Umepanga chumba kimoja unaoa ili iweje?

Umeangalia chumba tu Ila haujaangalia mambo mengine Kama kuweza kumpa mwanamke huduma zote za muhimu .


Kuna watu wamepanga vyumba viwili Ila anakula mlo mmoja yeye na mke wake pamoja na watoto.
 
Don't go back , ikiwa unafikiria kuoa in single room just do it

Make sure you live ur life to the fullest

This life is not immortal so don't complicate anything.
Maisha mkuu sio hivyo every move inabidi iwe calculated just do it zitakupeleka kwenye majuto.. kuoa sio la kukurupuka sio Leo nimepata wazo la kuoa basi haraka nakimbilia kuoa bila kuangalia nipo katika position?
 
Tusipende ubishi chumba kimoja ni kwaajiri ya mtu au watu wanaotaka kuanza maisha ila sio mtu au watu wanaotaka kuanzisha familia
Kuanzisha familia kuna haja ya kujipanga ktk suala la makazi
Watu wanapenda kuchukulia vitu simple sana mazingira mnayoishi Yana impact kubwa sana kwenye mahusiano
 
sasa yupi hakujipanga, aliyezalia kwao au yule aliyezalia kwake kwenye chumba kimoja?
Kwenye maisha yangu sikuwahi kuishi chumba kimoja na mzazi wangu yoyote nawapongeza kwa hilo
 
Mi nikajenga nikaoa afu nikaishia kupanga maisha hayana fomula
Kupanga sio tatizo kabisa ila kupanga chumba kimoja na kuishi na familia ndio tatizo kama baba wa familia inabidi upambane isitokee
 
Kwa maisha ya Mtanzania wa ile hali/mnyonge(?)siwezi kushangaa akipanga chumba kimoja anapoanza kuishi na mke.Uchumi "umebovuka"!Tukitaka wawe wamejikamilisha tutarajie waoe wakiwa na miaka 49-55.Yaani watafikia u-senior citizen ndiyo wataposa wachumba.
 
Mkuu,

Unataka kulazimisha watu waishi kwa standards zako?
 
Maisha mkuu sio hivyo every move inabidi iwe calculated just do it zitakupeleka kwenye majuto.. kuoa sio la kukurupuka sio Leo nimepata wazo la kuoa basi haraka nakimbilia kuoa bila kuangalia nipo katika position?




Maisha yapo katika level (viwango)


Kuna Ambao wanakula wanachotaka na wengine wanakula kinachopatikana


So wakati wewe ukiwa unaamini ili uoe unabidi kuwa na nyumba wengine hata sehemu ya kulala hawana.

So acha watu wajipimie

Mwanzo sio mwisho
 
Kuna wanandoa Wana watoto wanne na mwingine yupo njiani wanalala chumba kimoja.
Mtoto WA kwanza ni wakiume yupo form 3
Kuna siku nilimwambia mama mtu kama ataridhia huyo kijana awe anakaa kwetu..(kwa wazazi wangu)
Nilitukanwa ...
Mpaka Leo Hawa wanandoa Huwa siwaelewi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…