Umasikini wa mtoto umefungwa ndani ya fikra na akili ya mzazi! Tusiwalaumu watoto tu wakati mwingine!

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Umasikini umefungwa ndani ya fikra na akili ya mtu. Wazazi kama fikra zao ni za kimasikini huwa na uhakika uzao wake wote watakuwa masikini. Katika jamii ninayoishi kuna watoto wengi ambao tunawasomesha shule za umma na za binafsi.

Sasa hizi shule za umma (za Serikali) kutokana na changamoto za shule, wazazi wanaojitambua uanzisha kamati/jukwaa la wazazi ili wajiongeze na kuchangia mapungufu ya pale serikali imeshindwa kufanya. Kuna maeneo kama uhaba wa madawati, uhaba wa waalimu, chakula cha watoto wawapo shuleni (kwa shule za msingi na sekondari za kutwa).

Wazazi wanaojielewa utoa michango waliyokubaliana. Sasa kuna hawa wazazi wenye fikra za kimasikini ambayo wao wanajua ukishampeleka mtoto shule za serikali baasi kila kitu kitafanywa na serikali. Wote tunajua matokeo yakitoka wanafunzi wengi wanafeli kwa wasitami wa “D” kwa shule za msingi au Dv. 0 au Div. 4 kwa sekondari.

Sasa hawa wazazi ambao walikuwa na mdomo mrefu kukataa kuchangia hela ndogo tu elfu 10, 20, 30 kwa shule za msingi au elfu 120, laki, 80, 60, nk kwa shule za serikali wakilalamika eti laki na 20 ni kubwa mno kwa kidato cha 5 na cha 6 kufidia mapungufu ya uhaba wa walimu na miundombinu wezeshi. Sasa mwanao akifeli kwa kupata Dv. 0 au Div. 4 hapo wapi kuna gharama kubwa?

Wee mzazi unaambiwa changia kiasi kidogo kwa ajili ya mwanao anabwabwaja maneno “hiyo hela ni nyingi!!!! mbona serikali ilisema elimu bure!!!! Mimi sitoi!!!! Haya sasa mwanao kamaliza shule na matokea wastani “D” hawezi kwenda hata shule za kata!!! Haya!!!! matokeo ya kidato cha 4 au 6 kapata Div 0/4 zigo hilo hapo pambana nao ndo uone gharama wapi kuna gharama kubwa kati ya kutoa mchango waliokubaliana wazazi au kupambana na Div. 0/4 ya mwanao??? Pia mwanao akifaulu ufaulu hafifu wa Div. 3 kuna kupelekwa vyuo mbalimbali lakini kwa kuchangia.

Mwanao kafaulu ufaulu hafifu Div. 3 kapelekwa vyuo vya ufundi na unaadikiwa karo laki 7 hadi milioni 2 kutegemeana na chuo. Haya pambana na hilo zigo wewe uliyekuwa unaona laki moja mchango wa wazazi ni mkubwa! Kalaghabao!
 
Ukiona mzazi/mlezi anawaza eti mtoto kuijua hela ni kosa jua huyo anamchimbia shimo la umasikini mwanae.

Mtoto ni lazima aifahamu hela na afahamu thamani yake, sio mtoto akipewa shilingi 100 anaanza kuona kama vile inauwezo wa kununua duka zima la mangi, lazima ajue hii ni shilingi 100 ya kachori 1 nikitaka kachori 3 niombe shilingi 300.

Wazazi/walezi wengi wa kiafrika ni waoga watoto wao wakiijua thamani halisi ya hela, hili ni bonge ya kosa
 
Haswaah!
 
Mshua alikataa kulipa ela ya chakula nikiwa form one, alikua ananipa jero daily ya kula shule.
Aisee enzi hizo jero ni jero kweli, kwakweli nilitaman msimamo wake wa kutolipa msosi uendelee..
 
Mshua alikataa kulipa ela ya chakula nikiwa form one, alikua ananipa jero daily ya kula shule.
Aisee enzi hizo jero ni jero kweli, kwakweli nilitaman msimamo wake wa kutolipa msosi uendelee..
Kwanini mkuu? Hujui hiyo jero aliyokataa ilikurudisha nyuma? Ulipata Division gani kutokana na kushinda njaa?
 
Ingekuwa elimu ni bure wao wasingepeleka watoto wao shule za saint
Haswaaa! Wazazi tuchukulie fursa ya watoto kwenda shule tuchangie kidogo watoto watimize ndoto zao! Wakati mwingine wazazi tunazima ndoto za watoto kwa ubinafsi wetu! Hiyo elfu 10 hujui ikichangwa na elfu 10 ya mzazi mwingine inawezesha kukodi mwalimu wa hisabati ili mwanao afaulu!!! Ukikataa kuchangia kutokana na makubaliano ya wazazi, serikali haiumii badala yake watakuletea zigo la mwanao lililofeli na kukubwagia nyumbani kwako upambane nalo! Shituka!!
 
Kwanini mkuu? Hujui hiyo jero aliyokataa ilikurudisha nyuma? Ulipata Division gani kutokana na kushinda njaa?
Hujaelewa, hakukipa chakula cha shule alikua ananipa jero.
Sasa jero inanirudisha vipi nyuma ndgu??
 
Nikajua unaongelea kwenye mkitadha mwingine kama wazaz kuwazuia watoto wao kushiriki kwenye shughuri za uzalushaji mali i. E biashara za familia ama wale wazaz wanaogoma kuwapa mitaj watoto wao kwa madai ya walisha somesha ikaisha, kumbe ni michango shuleni!! Waliosoma weng walichanga sana lakini hakuna cha maana kilichobadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…