Lazaro Nyalandu anafanya kazi nzuri sana, juzi nilikuwa Kindai karibia mkoa wote wa Singida ni Chadema tu, muda huu ninaoandika... No hate No fear
View attachment 1415752
Mkuu 'imhotep',
Samahani sana mkuu wangu, kwa sababu inachanganya sana namna hii.
Huyu ni Nyalandu, anafanya mkutano wa hadhara? Lini, na wapi?
Haya maswali ukiyajibu kwa ukweli, nitaelewa, lakini ndio akili yangu itaongezeka kuchanganyikiwa juu ya hili.
Hilo ni moja.
Pili.
Hivi huko CHADEMA yupo Nyalandu peke yake, Tanzania nzima; na wala siyo mbunge basi!
Hawa wengine wote wapo wapi?
Tunawajua wanaoshinda mahakamani na magerezani kiasi kwamba hawana nafasi kama aliyonayo Nyalandu. Hawa wengine wooote wako wapi?
Tusipeane sababu na visingizio za ushabiki wa chama. Tuelezeni tu kiuhakika kwa nini awe Nyalandu pekee ndiye aonekane kuwa imara. Akina Wenje wapo wapi? Na wengi wengine waliowahi kuwa viongozi ndani ya chama. Mbona hawaskiki.
Au wanasubiri uteuzi ndio waanze kazi ya kukijenga chama?
Ndio maana nikamwandikia rafiki yangu Erythro hapo juu, kwamba wakati wa mchujo, msikose kutafuta msaada wa mawazo ya watu. Mnao ma'opportunists' wengi sana ndani ya CHADEMA