Empedocles
Senior Member
- Sep 11, 2024
- 151
- 192
Kwa kuwa hakuna ukomo wa kuchangia,nirudi tena.Pasco Mayalla aliwahitoa mada juu ya viongozi wetu humuhumu JF.Kwamba viongozi wetu ni sehemu ya jamii na hivyo walivyo ndivyo jamii tulivyo.Swali ni:kuwatwika zigo la lawama kwani sisi tukoje?Kiongozi atakuletea maendeleo mlangoni kwako umekaa?Kama ni wabovu nani kawapa ridhaa kuongoza?Nchi haina vurugu,miundombinu wezeshi kama barabara,maji,umeme,ardhi vipo na hufungwi kukaa sehemu moja:wataka uwezeshwe kwa kipi Mtanzania ili uwe mlipa kodi mzuri?Huyu kiongozi unayemlaumu kwani anatoa fedha mfukoni kwake ili kuleta maendeleo?Serikali inapata wapi kodi wakati wewe hujishughulishi?