Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Mwalimu wangu wa civics kidato cha kwanza alini fundisha kuwa Human basic needs ni shelter, food and clothes.

Sijui nime eleweka?
 
Sijui ni mimi nimemuelewa tofauti mleta mada au laaaah.....ila ninachoamini ni kwamba sio lazima nyumba iwe kipaumbele cha kwanza kama watanzania tulio wengi tunavyoamini na mwisho inakua kama mateso kulitimiza hili takwa, unakuta mtu anajinyima kupitiliza ili ajenge kwa kudunduliza hata kwa miaka kumi na wengine hushindwa kabisa kuzimalizia nyumba zao.

Suala ni kwamba kipaumbele kiwepo palipo msaada wa kukuvusha kwanza ulipo halafu hayo mengine yatakuja baadaye. Let say mtu amepata milioni kumi from nowhere kama ni kwenye urithi or whatever halafu anakimbilia kuanza kujenga nyumba ambayo itamgharimu may be 30mil., hyu ataanza na kiwanja, msingi halafu hafiki popote anaanza kupigika ila hii hii milioni kumi km angeiwekeza sehemu sahihi after 2 to 3 years angekua na uhakika wa kujenga na kumaliza kwa wakati.
 
Sihitaji kuwa tajiri mimi ni mtumishi wa Serikali. Nina biashara kubwa Kariakoo na Mlimani City pia nina nyumba za kupangisha pamoja na mashamba na mifugo. Kwa upande wangu naona nimefanikiwa kwani nina uhakika ni watanzania wachache wenye maisha kama yangu.

Ninaijua biashara nina uhakika zaidi yako. Kabla awamu hii nimeenda China mara 17 kibiashara. Na kwangu mimi biashara ya nyumba ndio ina uhakika mkubwa wa mapato kuliko zote kwani haina supervision kubwa na haikuathirika na corona wala Kodi za TRA
Nikefurahi sana maana unaongea kama tumechunga kondoo wote. Day dreaming njema
 
Nilipata kazi. Nikajenga nyumba ya mama kule home, nikamaliza nikanunua gari la kutembelea. Kuna wastani wa milioni 55 imelala kwenye vitu ambavyo haviniingizii chochote (directly).

Indirectly napata amani wazazi kua na nyumba yao na mimi kupiga misele ya michakato yangu. Ila am sure hiyo pesa ningeiweka sehemu fulani nzuri ingekua inanipa hata milioni moja kila mwezi.
 
Mkuu Tatizo sio tuu kujenga tatizo unajenga nini...
Nikijenga Sasahivi Nitajenga upuuzi tuu.

Hicho kitu SITAKI, nimeandika kwa herufi kubwa kama msisitiozo,
Kuliko kujenga kijumba hakieleweki Miaka hii bora niishie kupanga,

Ila siwezi jenga nyumba kama aliyojenga babu miaka ya 60s, Narudia bora niishie kupanga kuliko kuchafua ardhi.

Masuala unajenga nyumba yako, Unaiongelea mbele ya wenzako baada ya kuita nyumba unaita Kibanda(na kweli unamaanisha) mimi siwezi.

Nikitaka hicho kibanda eti ilimradi nijiegamize kwangu hata leo naweza na wengi humu naamini wanaweza...
Ila maisha ya leo kuishi kinyonge kuanzia ndani mpk nje hapana.
Kuna rafk angu ameajiriwa kama miaka 6 nyuma hivi kuna siku ananiambia eti hataki kupoteza gharama zisizo za msingi rangi na gypsum na ile plasta anapiga mwenyewe sio kazi alienda kwa fundi akamuona siku moja akasema anafanya mwenyewe na kweli kafanya,ila hii yote ni kutokuwa na pesa ndio mawwzo kama haya ya kufanya mwenyewe yanakuja badala ya kuita mtaalamu afanye kitu cha uhakika huku akiwa na experience ya muda mrefu.

Kujenga bhana unajenga unaona hasa kwamba umejenga.

Kuna mzee wangu wa karibu anajenga pale kivule ukiangalia unasema yaas huyu mzee kajenga bhana na nyumba haijamaliza mpaka hii leo anafanya kitu uhakika unaona kazi kazi kweli.
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto zenu za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Ni ukweli mtupu,
Sema kuna baadhi ya watu wapo na vision za kuzaliwa. Yupo mzee mmoja sasa yupo Likizo ya kustaafu, nyumba ya kuishi aliyojenga ndo anaimalizia sasa huko nyuma yeye ilikuwa ni kusimika miradi, biashara, kujenga nyumba za kupangisha mfano frames, Bar etc.... leo anamalizia nyumba yake kutoka kwenye pesa anazopata kutokana na biashara zake.

Gari alilokuwa nalo ni pickup kwa ajili ya biashara zake.

Last 6 months amegiza gari ya kutembelea lk iliyotokana kipato cha biashara.

I guess jamaa ataishi kama mfalme fulani katika maisha yaliyobaki.

Watanzania walahi tubadilike pesa tunazopata hazitoshi kumaliza nyumba, matokeo yake nyumba unaijenga miaka 7-20. Poor planing and wastage of resources.
Mungu atusaidie
 
Kama kujenga ni umasikini, je, wenye nyumba ni masikini?

Je, ambao hawajajenga ni matajiri?

Maelezo yako hayana logical sequence.

Mfano,

Kujenga ni umasikini

Kupanga ni utajiri

Wenye nyumba ni masikini? Hapana

Wapangaji ni masikini? Hapana

Basi, kuwa tajiri haimaanishi kwamba una nyumba au huna na au unepanga.

Kwa hiyo kuwa na nyumba siyo sababu ya utajiri wala umasikini.

Wapo matajiri wasio na nyumba. Hawa wengi wapo mjini.

Wapo masikini pia wana nyumba. Wengi wa vijijini.

Mtoa mada tafuta tafsiri sahihi ya umasikini.
Huyu jamaa itakuwa anakaa home mambo safi hajui tabu za kupanga
 
Hapana mie napenda tu ujenzi. Niliona biashara easy kwangu ni kujenga na kupangisha watu (real estate) haina stress kama biashara nyingine na pia unaifanya huku unaendelea na kazi zake za kuajiriwa. All in all mtu ukiwa na makazi yako inakuondolea sana usumbufu ingawa katika stage fulani ya maisha lazima upange ila mambo yakikaa sawa jenga. Wapangaji wangu wengi nawashauri hivi.
Natamani ningekua mpangaji wako mkuu
 
Nilikua na akili kama uisemayo hapo,
Kwanza kumiliki gari, biashara na nyumba baadae,
Kama zali ndoto yangu ya kwanza ikatiki nkamiliki gari japo lilikua la bei rahisi, na nkafanikiwa kumiliki biashara pia, plan ya kujenga ilikua itokane na biashara zangu lkn kutokana usimamizi m'bovu wa niliowaamini wasimamie wakaziua zote, biashara 4 zote zilikufa kwa vipindi tofauti nkaanza kujuta bora ningenunua viwanja nkajenga, matokeo yake nimekuja kujengea ela ya kazini pamoja na shughuli zangu nyingine ambazo naziendesha mwenyewe..........

Yaani waafrica tunarudishana sana nyuma kimaendeleo, unamwajiri mtu badala awaze kufanya kazi kwa uadilifu anawaza kumiliki biashara kama ya mwajiri wake ndani ya miaka mi2 wakati boss wake kaitafuta kwa zaidi ya miaka 10.

Kiukweli nchi hii na nyingi za kiafrica hakuna tatizo la ajira hata kidogo, shida ipo kwa waajiriwa wenyewe sio waaminifu,
Kuna matajiri wengi wana uwezo wa kufungua maduka, viwanda, kulima na mengineyo lkn akiwaza uaminifu ulio sifuri kwa watanzania 99% anaamua bora ela yake ibaki bank au ajenge tu majumba ovyo.
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto zenu za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Kweli kabisa
 
Hivi Watoto wakiwa wakubwa watajivunia lkipi Kati ya nyumba ya mzazi wao au biashara ya mzazi ?

Ulishasikia Watoto wa Reginald Mengi wanajivunia nyumba ya mzazi wao? Wanajivunia biashara sio nyumba

ulishasikia Watoto wa Bakheresa wanajivunia nyumba ya mzazi wao ? Wanajivunia biashara

Wewe unajivunia nyumba ya mzazi wako?
Haujanielewa
 
Mwalimu wangu wa civics kidato cha kwanza alini fundisha kuwa Human basic needs ni shelter, food and clothes.

Sijui nime eleweka???
Sina nyumba na napata mahitaji yote matatu
 
Wahindi woga wao tu wa kutaifishwa vitu

ss haiwezekani tuishi kama wahindi nchini kwetu wenyewee!!watu kila mtu ajinafasi kadri Mungu alivyomjalia
 
Back
Top Bottom