Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Hapa nafikiri tulipigwa changa la macho!! Kama wazee wa kibondei walitembea kutoka Tanga hadi Dar es Salaam kwa siku 6 kuunga mkono Azimio la Arusha, umbali wa km 326 huku wakiimba Daisaama ni hai kwa mwendo wa miundi(Dar es Salaam ni mbali kwa mwendo wa miguu) lakini walitoboa maana yake hizo km 600+ wangetumia less than 14 days!! Huo ni mchanga wa wazi kabisa..
 
Aya ya 26 imetoa majibu. Asante sana
 
Hi
 
Hi
Misri ya Leo sio Misri ya enzi za Musa, pia haimaanishi kuwa walikuwa wakisafiri kwa miaka yote hiyo, Kuna process kuweza kuachiliwa kutoka mtumwa hadi kwa huru

Tunaziomba hizo process tafadhari na Nina Imani ndiyo shida ya mtoa post kukua kwanini?
 
Sijapitia majibu ya watu wengine. Lakini safari ya Waisraeli kutoka Misri hadi Kanaani, iliyochukua miaka 40, ilitokana na sababu kadhaa zilizoelezwa vizuri katika maandiko ya Biblia (huhitaji reference ya vitabu vingine vilivyonakili mapokeo ya agano la kale), hasa katika Kitabu cha Kutoka na Hesabu:

1. Kutotii na Kukosa Imani: Sababu kuu ilikuwa kutotii kwa Waisraeli na ukosefu wa imani kwa Mungu. Walipofika karibu na Nchi ya Ahadi (Kanaani), Musa aliwatuma wapelelezi 12 kuichunguza nchi hiyo. Hata hivyo, wapelelezi kumi walirudi na ripoti ya kutia hofu, wakisema nchi imejaa majitu na miji yenye ngome imara, jambo ambalo liliwakatisha tamaa watu. Ni Yoshua na Kalebu pekee waliosadiki kwamba wangeweza kuiteka nchi kwa msaada wa Mungu. Kwa sababu ya ukosefu huo wa imani, Mungu aliamuru kwamba kizazi hicho (isipokuwa Yoshua na Kalebu) kisingeingia katika Nchi ya Ahadi (Hesabu 13-14).

2. Kutangatanga kama Adhabu: Kama adhabu kwa uasi wao na ukosefu wa imani, Mungu aliwafanya Waisraeli wenye umri wa kwenda vitani watangetange jangwani kwa miaka 40 hadi kizazi cha wazee kife. Hii ilikuwa kuhakikisha kuwa kizazi kipya, ambacho hakikuasi, kingeingia Kanaani.

Hes 14:26-33 SUV
[26] Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, [27] Je! Nichukuane na mkutano mwovu huu uninung’unikiao hata lini? Nimesikia manung’uniko ya wana wa Israeli, waninung’unikiayo. [28] Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi; [29] mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung’unikia, [30] hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliinua mkono wangu ya kwamba nitawaketisha humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. [31] Lakini Watoto wenu, ambao mlisema watakuwa mateka, ndio nitakaowaleta na kuwatia ndani, nao wataijua nchi ninyi mliyoikataa. [32] Lakini katika habari zenu, mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili. [33] Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arobaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hata mizoga yenu itakapoangamia jangwani.

3.
Maandalizi na Majaribio: Miaka 40 jangwani pia ilikuwa kipindi cha majaribio na ukuaji wa kiroho kwa Waisraeli. Walijifunza kumtegemea Mungu kwa mahitaji yao ya kila siku, kama chakula (mana) na maji, na kilikuwa kipindi cha kujitakasa kabla ya kuingia Nchi ya Ahadi (Kumbukumbu la Torati 8:2-5).

Hivyo, safari iliyochukua muda mrefu ilikuwa adhabu kwa kutotii, lakini pia kipindi cha maandalizi ya kiroho.
 
Hahaa haah ahaa! Mkuu lyinga umenichekesha sana. We unadhani walikuwa wanafanya nini miaka yote hiyo njiani.

Eti kama kulikuwa na mama mjamzito, then akajifungua alikuwa na uwezekano wa kupata mjukuu akiwa safarini .emegine!
...kumbe ndo maana walitumia miaka 40...walikuwa wanagonga hadi kutiana mimba...kwa hiyo walikuwa pia wanakaa kulea...by the way jangwani hakuna nyumba walikuwa wanagongania wapi!!
 
Kumbukumbu la Torati 8 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
³ Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.
⁴ Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini.
 
Hao walisha laaniwa kitambo hio creature haifai kwa mwanadam
 
Unaweza tembea dar to moshi bila kupumzika sehemu yeyotee ? Elewa neno kupumzika , hiyo miguu itakuwaj kama unatembea bila mapumziko ? Kama umeelewa utaacha kuuliza maswali ya kipuuz , kwenye watu zaid ya 100 lzm Kuna sehemu mtahitaj kupumzika ili muwe fit kuendele na safari
 
Watumishi wa Mungu wanavyoelezea hili hua wanasema watu wa zamani walikua na nguvu sana..

Kuna jamaa shabiki wa mpira hapa Tz alitembea Mbeya - Dar almost Chini ya wiki 1


Thanks Google 👇👇

Hata kama utapumzika, huwezi tembea Kilimanjaro dar kwa miaka 40, watu wa dini mna shida gani mmefunga akili zenu au?
 
Misri ya Leo sio Misri ya enzi za Musa, pia haimaanishi kuwa walikuwa wakisafiri kwa miaka yote hiyo, Kuna process kuweza kuachiliwa kutoka mtumwa hadi kwa huru
ungejikalia kimya ungepungukiwa nn
 
Soma Biblia yako vizuri,kuna sehemu walikuwa wanaweka vituo na wanakaa kwa miaka kadhaa kabla ya kuanza tena safari...
 
Kumben
Kumbe muuaji alafu anasema kuua dhambi.
Je kusamehe anakotaka ss tufanye ni kupi wakati yy alishindwa kuwasamehe..??

Yote hayo yanaonesha kuwa yy naye hajakamilika
 

Waisrael walisafiri kwa mpango maalum na waliongozwa na wingi maalum la Mungu​

Hesabu 9:17​

Wakati wowote wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, nao Waisraeli waliondoka; mahali popote wingu liliposimama, Waisraeli walipiga kambi.
 
Hata kama wangekuwa wanatembea kwa masaa 6 kisha kupumzika mpaka siku ingine inaanza ndio wachukue miaka 40?
Niambie wewe kuna kilomita ngapi toka cairo mpaka jerusalem?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…