Umalaya na Umiliki wa Danguro ni Kosa La jinai

Umalaya na Umiliki wa Danguro ni Kosa La jinai

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Tukio la kusikitisha lililotokea Arusha , kwa kifupi binti anauza uchi, amepanga nyumba ambayo ni Danguro , kosa la jinai lakini walikuwa na matron wao, menas Kumiliki danguro ni kosa la jinai na kuishi au kufaidika na mapato ya biashara ya ngono (kuuza mwili) ni kosa kisheria chini ya Kanuni ya Adhabu.

1. Kunukuu Sheria Kuhusu Kumiliki Danguro (Brothel)
Kufungua, kumiliki, au kusimamia nyumba au chumba kwa ajili ya biashara ya ngono ni kosa la jinai. Kanuni ya Adhabu inatamka hivi: Kifungu cha 148 (Section 148): “Mtu yeyote ambaye anamiliki, anaendesha au anasimamia nyumba, chumba, au sehemu yoyote kwa ajili ya madhumuni ya ukahaba anatenda kosa.”


2. Kunukuu Sheria Kuhusu "Kuuza Malaya" (Kufanya na Kufaidika na Ukahaba)
Sheria haizuii tu kitendo chenyewe cha ngono, bali inafanya kuwa kosa la jinai kuishi kwa kutegemea mapato yanayotokana na ukahaba au kushawishi watu kufanya hivyo: -
Kifungu cha 145 (Section 145): Inahusu mwanamume anayeishi kwa kutegemea mapato ya ukahaba au anayeomba/kushawishi hadharani kwa madhumuni ya ukahaba.
Kifungu cha 146 (Section 146): Inahusu mwanamke anayeishi kwa makusudi (kwa sehemu au kikamilifu) kwa kutegemea mapato ya ukahaba, au anayemsaidia au kumdhibiti kahaba kwa masilahi yake.​


3. Nyumba ya Danguro inaweza kutaifishwa na Serikali.
Chini ya Kifungu cha 25(e) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mahakama ina mamlaka ya kutoa amri ya kutaifisha mali yoyote (Forfeiture Order) ambayo imetumika kutenda kosa la jinai au ambayo ni zao la uhalifu. Ikiwa mmiliki wa nyumba (mwenye nyumba au mpangaji) atapatikana na hatia ya kujua na kuruhusu nyumba hiyo itumike kama danguro, mahakama ina nguvu za kisheria kutaifisha jengo hilo kuwa mali ya Serikali.​



IMG_3340.jpg


​
 
Mi nadhani ingekua tuu biashara huru na itengewe maeneo rasmi walipe kodi..😇😇
La sivyo wanaume watabaka mpaka kuku...maana akili zao zikishuka chini hawaangalii. Kama kichaa anazaa hapo kuna nini tena...
 
Hii biashara wangepewa leseni na vitambulisho kabisa. Pia iwe ni sharti kupima magonjwa ya maambukizi kila baada ya miezi mitatu na status zao ziwekwe kwenye ID zao. Vilevile kuwe na sheria za kulinda wateja na wao pia.

NB: Binafsi naona kinyaa kulala na mwanamke wa kununua nikijua kabisa kuna jamaa mwingine katoka kuichapa
 
Mi nadhani ingekua tuu biashara huru na itengewe maeneo rasmi walipe kodi..😇😇
La sivyo wanaume watabaka mpaka kuku...maana akili zao zikishuka chini hawaangalii. Kama kichaa anazaa hapo kuna nini tena...
Sasa ndiyo muwe mnawapa msiwanyime
Tatizo mnajua halafu mnjifanya wehu kuwanyiwa wanaume
Wapeni huo utelez kwan anaondoka nayo
 
Back
Top Bottom