Umebaini tofauti gani Uwanja wa Mkapa na Uwanja wa Samia unaotarajiwa kujengwa Arusha?

Dah! Wanachuo wa Mwaka wa kwanza 2023/2024 wanalia kwa kupewa mkopo kiasi kidogo sana almost 70% wamepewa kiasi kidogo na wengine 20% kukosa kabisa ila bajeti ya uwanja wanaiweka juu sana au ndo michezo kwanza elimu baadae🤔
 
Mimi nimebaini kitu kimoja tu hapa!! Wahuni siyo watu wazuri hata kidogo.

Kama kwenye ununuzi wa ndege ya mizigo, Mama mwenyewe alikiri hadharani wahuni waliongeza cha juu! Ndiyo washindwe kwenye huo uwanja!! Narudia tena kusema Wahuni siyo watu poa hata kidogo.
 
Hivi kwann jina la uwanja usingeitwa MANGI MELI STADIUM jina la chief wa eneo hilo tukabak tunawaenz machifu katika eneo husika la uwanja kupunguza miradi mingi kuitwa majina ya raisi wakat machifu wa maeneo husika wakienda kusahaulika kabisa
 
Ndio tofauti iwe bilioni 200?
 
Wakati mnajadili juu ya Gharama ,angalieni hivi vipengele.
1.Thamani ya shilingi ahidi ya Dola imepungua.
2.Mfumuko wa bei
3.Aina ya Sanifu
4.Eneo la Nje ya uwanja litakalofanyiwa matengenezo ni kubwa kuliko awali.
5.Matilio yatakayotumika kwenye uwanja mpya ni bora zaidi.
6.Teknolojia itakayowekwa kwenye uwanja mpya ni bora zaidi
7.Riba ya Mkopo kwa miaka hii ni kubwa kutokana na kupanda kwa Interest ya Federal Bank.

Tusiwe wepesi wa kukurupuka na kulaumu...Tafiti muhimu
 
Nilidhani utakuwa na idadi kubwa kuliko wa mkapa ,your projects do not think about future generations
 
Hata mimi kwa tathmini ninaona hio ndio thamani halisi ya 30k capacity Arena. Ingekuwa 60K ndio ingefika kwenye 100B kihaki tu.
 
Ndio tofauti iwe bilioni 200?
Inashangaza mno, hebu waza nyumba tu ya room 3 ya ukubwa wa 9×12 kama mwaka 2007 ilikuwa inakamilika kwa 40M hadi finishing, mtu akikwambia kwamba leo atakujengea nyumba nyingine mpya ya vyumba viwili ya 8×10 lakini gharama zitakuwa 160M utakubali?

Kigezo akwambie dollar imepanda sijui material na cement bei iko juu. Hivi inaingia akilini kweli hio?
 
Hivi sasa ndio watu wanapiga pesa balaa yaani inafikilisha sana imagine
Tena mfano uliotoa wewe una nafuu kumbuka uwanja wa mkapa ni mkubwa kuliko wa Arusha then Gharama zinaongezeka bilion 200😳 duuh ni pesa nyingi hata kama ni 2007 na 2024 daah watu hawana huruma na kodi zetu
 
Duuuh,na hapa umetumia akili???
Aisee
 
Si bora wale hiyo hela na uwanja ukajengwa kuliko kula hela bila mradi wowote. Kwani mnadhani hozo bilioni 200 hawawezi kuchukua bila kupitia kwenye mradi wowote? Hata wangekula bila kujenga uwanja mngewafanya nini?
 
Duh! Yani uwanja wa Benjamin Mkapa wenye capacity ya 60,000 thamani yake inaingia mara 4 na upuuzi kwenye huu uwanja wa capacity ya watu 30,000!

Haya maajabu, ngojea tuuone huo uwanja mpya!
Value ya hela miaka20 iliyopota ni ile ile ya leo? Billions 60 miaka 20.iliyopita unajua leo itakuwa kiasi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…