Elungata, huwezi ku rule out Habari za Mungu kwa elimu yako ya archaeology. Archaeologist wameipindua dunia yote ya jangwa wakakosa fuvu? You must be kidding. Elimu yako ya Historia haiwezi kuwa juu ya Mungu eti ikuambie Mungu ni nani alianza lini, na kabla yake kulikuwapo mfalme wa aina gani baadaye, sijui zikaja nyota. Huna huo uwezo na naomba usijiaminishe kwa masuala ambayo hadi mwisho wa maisha yako hutakaa uyaweze. Historia unayoisema wewe ni ya kuanzia lini, halafu nani alikuambia huo muda ulikuwepo?
Hata mimi nilikariri habari za historia na evolution kama nilivyofundishwa darasani na nikafaulu mitihani. Lakini siwezi kutumia hiyo knowlege kusema Mungu hakuumba Mbingu na nchi, na kila kitu kilichomo. Na hili la pili (I mean spiritual context), ndiyo inabeba uhalisia kwa sababu siku zote haibadiliki. Lakini elimuz na taarifa za historia zinabadilika kila siku kulingana na nini kimegunduliwa na unakitazama kutokea angle gani.
Ninafikiri pia ulipaswa kujua nili respond kwa statements zipi niliposema huwezi Ku compete na Mungu. Kusemaa kuyaongelea mambo haya ni dhambi, pia inategemea na dhamira ya mwongeaji ambayo yeye tu ndiye shahidi. Ukijadili kwa kupanua wigo wa ufahamu, wala si tatizo. Lakini ukijadili kwa ku defend unachokielewa wewe ambacho kiko kinyume na Mungu, obvious hata moyoni mwako utakuwa unadhamira ovu mbele za Mungu. Hilo linabaki moyoni mwako.
Lakini pia unachosema hakuna ushahidi wa ki historia katika lipi? Kwamba Israel walikuwa Misri, Kwamba walitoka Misri kwa Mkono wa Nguvu wa Mungu, Kwamba walikuaa jangwani miaka 40 Kabla ya kufika kwao ama ni historia gani unayosema haipo. Haipo wapi? Na wewe historia yako unayoimini na kuisimamia unaipata wapi?