Umeona nini kwenye maziko ya yule tajiri wa Kibaniani, Patel tokea mwanzo hadi mwisho?

Covid 19 umepamba moto, kama una daktari rafiki yako mhimili muulize, tutakoma kukubali kuongozwa na washamba wapenda sifa za kijinga
 
CORONA haiitaji promo mzee.
Inajionesha yenyewe.
Covid 19 umepamba moto, kama una daktari rafiki yako mhimili muulize, tutakoma kukubali kuongozwa na washamba wapenda sifa za kijinga
 
Habari za vifo zimeongezeka ila wewe hufi?mashuleni watoto wangekua wameisha

Ifike wakati tusilazimishane kuishi kwa mapendekezo binafsi, mzee jipige lockdown wewe na family yako wala hakukuna wa kukuuliza ila usitake kutulazimisha kitu kisichopo

Kila mtanzania anakiri kwamba Corona ilikuepo ila sasa haipo sababu hawaioni mitaani na hivyo kuibuka maswali kama kweli hiyo ya zamani ilikua Corona kweli au ni tension tu!
 
Dah....waswahili tunapenda drama sie 😏😏

Kwani wewe kama wewe unawajua watu wangapi (na hapa naongelea personally sio hao maarufu ama wakuambiwa) waliokufa kwa corona??? Ndugu yzako wangapi??? Majirani je???
Mie binafsi sina nnaemjua hata mmoja.

Ila walioipata nawajua wakutosha...nikiwamo mimi binafsi, mwanangu, marafiki zangu etc. Etc....ila wote tumepona.

Kwahiyo ndio...CORONA IPO ila tuache kuikuza sana na kujazana hofu. Ukipata wahi kachukue NimrCuff. ..kama huwezi fuata ushauri wa muheshimiwa upige nyungu pamoja na madawa ya asili yanayojulikana siku zote kuwa yanasaidia unapopata mafua na kikohozi.
 
Wamarekani,waingereza wamewekeza billions of money kununua dawa ya corona. Ivi kwanini wasingetumia njia hii yakwako kutibu corona alaf hizo hela wafanyie mambo mengine ?

Kila jambo lina siri zake, hayawekwagi yote hadharani.

Wazungu wana mambo yao.

Sisi ya kwetu waafrika au waswahili ni kuwa siri utaipata shambani.
 
Hapo namba nne utawaua watu kwa ugonjwa wa moyo! Lita 3 - 4 kwa siku? Tiba asilia wanatudanganya sana! Ongeza na Dr. Mohamed Janabi akueleze matatizo ya maji mengi mwilini!
 
Hapo namba nne utawaua watu kwa ugonjwa wa moyo! Lita 3 - 4 kwa siku? Tiba asilia wanatudanganya sana! Ongeza na Dr. Mohamed Janabi akueleze matatizo ya maji mengi mwilini!

Ukinywa lita tatu hadi nne kwa siku halafu hukojoi na umekaa tuu hapo hufanyi zoezi lolote litalokutoa jasho, wala hujitaji maelezo ya Dr Janabi.... mwili utakuletea matokeo hasi tuu.

Uzuri inatakiwa wqtu wapate maarifa nini cha kufanya na kwanini unafanya hivyo. Asilimia kubwa ya kina sisi ni kusoma kukopi na kunakili bila kujiuliza matokeo yake ni yepi, hasi ama chanya...!

Na ili ujue sasa hivi mwili wako una maji mengi au umekaukiwa, utajuaje? Maarifa ndo yatakufikirisha cha kufanya kabla ya kubugia lita 2 au 3 au 1 au glasi 8.

Ukinakili ile ya kwamba mtu anywe glasi 8 kwa siku, je huyo mtu ana kilo ngapi? Mrefu ama mfupi? Wa miraba minne ama kimbaumbau, mtoto wa miaka 12 ama miaka 45 amani mzee wa miaka 78...!!!?
Hiyo ni moja tuu ya vipengele vingi vya kufanyia kazi kabla ya kuchukua hatua.

Alamsiki.
 
K.Matata kwenye ubora wake 😆😆
 
Acha umbea mungu katuepusha na korona wakala wa shetan unamiemko ya kisiasa wew
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…