nilisha sema exodus ni myth hamutaki kusikia hebu rejeab hapa
https://www.jamiiforums.com/dini-imani/733371-exodus-is-a-myth-3.html
Kwanini exodus ni myth (Kumbuka wamisri ni watunza kumbukumbuku wazuri sana)
1. hakuna ushahidi wowote kwa wamisri kuwa walishawahi kuwaruhusu wageni wengi kama 600,000 kuondoka.
2. wakiwa sinai inasemekana watu 3000 waliuwa kwa uvou lakin hakuna hata fuvu moja la ushahidi la binadamu wala mnyama.
3. mapigo kumi kama ilivyoandikwa kwenye bible haijawa documented mahali popote kwenye historia ya misri ajabu eeh tukio kubwa kama hilo.
4. ajabu jingine kuangamizwa na jeshi lote la misri baharini hili tukio halipo kwenye historia ya misri wala archeology haisapoti tukio hilo kumbuka uadui katai ya misri na nchi kama libya,assyrians,KUSHI enzi hizo kuangamizwa kwa jeshi lao kungeleta maafa sana kivita lakini hakikutokea kitu.
5. hakuna uhusiano wa culture kati ya wamisri na wa israel jambo la ajabu watu muishi kwa miaka 400 msifanane culture.
6. baadhi ya miji iliyotajwa kwenye exodus haikuwepo mingine ilikuwepo lakini ilkuwa na idadi chache sana ya watu na haikuwa na ngome kama ilivyoonyeshwa kwenye bible
7. inaonyesha farao aliyeongea na mussa pindi akiwa na 80 yrs ndo farao huyo huyo ambae binti yake alimuokota mussa. wa misri wanadai hakuna farao ambae aliishi muda mrefu kiasi icho only peppi alitawala kwa miaka 94 na hafiti hapo.
8. kanani ilikuwa inatawaliwa na misri kwa hiyo wa israel kuondoka misri kwenda kanani ni sawa na wamakonde kutoka dar es salaam kwenda mtwara kuanzisha nchi yao hapo ni kujitafutia vita na serikali ya tanzania hiyo hiyo wanayoikimbia dar.
9. rejea namba 8 wamisri wanadai kanani ilikuwa inakaliwa na wa israel toka zamani na wala hawakuhamia hapo toka sehemu nyingine.
10. inadaiwa wa israel walikuwa wanafanya kazi ya kufyatua tofali kweli wamisri wanadai hakuna project kubwa iliyokuwa inahitaji tofali nyingi kiasi cha kuhitaji labor supply kubwa kiasi hicho.