Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Umasikini umefungwa ndani ya fikra na akili ya mtu. Wazazi kama fikra zao ni za kimasikini huwa na uhakika uzao wake wote watakuwa masikini. Katika jamii ninayoishi kuna watoto wengi ambao tunawasomesha shule za umma na za binafsi.
Sasa hizi shule za umma (za Serikali) kutokana na changamoto za shule, wazazi wanaojitambua uanzisha kamati/jukwaa la wazazi ili wajiongeze na kuchangia mapungufu ya pale serikali imeshindwa kufanya. Kuna maeneo kama uhaba wa madawati, uhaba wa waalimu, chakula cha watoto wawapo shuleni (kwa shule za msingi na sekondari za kutwa).
Wazazi wanaojielewa utoa michango waliyokubaliana. Sasa kuna hawa wazazi wenye fikra za kimasikini ambayo wao wanajua ukishampeleka mtoto shule za serikali baasi kila kitu kitafanywa na serikali. Wote tunajua matokeo yakitoka wanafunzi wengi wanafeli kwa wasitami wa “D” kwa shule za msingi au Dv. 0 au Div. 4 kwa sekondari.
Sasa hawa wazazi ambao walikuwa na mdomo mrefu kukataa kuchangia hela ndogo tu elfu 10, 20, 30 kwa shule za msingi au elfu 120, laki, 80, 60, nk kwa shule za serikali wakilalamika eti laki na 20 ni kubwa mno kwa kidato cha 5 na cha 6 kufidia mapungufu ya uhaba wa walimu na miundombinu wezeshi. Sasa mwanao akifeli kwa kupata Dv. 0 au Div. 4 hapo wapi kuna gharama kubwa?
Wee mzazi unaambiwa changia kiasi kidogo kwa ajili ya mwanao anabwabwaja maneno “hiyo hela ni nyingi!!!! mbona serikali ilisema elimu bure!!!! Mimi sitoi!!!! Haya sasa mwanao kamaliza shule na matokea wastani “D” hawezi kwenda hata shule za kata!!! Haya!!!! matokeo ya kidato cha 4 au 6 kapata Div 0/4 zigo hilo hapo pambana nao ndo uone gharama wapi kuna gharama kubwa kati ya kutoa mchango waliokubaliana wazazi au kupambana na Div. 0/4 ya mwanao??? Pia mwanao akifaulu ufaulu hafifu wa Div. 3 kuna kupelekwa vyuo mbalimbali lakini kwa kuchangia.
Mwanao kafaulu ufaulu hafifu Div. 3 kapelekwa vyuo vya ufundi na unaadikiwa karo laki 7 hadi milioni 2 kutegemeana na chuo. Haya pambana na hilo zigo wewe uliyekuwa unaona laki moja mchango wa wazazi ni mkubwa! Kalaghabao!