Umasikini hurithiwa; masikini huzaa masikini

Umasikini hurithiwa; masikini huzaa masikini

Zamani kabla ya kutembelea duniani na kuona ya walimwengu nilikuwa nadhani mtu akishakuwa na sehemu ya kulala, chakula na vinywaji na pengine gari na fedha za akiba, basi huyo atakuwa ni mtu mwenye mafanikio na furaha tele. Kila niliposikia wazungu wakisema ''important thing is to be happy'' nilikuwa nadhani ukishakuwa na hayo niliyosema ni lazima uwe ''happy''. Sasa hivi nina mawazo tofauti kabisa baada ya kuona kumbe unaweza kuwa na yote hayo lakini usiwe ''happy'' na mtu anaweza kuwa anaishi kwa shida lakini akawa ''happy''
Umasikini ni takataka

Hakuna ufahari wowote ule kwenye umasikini, kabla hatujaendelea jua hilo.

Umasikini ni wimbi linalobeba takataka nyingi ndani yake
1)Njaa
2)magonjwa
3)kudhalilika
4)Elimu duni
5)makazi duni
6)mavazi duni
7)nk

Happy ni nini??
_Happy ni hali ya kujisikia vizuri, hulu, amani and all good condition zipo ndani ya Happy, Happy sio Subset ya umasikini wala utajiri...unaweza kuwa maskini ukawa Happy na unaweza kuwa tajiri ukawa happy and Vice-versa.

Kuna vitu vingi vinavyosababisha mtu asiwe na furaha most of them ni vitu vibaya na vitu vingi vibaya vipo kwenye Maskini, Maskini automatically.

Shida zinazomkumba masikini akakosa furaha
*Ana Ada yang shule
*mtoto anaumwa Hana PESA ya matibabu
*nyumba ipo bondeni mvua inanyesha halali mafuriko yakija anabeba godoro kujihifadhi Mchikichini Secondary
*Mlo mmoja kwa siku kawaida au kupita wima
*kudhalilishwa madeni
*nk nk

Unakiwaje Happy katika shida hizo zote au wewe mwenzetu mwanao akiumwa ukakosa pesa ya hospital unakuwa na furaha.

Hitimisho
_kila mtu anaweza kuwa na furaha au kutokuwa nayo ila kwenye Maskini na tajiri, Asilimia 99% ya masikini hawana furaha kwa matajiri ni asilimia ndogo sana wasio na furaha 10% tu.

Hivi hawa wanapata wapi utulivu wa nafsi 👇


 
UMASIKINI HURITHIWA; MASIKINI HUZAA MASIKINI.

Na, Robert Heriel

Andiko hili linaweza lisifurahishe watu wengi hasa watu masikini, lakini huu ndio ukweli na acha niseme ukweli tuu. Hata hivyo sitakuwa wa kwanza kuusema ukweli huu kwani wahenga pia walishasemaga; Ng'ombe wa masikini hazai, na akizaa ndama anakufa. Baadaye wakaongeza kusema, maji hufuata mkondo kwani mwana wa nyoka ni nyoka. Leo hii semi hizo na nyingine kama hizo zinathibitika katika maisha yetu.

Andiko hili nimeandika kwa lengo la kuamsha utambuzi wa mtu binafsi, kwa mtu akijitambua ni rahisi kujisaidia, andiko hili liwe sehemu ya kujitambua na kujinasua kutoka katika mizizi ya mtu ya umasikini kama nitakavyoeleza hapo chini.

Ikiwa Baba na mama, na Babu, na Bibi, na ukoo wenu kwa ujumla ni masikini basi umasikini wako ni dhahiri hauepukiki, umasikini wako ni wakurithi.

Babu yako alikuwa masikini, akamrithisha Baba yako;naye ni masikini, Baba yako naye akakuzaa wewe kisha akakurithisha umasikini. Nawe unavitoto vyako bila shaka lazima virithi umasikini kwani umasikini ugonjwa wa kurithi.

Kwenye hii Dunia kuna mambo Au watu EXCEPTIONAL. Watu exceptional ni wale ambao wanavunja au hawafuati kanuni, desturi au asili iliyokuwepo. Kwa mfano, zipo jamii zina watu wafupi kama vile waluguru, hivyo sio ajabu mtu akisema Waluguru ni wafupi kwa kimo na watu wakamuelewa ingawaje wapo waluguru wachache warefu, hao wachache ndio tunaita exceptional yaani waliovunja kanuni ya asili ya ufupi.

Au Wasukuma ni warefu na majitu lakini wapo exceptional ambao ni wafupi.

Hivyo hivyo hata katika Kurithi Umasikini katika familia, kama familia ni yakimasikini basi ni dhahiri watoto wote wanaweza kuwa masikini na kama akitokea mtoto mmoja akawa na uwezo basi huyo tunamuita exceptional.
Yaani unakuta kwenu mmezaliwa watoto saba, watano ni masikini na wawili kidogo wanajiweza, hawa wawili ni exceptional ambao kimsingi hawaondoi asili yenu kuwa ninyi ni koo masikini. Exceptional haiondoi asili.

Hii pia ipo kwa utajiri, kama mmezaliwa saba, watano wanauwezo alafu wawili ni masikini, basi familia hiyo ni yakitajiri hao masikini wawili ni exceptional hawaondoi utajiri wa familia.

Umasikini ni ugonjwa wa kurithi ambao bado wataalamu hawajaubainisha katika magonjwa. Na moja ya magonjwa mabaya ya kurithi ni ugonjwa umasikini.

Mtoto unapozaliwa haujizai, unabeba vinasaba, maumbile na tabia za wazazi wako. Kuanzia sura, tembea, mikao, uongeaji na tabia zako zingine kwa sehemu kubwa unazirithi kutoka kwa wazazi wako. Ikiwa ni hivyo mambo hayo unayoyarithi ndio yanayokufanya uwe masikini au uwe tajiri.

Wazazi au ukoo masikini wanaongozwa na kanuni na mifumo ya kimasikini, unapozaliwa kwenye umasikini kwa sehemu kubwa kanuni na mifumo unayoitumia itatokana na mifumo ya kimasikini. Kanuni na mfumo wa kimasikini hukupelekea wewe kuwa masikini upende usipende.

Ukioa au kuolewa na masikini au jamii masikini ni wazi kwa 90% lazima familia yako iwe masikini tuu, labda ujidanganye. Ni sawa uwe mweupe na asili yenu ni weupe alafu uolewe au kuoa mwenza mweupe mwenye asili nyeupe alafu utarajie utazaa mtoto mweusi huko ni kujidanganya.

Umasikini hurithiwa kutokana na kuwa umasikini ni mfumo na kanuni, kama vile ulivyo utajiri ambao nao ni mfumo na kanuni.

Ukibahatika kuwa na pesa kwenu, yaani kama kwenu mumezaliwa sita, kisha wewe ndiye umefanikiwa kupata vipesa basi jua kuwa bado haujasalimika, waliochini ni wengi na wananguvu ya kukuvuta chini zaidi ya waliojuu hivyo ni rahisi kurudi chini kuliko kwenda juu.

Umasikini ni kama Gravity Force na Utajiri ni kama Centrifigal Force. Gravity force inakuvuta chini wakati Centrifigal inakuvuta juu. Hivyo kama Gravity(force ya umasikini) Ikiwa na nguvu kuliko Centrifigal force ni wazi wewe lazima uwe masikini. Na force ya umasikini inakuwa kubwa na nguvu pale ambapo kwenye familia masikini ni wengi kuliko matajiri.

Mkiwa mmezaliwa saba, watano wanapesa na wawili ni masikini, hii inamaanisha matajiri kutokana na wingi wao watakuvuta kwenda juu hata kama sio juu sana lakini angalau, na force ya chini itakuwa ni ndogo ya kukufanya uwe masikini.

Hata kama utazingua lakini bado watoto wako utasaidiwa kusomeshewa na ndugu zako hao watano wenye pesa, pale wakikuona wewe umezingua na unamambo ya kimasikini.

Familia masikini na koo masikini zina mitizamo yao(Their attitudes) ambayo ni yakimasikini wanayoirithisha kwa watoto wao. Familia masikini nyingi ni masikini kwa mali na masikini kwa fikra zao.

Kama ilivyo rahisi kwa mtoto kurithi maumbile ya wazazi wake ndivyo ilivyo rahisi kurithi na umasikini wa wazazi wake.

Waafrika wengi ni masikini, sio wafrika waiishio bara la Afrika pekee bali hata waishio mabara mengine kama vile Bara Hindi, Amerika na Ulaya, pamoja na Carribien. Umasikini wa Muafrika ni wa Kurithi na hiyo ndio sababu kubwa. Kama tunavyorithi ngozi nyeusi za wazazi wetu ndivyo tunavyorithi na Umasikini. Kuna watu wanasema kuwa umasikini wa Muafrika unasababishwa na athari za Biashara ya utumwa, ukoloni na athari ya ukoloni mamboleo jambo ambalo sio kweli. Kuna nchi kama Ethiopia tangu dunia kuumbwa haijawahi kuwa chini ya Ukoloni, tena kwenye dunia hii nchi zote zimeshawahi kutawaliwa na mataifa mengine lakini Ethiopia haijawahi. Lakini wapo wapi hivi leo.

MBINU KUU ZA KUONDOA UMASIKINI WA KURITHI

1. KUOA AU KUOLEWA NA MATAJIRI. CHANGANYA DAMU
Hii ndio mbinu namba moja, achana na ile wanakuambia fanya kazi kwa bidii, sijui acha uvivu huo ni uongo, hata uchape kazi miaka nenda rudi, usiku na mchana kama umetoka familia masikini utabaki kuwa masikini tuu na kama utapata vihela alafu ukaoa/ukaolewa na masikini bado upo kwenye mzunguko ule ule wa kurudi kwenye umasikini.

Zipo koo zililigundua jambo hili muda mrefu, wengi waliolewa na kuoa jamii zenye utajiri na sasa ni matajiri, wangapi wameoa wazungu au kuolewa na wazungu miaka ya 80 au 90 na leo hii familia zao ziko vizuri. Sio tuu wazungu, hata baadhi ya waafrika wanaotoka kwenye jamii zenye asili ya utajiri. Wamechanga damu na sasa wanakula bata kwa kuzaa watoto mchanganyiko wa umasikini na utajiri.

Kuchanganya damu ni muhimu sana kwa watu wenye mipango ya milleniamu lakini kama unamipango ya leo kesho basi sio lazima ufuate nikisemacho.

Masikini wanafikiri Mungu anawapangia maisha wakati Mungu hana time nao, wewe na ufupi wako jaribu kuoa/kuolewa na mfupi mwenzako alafu uone Mungu atakupangia uzae mtu mrefu, hakuna
Mungu kama huyo.

Ukioa au kuolewa na mtu mwenye uwezo wakati ninyi hamna uwezo watoto wenu watatoka na damu mchanganyiko.

2. BADILISHA IMANI
Imani ya Masikini na imani ya matajiri ni vitu viwili tofauti, mbingu na ardhi. Wakati masikini wanaamini kesho ni nzuri kuliko leo, tajiri anaamini leo ni nzuri kuliko kesho. Tajiri anaitumia leo aliyonayo kuipata kesho asiyonayo. Masikini anataka kuitumia kesho anayoiamini ni nzuri kuliko leo na kuacha kuitumia leo aliyonayo. Mwisho wake anaishia kuwa masikini.

Masikini anaamini Mungu ndiye amepanga maisha yake, wakati tajiri anaamini yeye ndiye mpangaji wa maisha yake. Imani ya masikini ya kuamini upande wa pili(Mungu) ndiye mpangaji wa maisha umejijenga zaidi kuhalalisha umasikini wake, yaani ni kisingizio cha kujihami, imani hii baadaye huleta malalamiko na lawama. Masikini ni mtu wa lawama na hii inatokana na imani yake hiyo.

Tajiri haamini upande wa pili unaweza muamulia maisha yake, tajiri anaamini yeye ndiye muamuzi wa maisha yake. Hii inamfanya Tajiri kutokuwa na lawama kwa mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe. Tajiri hamuachii Mungu, lakini masikini anamuachia Mungu.

Badilisha imani lakini usisahau kuchanganya damu na watu wenye utajiri.

Kwa leo niishie hapa;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro

Mwenye masikio na asikie, kisha ajikomboe!
 
Umasikini ni takataka

Hakuna ufahari wowote ule kwenye umasikini, kabla hatujaendelea jua hilo.

Umasikini ni wimbi linalobeba takataka nyingi ndani yake
1)Njaa
2)magonjwa
3)kudhalilika
4)Elimu duni
5)makazi duni
6)mavazi duni
7)nk

Happy ni nini??
_Happy ni hali ya kujisikia vizuri, hulu, amani and all good condition zipo ndani ya Happy, Happy sio Subset ya umasikini wala utajiri...unaweza kuwa maskini ukawa Happy na unaweza kuwa tajiri ukawa happy and Vice-versa.

Kuna vitu vingi vinavyosababisha mtu asiwe na furaha most of them ni vitu vibaya na vitu vingi vibaya vipo kwenye Maskini, Maskini automatically.

Shida zinazomkumba masikini akakosa furaha
*Ana Ada yang shule
*mtoto anaumwa Hana PESA ya matibabu
*nyumba ipo bondeni mvua inanyesha halali mafuriko yakija anabeba godoro kujihifadhi Mchikichini Secondary
*Mlo mmoja kwa siku kawaida au kupita wima
*kudhalilishwa madeni
*nk nk

Unakiwaje Happy katika shida hizo zote au wewe mwenzetu mwanao akiumwa ukakosa pesa ya hospital unakuwa na furaha.

Hitimisho
_kila mtu anaweza kuwa na furaha au kutokuwa nayo ila kwenye Maskini na tajiri, Asilimia 99% ya masikini hawana furaha kwa matajiri ni asilimia ndogo sana wasio na furaha 10% tu.

Hivi hawa wanapata wapi utulivu wa nafsi 👇


Nadhani ndicho hicho hicho nilichoelezea ila wewe conclusion yako ndiyo sikubali.
1. Mimi sikusema umaskini ndiyo furaha wala sikusema utajiri ndiyo huzuni. Nimejitahidi kuonya baadhi ya watu wanaodhani utajiri ni kila kitu na umaskini ni kukosa kila kitu (kama wewe).
2. Sasa kama unakubali kuwa ''happiness'' siyo subject ya umaskini wala utajiri, inakuwaje tena ufanye conclusion kuwa asilimia 90 ya maskini hawana furaha? Nilichokuwa nasisistiza mimi ni ile mtu kudhani akishakuwa tajiri basi kinachofuata automatically ni ''happiness''.
 
Nadhani ndicho hicho hicho nilichoelezea ila wewe conclusion yako ndiyo sikubali.
1. Mimi sikusema umaskini ndiyo furaha wala sikusema utajiri ndiyo huzuni. Nimejitahidi kuonya baadhi ya watu wanaodhani utajiri ni kila kitu na umaskini ni kukosa kila kitu (kama wewe).
2. Sasa kama unakubali kuwa ''happiness'' siyo subject ya umaskini wala utajiri, inakuwaje tena ufanye conclusion kuwa asilimia 90 ya maskini hawana furaha? Nilichokuwa nasisistiza mimi ni ile mtu kudhani akishakuwa tajiri basi kinachofuata automatically ni ''happiness''.
Kwanini unauliza kuhusu conclusion ya 90% as if ujaelewa nilochochambua kwenye main body.

Kwanini kila unapoona Mada au suala linalohusu utajiri ulete masuala ya 'furaha' kwanini hukuleta masuala ya 'kulala' kuna uhusiano gani.

No nani humu aliyesema akipata utajiri atakuwa total happiness nilichoona Mimi watu wanajdiri umasikini na utajiri tu sasa hili suala la 'Furaha' kwenye mada limetokea wapi...bilashaka jibu umelileta wewe hapo sasa swali kwanini ulilete ni 'Sentensi za maskini na kimasikini kuendeleza dhima zao za kuuchukia utajiri'.

Kwanini nimeshambulia sana 'jambo la furaha' si furaha tu kuna visentensi vingi sana kwenye mada zinazohusu utajiri...utasikia 'wote tutakufa' ni ipi mantiki ya kuzungumzia 'Kifo' kwenye mada inayohusu utajiri.

Jibu mpaka sasa huna mantiki yoyote ya kuleta mambo ya Furaha kwenye mdahalo huu hii ina collorate kuwa una spirit ya kumtetea takataka umasikini.
 
Ukweli mchungu mkuu tusikubali kuoa au kuolewa na masikini ni laana
 
Ni kweli kabisa uliyonenea hujakosea hata kidogo...

Kuna mtu nilionana nae katika salama nikamuuliza maisha yanasemaje... akajibu bila kusita maisha nimazuri sana... nilipenda jibu...

Shunie pitia hapa kuna chakujifunza...
Hii Sasa Ni hatua moja wapo ya kufanikiwa
 
Umasikini ni mada pana sana na inahitaji mjadala mpana sana.....andiko la mtoa mada ni dokezo tu la huo mjadala mpana wa umasikini.......lakini kujikwamua kunategemea vitu vingi sana na mojawapo ni
(1) Fikra
( 2) Nidhamu
(3) Bidii

1) Fikra
-Unahitaji uchanganuzi yakinifu ya fikra na tafakuri juu ya mazingira yanayokuzunguka na changamoto zake ili uweze kutambua namna ya kujikwamua.....

2) Bidii
-Baada ya uchanganuzi wa fikra na kujua njia za kukabiliana na hizo changamoto zinazokuzunguka....unahitaji kuwa na bidii kwenye kuzitatua au kuziendea changamoto hizo......

3) Nidhamu
-Nidhamu ni sehemu muhimu sana kuelekea kwenye kujikwamua kutoka katika umaskini.....unatakiwa kuwa na Nidhamu ya muda na kipato ili uweze kufikia malengo yako.........

Bado huu mjadala ni mpana sana na unahitaji mawazo yakinifu.......karibuni wadau.....
Mimi binafsi nakubalina nawe kwa asilimia zote namna ulivyowasilisha comment hii ndio uhalisia.

Umaskini na utajiri kwa namna zake mjadala wake sio mrahisi au mwepesi Kama hii mada iliopo.

Lakini tunaweza kuu summarise Kama wewe ulivyowasilisha hapa, na hii ni hatua ya mwanzo.
 
Nimezaliwa kwenye familia masikini lakini sasa hivi nina helaa sidhani kama nitakufa masikini au kufirisika.
Umenielewa vyema mtoa mada !?? Amesema kwamba Kama umezaliwa katika Koo masikini halafu katika ukoo wenu mliofanikiwa kuwa na uchumi mkubwa mkiwa wawili halafu wale masikini wakiwa Ni wa 5 hiyo I nakufanya uendelee kubaki kuwa unatoka katika family ya kimasikini Yaani ukwasi wako ulionao haiwezi kukusafisha na kukufanya uonekane unatoka katika family tajiri

Binafsi nimemuelewa sana mleta thread

Serikali impe ulinzi haraka Sana
 
Hakika wewe ndiye uliye-summarize vizuri. Umaskini uko zaidi kwenye culture za jamii. Jamii inaishije? Nini kinasemwa kama mafanikio kwenye jamii? kuna vitu vidogo vidogo ndani ya jamii ambavyo ndiyo huamua bidii za mtu. Kama mtu alizaliwa kwenye jamii na akaona wanaokwenda mjini kuomba ndiyo husemwa wana mafanikio basi ni rahisi na yeye kuishia kuomba. Kwa maoni yangu kuondoka na hii visual circle ni kupata elimu sahihi na exposure kwenye jamii nyingine. Nasema elimu sahihi kwa sababu unaweza kuwapa watu elimu isiyo sahihiu na isisaidie chochote au ikazidisha tatizo.
Well said
 
Kuna umaskini wa mali.
Umaskini wa akili.
Umaskini wa roho.

Katika maisha hakuna kitu muhimu kama amani ya rohoni na moyoni. Kulala usingizi bila kushtukashtuka. Na maskini wengi hatuna usingizi wa mang'amung'amu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Nimecheka Sana

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Screenshot_20210228-155653~2.jpg
 
Back
Top Bottom