Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Huwa nasoma maandiko yote yaliyombele yangu, yawe ya wasomi na wanamajumui ama ya wajinga na yakijinga, mimi husoma tu. Hii imenipa uwezo na ujasiri wakuyajua mambo mengi yaliyohifadhiwa kwa maandishi,

Lakini kuna jambo hakika kwa miaka mingi nimekuwa nikiumiza akili yangu bila kupata jibu, nimejaribu kuzama kiroho imeshindikana, nimejaribu kuzama kihistoria imeshindikana,

Umbali kati ya Misri na Israel ni km 613, kwamjibu wa Biblia inasema wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40, inamana kila siku walisafiri mita 43?

Mafanikio ya binadamu duniani hutazamiwa afikapo miaka 18-40. Inaelezwa kwamba huo ndio mwenendo pia wa mafanikio ya taifa...

Wanamajumui wanasema ukizidi umri huo wewe uwe unatafuta hela ya kula tu, utajiri na hekima utavisikia tu

Wachungaji naomba msaada wa ufunuo hapa hapa....
IMG-20160920-WA0176.jpg
 
Mtu msomi hawezi kuuliza huo ujinga. Tangu lini wachungaji waka wataalam wa kujua mafanikio ya kidunia? Na kama kweli wewe unasoma kila kitu ungejua watu wengi waliofanikiwa wakiwa na umri zaidi ya miaka 40.
 
Nafikiri inawezekana kutajirika baada ya kuvuka miaka 40 lakini kwa hakika ni vigumu mno. In fact huwezi kujiahidi au kuahidi watoto wako kuwapa utajiri baada ya kuvuka umri wa 40-45.
 
Mkuu Moderator naomba uweke sawa heading ya uzi huu iwe ni
"Hii ni tafsiri gani katika Safari?"
Mkuu ebu kuwa specific.Hilo swali lililokuumiza kichwa kwa miaka mingi ni lipi?.....ebu lifupishe kwa sentesi moja.

Maana mada yako kama ina ukakasi wa kuielewa kwa jinsi nilivyoiona.
 
Mbona biblia imeelezea kilicho fanya wasafiri kwa miaka 40 we sio msomaji wa vitu tofauti nina mashaka na ww hebu nenda ujifunze zaidi na kasoma katika biblia KUTOKA yote huoni hata biblia kila kitabu kinajieleza, KUTOKA maana kutoka misri
Huyu jamaa nahisi anaelezea kitu kingine kabisa, hyo habari ya israel anajaribu kuficha kitu anachotaka kusema..
usisome kwa haraka haraka

ngoja niendelee kufuatilia
 
Umbali kutoka Misri kwenda Israel ni kilomita 623 tu. Lakini Musa na kundi lake (wana wa Israel) walitumia miaka 40 kutembea hadi kufika nchi ya ahadi. Huu ni wastani wa kilomita 15 kwa mwaka, sawa na kilomita 1.25 kwa mwezi. Hii ni sawa na mita 42 tu kwa siku, yani umbali nusu ya uwanja wa mpira.

Moderators , mnamba ya simu ya Musa umlete hapa ajieleze, huu uvivu waliutoa wapi.

Sipendagi ujinga
 
Mtoa mada kabla hujauliza swali lako kuna vitu vingi unatakiwa ujiulize,
a) Idadi ya watu kwenye msafara.
Kwa vile walikuwa wengi, iliwabidi waende taratibu, mmoja wapo akipata tatizo ni lazima wamsubirie. Kundi lilikuwa kubwa ilibidi ifike sehemu watafute chakula.

b) Jiografia ya kati ya Misri na nchi ya ahadi, kuna jangwa,milima,mabonde,mito na bahari. Kutokana na hayo inabidi sehemu ya kutumia siku moja inabidi mutumie miezi kadhaa kuuzunguka mlima au kukwepa bonde. Kumbuka kizazaa walichokipata wakati wanavuka bahari ya shamu.

c) Umri tofauti katika kundi, kulikuwa na watoto wazee na vijana.

d) Aina ya usafiri waliokuwa wanautumia, fikiria unatembea kwenye jangwa itakuchukua muda gani kurudisha nguvu zilizopotea.

e) Muda wa ibada, kuna wakati Musa ilibidi aende mlimani(sehemu yenye utulivu) kusali na kuongea na Mungu, kumbuka Mungu hapangiwi muda,unaweza msubiri hata miezi 8 hajakujibu.

Mwisho kabisa ulikuwa ndio mpango wa Mungu watumie miaka 40 kufika nchi ya mito na maziwa. ATAKAYE VUMILIA MPAKA MWISHO HUYO NDIE ATAKAYEIONA NCHI MUNGU ALIYOWAAHIDI WATU WAKE
 
Back
Top Bottom