Umeanza kutumia mtandao lini? Wale wa kale tukutane hapa

Kipindi cha move za kina Rambo? Enzi hizo mtoto akifaulu na kwenda shule ya Serikali anaonekana kipanga na anaepelekwa shule ya kulipia anaonekana kizibo, sasa hivi ni kinyume chake wapi zamani arif??
 
Nimbuz, Mig33 na nakumbuka tulikuwa tunatumia VoIP kama VoIP Discount kutwanga simu za international...

Hotmail account yangu ya kwanza '99 ninayo hadi leo, nashangaa kwa nini hawa jamaa hawanipi tuzo.teeh
 
Kulikuwa na Msn chat, yahoo chat, hi5, myspace wajanja walikwepo kibao huko, hapa bongo kulikuwa na darhotwire, marafiki.com. Facebook alipokuja akauwa yote ingawa hi5 bado nipo lkn haina mvuto tena
 
hahahha umenikumbus
ha mbali sana ndugu yangu... Binafsi nimeanza kutumia migg33 hasa kwenye chat rooms za mademu na romantics rooms!! hahaha tumewasumbua sana.. enzi simu gprs sijui vile ndio inauwezo! Nokia N70, motorola bapa n.k
na enzi hizo computer tunatumia za internet cafe (moja maarufu pale fire ilikua inaitwa cyber cafe kama sijakosea)... website maarufu ya kusikiliza nyimbo za kibongo ilikua www.mzibo.net Aisee siwezi kusahau hizi moment!
 
yahoo inazunguka hadi muda wa kukaa cafe unaisha.
unauliza nini tatizo, wanasema ni network... ukiuliza network ndio nini hata mtaalam wa cafe naye kilaza. mimi nilikuwa nawaona kama wanaPHD ya IT kumbe ni masekretari tu.
Hahaha page haifunguki haha
 
Haha ndiyo mkuu yan ilikuwa fire
 
Kulikuwa na Msn chat, yahoo chat, hi5, myspace wajanja walikwepo kibao huko, hapa bongo kulikuwa na darhotwire, marafiki.com. Facebook alipokuja akauwa yote ingawa hi5 bado nipo lkn haina mvuto tena
Yes ila hizo za juzi Darhotwire
 
Baadae ikajaga mtandao mmoja unaitwa "tagged" ulipata maarufu sana kwetu miaka ya 2000-2009 hivi... ilikua una earn money amabazo hata huwezi kuzitumia physically! ila unaweza kuzinunulia pets humohumo mtandaoni... na pets wenyewe ni wachezaji wenzako.. hahahahaha
 
line ya voda ikiwa 32,000/= unapata na manual bonge la kitabu kwny pack ukasome namna ya kutumia line BUZZ(sasa Tigo) line 22,500 iko ndANI YA kasha la cd na kakitabu flani kadogo manual ya jinsi ya kutumia line bila kusahau wazee wa tritel walioibuka na mabei yao makubwaaa vilaza sana watu hadi kuwekewa mavitabu ya kusoma notes ili uelewe kuweka kline jinsi ya kupiga kutuma sms na kucheza gemu la nyoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…