Umeoa halafu unamzuia binti wa watu asifanye kazi na huna uwezo wowote kifedha. Unafanya hivyo kwa faida gani na ili iweje?

Umeoa halafu unamzuia binti wa watu asifanye kazi na huna uwezo wowote kifedha. Unafanya hivyo kwa faida gani na ili iweje?

Huu uzi wako umenikumbusha kile kisa cha yule mwanariadha wa Uganda "Rebecca Cheptegei" aliyeuwawa na mpenzi wake kwa kuchomwa motošŸ”„ kisa wivu wa hela alizopata kutoka kwenye mashindano ya olimpiki ya Paris.
 
Ni kanuni mwanaume kupambana zaidi ya mwanamke
Ndio mwanaume ni mpambanaji tangu kutungwa mimba, wewe fikiria tu mimba ya mwanaume inatungwa kwa kuotea siku ya 14, mimba za wanaume zinawasumbua sana wanawake wanakuwaga na tabia za ajabu ajabu hapo utasikia mimba ya mtoto wa kiume hiyo, lazima tupambane haswa
 
Suluhu ni yeye kuonesha jitihada za kupambana,yamkini kuna wanawake wengi wanamna hiyo,lakini mwanaume huwezi kuishi kwa hofu,pia haya mambo ni tabia na ethnicity huchangia na unaa,mwanamke kuna vitu anavihitaji hawezi kumwambia mwanaume kila kitu,kama ndivyo amfungulie biashara inayoeleweka sio kumzuia,siku akipata changamoto ndani kunakuwa kama tanuri la moto lakini mwanamke akiwa na kipato inamsaidia,hawa ni backup
Asante kwa maoni yako ni mazuri.
Nimeongea na kijana anasema hivi

"Wanawake wa sahivi wamelishwa sumu inaitwa Feminism kutoka kwa wenzao wa marekani
Sumu hio Inakataza mambo ya 50 kwa 50 yaani mwanaume ndo mleta mkate hata kama mwanamke anakipato kikubwa.pesa ya mwanamke ni ya kwake sio ya familia

Sumu hio pia inasema No Man No Stress live your Best life. Mafriage has no happines

Na wasilisha mawazo ya kijana huyo
 
Hofu ya kusalitiwa na hofu ya kudharauliwa ndio humfanya mwanaume achukue uamuzi kama huo.

Of course, kwa uhalisia wa maisha ya sahivi pesa ndio kila kitu. Mwanaume lazima awe na kipato ambacho si cha kubangaiza, hasa pale unahitaji kuwa na familia ya mama na watoto.

Mimi mwanaume kiukweli huwa napenda kuwa na familia ambayo inapendeza sana kuwa na mwanamke nyumbani. Na hivo ndivo ilipaswa kuwa ukiondoa maisha yalio katika uhalisia wa leo kwamba kila mtu lazima a-fight.

Kiukweli makatazo au mazuio hayana msingi kama mwanaume haunakipato cha kukidhi kuweza kumkalisha mama ndani. Utamtengenezea tamaa na kujidharau na aone kama hafai kujiita kuwa ameolewa.

Ndio maana sometimes unakutana na bibie town unamuuliza "Umeolewa" anajibu "Ndio, lakini sio kiviile". šŸ˜„
Anashindwa kujiamini, maana aliyemuuliza atajiuliza huyo mme hana care!? šŸ˜€
 
Roho mbaya tu. Wanaogopa mwanamke akowa na kipato atakuwa na nguvu ya kusimamia haki zake.
Kwani kafungwa minyororo huyo mwanamke? akitaka si atoke kwenye ndoa akatafute maisha!

Vipaumbele katika maisha hutofautiana, ujuha ni kuamini kipaumbele chako wewe (mwanamke kufanya kazi ili muongeze kipato) kuwa ndo kipaumbele cha kila mmoja.
 
Kuna vijana mimi nawaona wa hovyo sana,utakuta kaoa mke ana Taaluma yake ,yeye maisha yake ni yakubangaiza mwenzangu na mimi kama sio zaidi ya mimi lakini anamzuia mke wake asifanye kazi kwa kuajiriwa na anakuwa mbogo,ukimuangalia mwanamke kachokaaa na Ana taaluma yake Angeweza kupambana akapata ajira mambo yakaenda ila anaishia kukaa nyumbani.

Wazazi wake walimsomesha ili iweje sasa kwa muktadha wa elimu yetu,?
Wapeni uhuru wake zenu kufanya kitu wanajisikia amani maana wanakuwaga msaada sana hawa mara nyingi ukibakiwa na buku mia mbili zako.

Unafanya hivyo kwa faida gani na ili iweje?, kama hutati afanye kazi kwa watu basi mpe biashara inayoeleweka aifanye.

Ni ushamba
Ndoa ni makubaliano, ikiwa binti ana taaluma yake na amekubali kuolewa bila ya kuwa na makubaliano na muonaji juu ya suala ya kufanya ama kutofanya kazi hilo ni kosa la binti na wazazi wake. Ikiwa utaratibu sahihi unafuatwa hili tatizo linaweza kuwa minimized kwa kiwango kikubwa sana! ... tatizo vijana wengi wanaokotana okotana tu bila ya utaratibu maalum halafu wanaanza kubebeshana malawama.

Pia nakubali kabisa kama kijana umeenda kuoa binti aliyesoma na wewe hutaki afanye kazi basi ulipaswa kuliweka wazi hilo kabla ya kuoa. Ila siamini kama mwanaume aisiyetaka mkewe afanye kazi kuwa huo ni ushamba bali ni kipaumbele chake cha kulingana vigezo vyake vya maslahi mapana ya familia yake.
 
Mwanamke hapa unamanisha anaachishwa kazi au tuwape uhuru wakatafute kazi?
 
Mwanamke hapa unamanisha anaachishwa kazi au yuwape uhuru wakatafute kazi?
kuna walio kutwa wanakazi wakaachishwa kazi waachwe warudi kazini,nakuna waliokutwa bado hawana kazi na walikuwa wapo mbioni kupata kazi ila wakazuiliwa kufanya kazi,hawa wote ni wahanga kwa mujibu wa mantiki ya chapisho yangu
 
Ndoa ni makubaliano, ikiwa binti ana taaluma yake na amekubali kuolewa bila ya kuwa na makubaliano na muonaji juu ya suala ya kufanya ama kutofanya kazi hilo ni kosa la binti na wazazi wake. Ikiwa utaratibu sahihi unafuatwa hili tatizo linaweza kuwa minimized kwa kiwango kikubwa sana! ... tatizo vijana wengi wanaokotana okotana tu bila ya utaratibu maalum halafu wanaanza kubebeshana malawama.

Pia nakubali kabisa kama kijana umeenda kuoa binti aliyesoma na wewe hutaki afanye kazi basi ulipaswa kuliweka wazi hilo kabla ya kuoa. Ila siamini kama mwanaume aisiyetaka mkewe afanye kazi kuwa huo ni ushamba bali ni kipaumbele chake cha kulingana vigezo vyake vya maslahi mapana ya familia yake.
Ni kigezo kama ana misuli ya kiuchumi hivyo Ana mtimizia mahitaji mwanamke bila shida,nje ya hapo anakosa sifa Za kuweka kigezo
 
Ni kigezo kama ana misuli ya kiuchumi hivyo Ana mtimizia mahitaji mwanamke bila shida,nje ya hapo anakosa sifa Za kuweka kigezo
Kuna wengine hata ukisema utawatimizia mahitaji yao ama utampa reasonable allowance on top ya kumtimizia mahitaji yake lakini bado wanaona wamenyimwa uhuru. Muhimu ni kukubaliana kwanza juu ya vipaumbele vyenu.

Dhana ya kuamini eti kufanya kazi ndo only way kuboresha maisha ya familia ni potofu sana, tunawaona wahindi na waarabu wengi tu wake zao wapo majumbani na bado wao ndo wanaomiliki mabiashara makubwa na kuwa na vipato vikubwa kuliko kina sie. Jambo la msingi ni nyinyi mtu mbili kukubaliana kwenye ujinga na werevu basi!
 
Back
Top Bottom