Umbo la mke wangu limebadilika baada ya kujifungua

Wala usisikitike. Mwanamme anaoa mwanamke akitegemea hatabadirika. Mwanamke anaolewa na mwanamme akitegemea atambadirisha. Mara nyingi matokeo yake ni kinyume na matarajio. Kaza moyo uishi na mkeo, ni wewe mwenyewe uliyemchagua na kuapa kuishi naye jua liwake au mvua inyeshe.
 
Kama ulimpendea umbo tu mzee ishakula kwako na bado apo wanakuwaga mabonge kama viboko.
Kuinusuru ndoa tafuta kitu kingine cha kumpendea haraka sana.
 
Yaani mwanamke ajifungue anenepe akafanyie surgery, akili ya wapi hiyo?
na akijifungua tena na tena???
Siku wanaume huwapeleka wake zao kutengenezwa shape baada ya uzazi tumbo
Linatolewa ndio ugharamike
 
Mtoto akikua anaweza kupungua ila kama hana stress itakua ngumu
 
Unakuta unaandika haya na wewe ukiwa na bonge moja la ndambi anyways , anzeni kufanya mazoezi na mzingatie diet.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Huu sasa ni utoto. Je mtoto ana kuvutia? Ukimuangalia mtoto unajisikiaje?
 
Kaa nae chini muongee, mwite mwambie baby let's talk man to man
ahahaha et man to man nimecheka mie jaman loooh JF is a nice place to be. ukiwa na stress chukua kiti sogea karibu na JF
 
Hukuwa unalitambua hili kabla hujaoa? Ni muda sasa umefika vijana wa kiume mfanyiwe kitchen party.
 
Huyo naweza kuwa namjua kama anafanya kazi, Niko naye offisini hapa.

Lakini ushauri Kwa wasiooa na wanatafuta mke na wanapenda wembamba. Usidanganyike Kwa Hali yake ya Sasa, Chungunza familia yake kwanza mama, dada, shangazi na Hata bibi zake. Ukiona wembamba Kwa level yako ya ustahimilivu chukua, maana na yeye akizaa uwezekano wa kuwa mnene kupitikiza ni nadra sana.

Kwa Sasa nakushauri mtengenezee mawazo aka stress akinyauka Kwa kiwango chako unaregeza kamba(jinsi ya kutengeneza stress si husiki)
 
DR SANTOS Dr Nyimwa ni kwamba lazima mwanamke awe mnene baada ya kujifungua au vipi?

Kitaalam hii imekaa vipi?

Changamoto kweli.
wakati wa ujauzito mwili huifadhi vimiminika (maji na damu)vya ziada ili kuwezesha ukuaji wa mimba hii hipelekea misuli ya tumbo kutanuka kabla na mara baada ya kujifungua( sasa hapa asipofanya mazoezi kutokana na lifestyle after birth hupelkea kuongezeka mwili

Pia mabadiliko homoni (yanaweza kukufanya unenepe ama ubaki kawaida tu)

Ikiwa homoni (estrogen &progesterone) zikiongezeka baada ya mwanamke kujifungua hufanya mwanamke anenepe na vice versa.
 
We ni ke au me!!, maana unajua mipasho kweli kweli mmmh!!,lkn si poa hivyo.
 
Kwani we ulioa wembamba au mke?,,tambua kuwa mabadiliko ni kawaida,usimwache kwa sababu hizo za kipuuzi,utakuwa wa ajabu sana katika jamii,,kwa fikra hizo potofu utaacha wengi sana.,alafu jikite katika imani yako kikamilifu,utaishinda hii mitazamo ya ovyo.
 
Huyo ni chaguo lako, sasa unataka umpe nani?. Rubbish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…