Umasikini ambao upo nchi za Africa ni umaskini bandia na sio umasikini unaotokana na Mazingira au umasikini halisi

Kwa kuwa hakuna ukomo wa kuchangia,nirudi tena.Pasco Mayalla aliwahitoa mada juu ya viongozi wetu humuhumu JF.Kwamba viongozi wetu ni sehemu ya jamii na hivyo walivyo ndivyo jamii tulivyo.Swali ni:kuwatwika zigo la lawama kwani sisi tukoje?Kiongozi atakuletea maendeleo mlangoni kwako umekaa?Kama ni wabovu nani kawapa ridhaa kuongoza?Nchi haina vurugu,miundombinu wezeshi kama barabara,maji,umeme,ardhi vipo na hufungwi kukaa sehemu moja:wataka uwezeshwe kwa kipi Mtanzania ili uwe mlipa kodi mzuri?Huyu kiongozi unayemlaumu kwani anatoa fedha mfukoni kwake ili kuleta maendeleo?Serikali inapata wapi kodi wakati wewe hujishughulishi?
 
3.£limu mbovu/makapi.
kwangu hili ndo lilipaswa kuwa namba moja maana linaathiri hayo mengine. juzi nikiwa ktk mstari wa kupiga kura nikashangaa kuona bado kuna wasiojua kusoma na kuandika. sasa nikafikiri tu nchi ina watu wangapi kama hawa? hlf ndo tutegemee kupiga hatua kimaendeleo? apo sahau ndugu.
 
Umasikini wa Africa ni Kwa ajili ya wazungu kuendelea kutawala bara lake,ktk bara lililojaaliwa Kwa malighafi duniani Africa ni lakwanza,malighafi zote,madini,gas,mafuta,vimejazana ila wazungu wametengeneza mfumo kua huwezi pata hela from hizo malighafi,mbaya zaidi wanapandikiza viongozi na vita ili muendelee kuwaabudu wao tu,DRC moja ya nchi tajiri Kwa malighafi,Somalia-gas+mafuta,madini,Central African,Mali,Bukoba faso,Libia,in nutshell Africa ni migodi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…