweka vizuri.
 
Lazima niwashangae. Kwani wenye kuchagua kiongozi wao ni nani. Huyu ni msomi wa sheria na alilo lifanya kwenye mchakato wa katiba ni kusimama na msimamo wake. Hapo sioni kosa. walipokuja kwenye mchakato wa katiba viongozi wote wa zanzibar walikuwa na msimamo mmoja. walipofika daressalaam, CCM waote waligeuka sababu ya uluwa isipokuwa mwana sheria wao ambae alisema hawezi kuyumbishwa baada ya kukubaliana na wenzake halafu kusaliti wazanzibari. sasa hapo kuna siasa za kiislamu zimetoka wapi. Huyu Othmani, ulizeni mke wake ni nani?. Acheni kutuletea ujinga wa CCM hapa. Sisi tunajadili masuala kabambe ya kuendesha taifa na nyinyi wenzetu munajadili fitina tu. Munafikiri sisi wazanzibari wajinga?. Basi tuheshimiane sana. Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Majority tulitaka serikali Tatu na mpaka leo ndio msimamo wetu. Sisi tumekataa UDIKTETA katika nchi yetu na Tumeikataa CCM kwa jumla. Liliopo ni kukubaliana na ndicho kiliopo venginevo hatushindwi kujieleza na mutaipata habari karibuni. ACT na makubaliano yao haiwahusu. Akiwa Juma Duni au Othman Masoud , hilo ni chaguo la ACT wazalendo na nyinyi mulimueka Hussein kwa maguvu. sasa kuna nini tena. DEMOKRASIA au UDIKTETA?.
 
Mbona watu mnamuogopa mwanasheria mwenye misimamo madhubuti na iliyo wazi? ACT inachagua wao si wajinga wakurupuke. Serikali moja muungano, serikali mbili muungano na serikali tatu muungano. ACT itaamua makamu wanaempeleka akasimamie nini. Huenda ni wakati vijana "washirikiane" kuijenga Zanzibar.
 
Kama alikuwa kinyume na wenzake wote wa Zanzibar ina maana hafai na usomi wake hajui maana ya maamuzi ya pamoja ina maana hata akiingia serikali ya umoja wa kitaifa wakifanya maamuzi kwa pamoja akiwa yeye hakubaliani nayo atapinga hajui maana ya makubaliano ya pamoja!!!

pili waliosrma adilimia kubwa kwenye kutoa maini kutaka serikali tatu zanzibar wengi walikuwa wapemba wallikuwa wakisikia tume inaenda mahali fulani na wao mbio wanaenda adi jaji.warioba akahoji mbona lafudhi ni zile zile za sehemu zote tunakoenda vikao wanaaongelea serikali tatu ni wale wale wa kutoka sehemu moja ya zanzibar yaani pemba? Walikuwa Wamepanga watu kila kila kikao na wanaongea kitu kile kile kwa kukariri hadi nukta na mikayo kuanzia mwanzo wa sentensi hadi mwisho tume ya maoni wakashtuka.Lakini kwa kuwa kazi yao ilikuwa tu kukusanya maoni tu ndio wakaatoa takwimu hizo lakini with reservation ya kilichotokea Zanzibar.Ile haikuwa kura ya maoni ilikuwa kukusanya tu maoni roughly lakini wapemba wakaharibu mchakato uonekane kama ni wa kwao zaidi badala ya kuuacha freely bila kupanga watu kila mkutano
 
Nafikiri hata huelewi kazi ya makamu wa Raisi kule haendi kuwa mbunge wa kupigania serikali tatu akishateuliwa anaapishwa kuilinda katiba ya zanzibar iliyoko sasa inayotambua muungano wa serikali mbili !!! Hilo la kusema ohhh akapiganie serikali tatu sio mandate yake na halimo.kwenye kiapi chake!!! Hapewi hiyo kazi kuwa nenda kapiganie serikali tatu!!! Kule ni kuapa kulinda katiba tu iliyopo inayotambua muungano uliopo!!!
 
Kwanini isiwe Zitto Kabwe?
 
Mnataka mtu legelege ili muendeleze usanii wenu???
 
Wee bi.mdogo ni msumbufu kwel hakuna kinachokusumbua zaid ya ukafr wako uliokubuhu
 
Acha porojo
 
Wewe unataka kusema unamfahamu Othman kuliko wafuasi wa upinzani na wazanzibari wenzake?

Kwahiyo Serikali ya Zanzibar ilikuwa na AG wa Uamsho ?
 
Inaonekana hujui chochote., Makamo wa kwanza siyo ihsani toka kwa DrMwinyi kuendeleza umoja, ni takwa la kikatiba ya Zanzibar, haijalishi
Mwinyi atake au asitake akipewa jina la Othman Massoud kutoka ACT hana alternative katiba inamtaka amchague tena mara moja ili kukidhi zile % mgombea wa 2 alyepata asilimia kadhaa chini ya mshindi katika uchaguzi mkuu.

Suala la Othman kua na agender tofauti na DrMwinyi akiwa kwenye huo umoja wa kitaifa haijalishi as long as yeye Othman ameaminiwa na chama chake juu ya kusimamia kile wanachokiona kina maslahi na Zanzibar.

Na hapa ifahamike uzuri kwamba ccm wanataka ku-take advantage kwamba maalim seif dakika za mwisho alihimiza umoja kwaiyo wao wanataka umoja udumu hata watu wakiporwa ushindi wao kwa nguvu za kijesh waendelee kuwa laini laini na utiifu tu jambo ambalo ACT hawatatakiwa kuendelea kutii mpaka haki zitakapotamalaki ili huo umoja na mshikamano wanaohubiri kuachiwa na maalim seif uambatane na haki sawa kwa wote.

Dr Mwinyi ni rais wa Zanzibar kwanini litakapokuja suala la Zanzibar kuwa na mamlaka yake kama hapo kabla aje akatae? Nadhan Dr Mwinyi aungane na huyo Othman massoud kama atapendekezwa jina lake ili wote kupigania maslahi ya Zanzibar hapo watakuwa wamemuenzi maalim seif vizuri
 
Kumbe ni huyu,apewe mitano!
 
Mtu aliyekuwa kwenye Trenches na Maalim kwa miaka na miaka ndiye anayefaa.
CV ya Babu duni inajitosheleza sana kuanzia kisomo, utendaji kazi serikalini hata harakati za kisiasa
 
Mnataka mtu legelege ili muendeleze usanii wenu???


Wala hakuna anaebishia hilo ‘Othman Masoud’ ni tough cookie to bite na msimamo wake ni mmoja tu getting out of the union.

Tofauti yake na wenzake wa anti union he is very clever and calculating. Hana pupa ya kutaka yote kwa pamoja, mbinu zake ukimsikiliza ni kumega taratibu nguzo za muungano mpaka unavunjika.

Kwa Othman Masoud siasa ni daraja tu la kufikia adhma yake but deep down ni scholar ambae pengine sasa hivi angekuwa anafundisha that’s his passion ukimsikiliza. Isipokuwa siasa ndio njia pekee other than mbinu za kuingia msituni kuharibu muungano ambao haupendi with passion.

Tanzania ni moja bara na visiwani ni ndugu ukienda Tanga mjini asilimia kubwa ya population ni wapemba leo, so I am told. Yeye hataki mahusiano mazuri ya watanzania sujui ana matatizo gani.
 
Si kweli walikuja wote wameridhia kuna watu kama VP mama Samia, Nahodha na wengine wachache awakuunga mkono maamuzi ya serikali tatu tangia Zanzibar. Waliobaki walihitaji kupewa perspective nyingine ya mapendekezo ya rasimu ili wafanye maamuzi sahihi, sio kufuata porojo za bwana Masoud.

Ndio maana namuona Othman Masoud being poisonous for the stability of Tanzania; very persuasive and tactical with his long term plan.
 

Unajua ukija kwenye maslahi ya Tanganyika hakuna mzanzibar atakae faa ispokuwa mlafi wa madaraka, ukija kwenye maslahi ya Zanzibar mtu Kama huyu ndie anae faa, kwa msemo mwengine nyinyi hutumia kuwa sio Mtu mzuri kwa maslahi ya Tanganyika na Muungano.

Kama wazanzibari Sisi tunaangalia Zanzibar, na ndio sababu kuu ya marehemu Maalim seif kukubalika visiwani Zanzibar.

Huyu kijana ni jembe
 

Unaongea about family or about countries? Don’t be a fool 🥸
 
Sema maslahi yako sio wazanzibar wote maana wapo wengi tu pro union Zanzibar na Pemba; ambao wapo tayari kuulinda muungano kwa nguvu zote.

If anything watu kama kina Othman Masoud ni tatizo la social unrest na wanaotenesha vidonda kila siku.

Yaleyale ya Alex Salmond na Nicola Sturgeon na siasa za Scotland kumbe kuna vita kubwa nyuma yao kisa siasa za kupishana kwenye maswala ya muungano hadi kutungiana kesi za sexual abuse.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…