Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Mwalimu wangu wa civics kidato cha kwanza alini fundisha kuwa Human basic needs ni shelter, food and clothes.

Sijui nime eleweka?
 
Sijui ni mimi nimemuelewa tofauti mleta mada au laaaah.....ila ninachoamini ni kwamba sio lazima nyumba iwe kipaumbele cha kwanza kama watanzania tulio wengi tunavyoamini na mwisho inakua kama mateso kulitimiza hili takwa, unakuta mtu anajinyima kupitiliza ili ajenge kwa kudunduliza hata kwa miaka kumi na wengine hushindwa kabisa kuzimalizia nyumba zao.

Suala ni kwamba kipaumbele kiwepo palipo msaada wa kukuvusha kwanza ulipo halafu hayo mengine yatakuja baadaye. Let say mtu amepata milioni kumi from nowhere kama ni kwenye urithi or whatever halafu anakimbilia kuanza kujenga nyumba ambayo itamgharimu may be 30mil., hyu ataanza na kiwanja, msingi halafu hafiki popote anaanza kupigika ila hii hii milioni kumi km angeiwekeza sehemu sahihi after 2 to 3 years angekua na uhakika wa kujenga na kumaliza kwa wakati.
 
Nikefurahi sana maana unaongea kama tumechunga kondoo wote. Day dreaming njema
 
Nilipata kazi. Nikajenga nyumba ya mama kule home, nikamaliza nikanunua gari la kutembelea. Kuna wastani wa milioni 55 imelala kwenye vitu ambavyo haviniingizii chochote (directly).

Indirectly napata amani wazazi kua na nyumba yao na mimi kupiga misele ya michakato yangu. Ila am sure hiyo pesa ningeiweka sehemu fulani nzuri ingekua inanipa hata milioni moja kila mwezi.
 
Kuna rafk angu ameajiriwa kama miaka 6 nyuma hivi kuna siku ananiambia eti hataki kupoteza gharama zisizo za msingi rangi na gypsum na ile plasta anapiga mwenyewe sio kazi alienda kwa fundi akamuona siku moja akasema anafanya mwenyewe na kweli kafanya,ila hii yote ni kutokuwa na pesa ndio mawwzo kama haya ya kufanya mwenyewe yanakuja badala ya kuita mtaalamu afanye kitu cha uhakika huku akiwa na experience ya muda mrefu.

Kujenga bhana unajenga unaona hasa kwamba umejenga.

Kuna mzee wangu wa karibu anajenga pale kivule ukiangalia unasema yaas huyu mzee kajenga bhana na nyumba haijamaliza mpaka hii leo anafanya kitu uhakika unaona kazi kazi kweli.
 
Ni ukweli mtupu,
Sema kuna baadhi ya watu wapo na vision za kuzaliwa. Yupo mzee mmoja sasa yupo Likizo ya kustaafu, nyumba ya kuishi aliyojenga ndo anaimalizia sasa huko nyuma yeye ilikuwa ni kusimika miradi, biashara, kujenga nyumba za kupangisha mfano frames, Bar etc.... leo anamalizia nyumba yake kutoka kwenye pesa anazopata kutokana na biashara zake.

Gari alilokuwa nalo ni pickup kwa ajili ya biashara zake.

Last 6 months amegiza gari ya kutembelea lk iliyotokana kipato cha biashara.

I guess jamaa ataishi kama mfalme fulani katika maisha yaliyobaki.

Watanzania walahi tubadilike pesa tunazopata hazitoshi kumaliza nyumba, matokeo yake nyumba unaijenga miaka 7-20. Poor planing and wastage of resources.
Mungu atusaidie
 
Biashara yenyewe unaweza kuweka hela ikaisha bora kujenga
 
Huyu jamaa itakuwa anakaa home mambo safi hajui tabu za kupanga
 
Natamani ningekua mpangaji wako mkuu
 
Nilikua na akili kama uisemayo hapo,
Kwanza kumiliki gari, biashara na nyumba baadae,
Kama zali ndoto yangu ya kwanza ikatiki nkamiliki gari japo lilikua la bei rahisi, na nkafanikiwa kumiliki biashara pia, plan ya kujenga ilikua itokane na biashara zangu lkn kutokana usimamizi m'bovu wa niliowaamini wasimamie wakaziua zote, biashara 4 zote zilikufa kwa vipindi tofauti nkaanza kujuta bora ningenunua viwanja nkajenga, matokeo yake nimekuja kujengea ela ya kazini pamoja na shughuli zangu nyingine ambazo naziendesha mwenyewe..........

Yaani waafrica tunarudishana sana nyuma kimaendeleo, unamwajiri mtu badala awaze kufanya kazi kwa uadilifu anawaza kumiliki biashara kama ya mwajiri wake ndani ya miaka mi2 wakati boss wake kaitafuta kwa zaidi ya miaka 10.

Kiukweli nchi hii na nyingi za kiafrica hakuna tatizo la ajira hata kidogo, shida ipo kwa waajiriwa wenyewe sio waaminifu,
Kuna matajiri wengi wana uwezo wa kufungua maduka, viwanda, kulima na mengineyo lkn akiwaza uaminifu ulio sifuri kwa watanzania 99% anaamua bora ela yake ibaki bank au ajenge tu majumba ovyo.
 
Kweli kabisa
 
Haujanielewa
 
Mwalimu wangu wa civics kidato cha kwanza alini fundisha kuwa Human basic needs ni shelter, food and clothes.

Sijui nime eleweka???
Sina nyumba na napata mahitaji yote matatu
 
Wahindi woga wao tu wa kutaifishwa vitu

ss haiwezekani tuishi kama wahindi nchini kwetu wenyewee!!watu kila mtu ajinafasi kadri Mungu alivyomjalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…