Umepanga chumba kimoja unaoa ili iweje?

Umepanga chumba kimoja unaoa ili iweje?

Umeangalia chumba tu Ila haujaangalia mambo mengine Kama kuweza kumpa mwanamke huduma zote za muhimu .

Kuna watu wamepanga vyumba viwili Ila anakula mlo mmoja yeye na mke wake pamoja na watoto.
 
Don't go back , ikiwa unafikiria kuoa in single room just do it

Make sure you live ur life to the fullest

This life is not immortal so don't complicate anything.
Maisha mkuu sio hivyo every move inabidi iwe calculated just do it zitakupeleka kwenye majuto.. kuoa sio la kukurupuka sio Leo nimepata wazo la kuoa basi haraka nakimbilia kuoa bila kuangalia nipo katika position?
 
Tusipende ubishi chumba kimoja ni kwaajiri ya mtu au watu wanaotaka kuanza maisha ila sio mtu au watu wanaotaka kuanzisha familia
Kuanzisha familia kuna haja ya kujipanga ktk suala la makazi
Watu wanapenda kuchukulia vitu simple sana mazingira mnayoishi Yana impact kubwa sana kwenye mahusiano
 
sasa yupi hakujipanga, aliyezalia kwao au yule aliyezalia kwake kwenye chumba kimoja?
Kwenye maisha yangu sikuwahi kuishi chumba kimoja na mzazi wangu yoyote nawapongeza kwa hilo
 
Mi nikajenga nikaoa afu nikaishia kupanga maisha hayana fomula
Kupanga sio tatizo kabisa ila kupanga chumba kimoja na kuishi na familia ndio tatizo kama baba wa familia inabidi upambane isitokee
 
Kuna baadhi ya vitu ukikaa ukawaza unaona kabisa ni kama tunaforce kufanya jambo kwa wakati usio sahihi mfano mzuri ni watu kuamua kuanzisha familia kwenye chumba kimoja.

Ni maisha ya aibu fikiria umetembelewa na rafiki, ndugu hata wakwe unawakaribisha wapi? Chumba kimoja umeweka kitanda, vyombo, ndoo za maji, mabegi yenu ya nguo, sofa, jiko kimsingi chumba kimejaa ingekuwa kwa mkapa wanasema full house.

Vipi kuhusu privacy yenu mkibarikiwa kuwa na mtoto hapo mbeleni utabadilisha vipi nguo? Mtashiriki vipi tendo la ndoa?

Conclusion Mwanaume unayeoa kwenye chumba kimoja ni wazi hujajipanga financially umeruhusu kuongozwa na matamanio ya kuoa tu huna plans.
Kwa maisha ya Mtanzania wa ile hali/mnyonge(?)siwezi kushangaa akipanga chumba kimoja anapoanza kuishi na mke.Uchumi "umebovuka"!Tukitaka wawe wamejikamilisha tutarajie waoe wakiwa na miaka 49-55.Yaani watafikia u-senior citizen ndiyo wataposa wachumba.
 
Kuna baadhi ya vitu ukikaa ukawaza unaona kabisa ni kama tunaforce kufanya jambo kwa wakati usio sahihi mfano mzuri ni watu kuamua kuanzisha familia kwenye chumba kimoja.

Ni maisha ya aibu fikiria umetembelewa na rafiki, ndugu hata wakwe unawakaribisha wapi? Chumba kimoja umeweka kitanda, vyombo, ndoo za maji, mabegi yenu ya nguo, sofa, jiko kimsingi chumba kimejaa ingekuwa kwa mkapa wanasema full house.

Vipi kuhusu privacy yenu mkibarikiwa kuwa na mtoto hapo mbeleni utabadilisha vipi nguo? Mtashiriki vipi tendo la ndoa?

Conclusion Mwanaume unayeoa kwenye chumba kimoja ni wazi hujajipanga financially umeruhusu kuongozwa na matamanio ya kuoa tu huna plans.
Mkuu,

Unataka kulazimisha watu waishi kwa standards zako?
 
Maisha mkuu sio hivyo every move inabidi iwe calculated just do it zitakupeleka kwenye majuto.. kuoa sio la kukurupuka sio Leo nimepata wazo la kuoa basi haraka nakimbilia kuoa bila kuangalia nipo katika position?

Maisha yapo katika level (viwango)

Kuna Ambao wanakula wanachotaka na wengine wanakula kinachopatikana

So wakati wewe ukiwa unaamini ili uoe unabidi kuwa na nyumba wengine hata sehemu ya kulala hawana.

So acha watu wajipimie

Mwanzo sio mwisho
 
Kuna wanandoa Wana watoto wanne na mwingine yupo njiani wanalala chumba kimoja.
Mtoto WA kwanza ni wakiume yupo form 3
Kuna siku nilimwambia mama mtu kama ataridhia huyo kijana awe anakaa kwetu..(kwa wazazi wangu)
Nilitukanwa ...
Mpaka Leo Hawa wanandoa Huwa siwaelewi...
 
Back
Top Bottom