Umepigwa na kijana mdogo aibu imekupata - Mbaraka Mwinshehe, kama anamwimbia Putin!

Kuna Mtu alinijaza eti huu wimbo ni dongo kwa JUMA KILAZA wa pale Morogoro mtaa wa FIRE wkt huo Mbaraka anakaa Nunge!
Ila kwa upande mwengine hii stori ilitokea kweli pale Morogoro kwenye hiyo miaka ya Sabini.
 
Mkuu Elungata hii ni kweli. NATO hawataki Ukraine wapige ndani ya Urusi, na wanajua wakiwapa hizo silaha za masafa marefu nao wataanza kupiga ndani ya Urusi. Ndio maana hadi leo Mrusi akilipuliwa ndani Ukraine hawasemi ni wao kwa kuwa wamekatazwa.

Kuna wakati walitaka kumuua General wa Urusi Marekani wakasema msifanye hivyo.
 
Okay, western media inasema Urusi wamerudishwa nyuma na wameachia maeneo baada ya kipigo. Vyombo vya Urusi vinasemaje, karibu Urusi wanateka Kiev?

Anyway, mie niko zaidi Aljazira. Au nao ni westerm mededia?
Sasa Aljazira ndo source yako, hao hawapatan na warusi !!.

Habari zao zote ni ,kumponda mrusi
 
Kama vipi mataifa yenye nguvu za kijeshi yaache kuipa silaha na fedha ukraine. Zelensk atakimbia nchi, hana uwezo wa kupambana na urusi.
Vita ni pamoja na uwezo wa kiongozi wa nchi ku-organize misaada ya kijeshi. Hata Uingereza bila Marekani angepigwa na Hitler. Sasa huwezi kumlaumu Mwingereza eti hakuwa fair kwenye WW2 kwa sababu alisaidiwa na USA, wewe una theory za namna gani? Unataka usawa kwenye vita mura?

Hata sisi tulipompiga Idd Amin tulisaidiwa silaha. Kwa hiyo ulitaka tusisaidiwe ili vita na Uganda iwe fair?

Msumbiji tuliwasaidia silaha na askari Wareno wakaona hawawezi kuendelea kuhimili.

Vita ni vita mura kama huwezi usivamie jirani zako, kama huwezi kura ukarare, sio unapigwa unararamika!
 
Putin hapigani na zelensk pekee, anapigana na mataifa mengi ndani ya ukraine. Isingekuwa mataifa hayo yenye nguvu za kijeshi ukraine ingeshatekwa siku nyingi isingefika miezi kumi tangu vita kuanza
Hivi Ukrain anavyopewa vifurushi vya misaada na baadhi ya mataifa ya magaribi ndio kumaanisha Urusi anapigana na NATO?! Pro Putins' ideology msitafute mgongo wa kupumulia, anayewanyoosha ni Zelensky na jeshi lake tiifu.
 
Putin hapigani na zelensk pekee, anapigana na mataifa mengi ndani ya ukraine. Isingekuwa mataifa hayo yenye nguvu za kijeshi ukraine ingeshatekwa siku nyingi isingefika miezi kumi tangu vita kuanza
Tuko tayari kutaja nchi zinazoisaidia Ukraine, ila hatuko tayari kutaja nchi zinazoisaidia Urusi. Kwanza hata vita vyenyewe alishambulia kutokea Belarus.
 
Wewe na akili zako unaamini Ujerumani imebakia na vifaru 50?
 
Labda sio marekani hii tuijuayo, marekani ya kihiroshima.
 
Na kama isingekuwa ATO kumkataza, Urusi sasa hivi angekuwa anapata kichapo ndani ya Urusi. Ni kwa vile tu NATO wanamwambia Ukraine ukianza kumchapa ndani ya Urusi tutasimamisha misaada ya silaha.


Hapo ndipo Ukraine angalijua Russia ni nani na uwezo wake wa silaha zake za siri ukoje, Ukraine ingangamizwa pakubwa, NATO wanalijua hilo, hofu ya NATO ni kwamba vita ya dunia ingeanzia hapo.--- Mrusi hadi sasa hataki kutumia silaha zake tegemezi.
 
Kwa hiyo huyo "Bwana mdogo Ukraine" kashinda ama???


Hakuna hajashinda, bado anatandikwa huku anapiga yowe kama fisi aliyeng'atwa na Simba, anazidi kuomba msaada wa fedha na silaha kutoka US--- ni mashabiki ndio wanaompigia debe la ushindi.🤣🤣
 

Ujerumani anabakije na vifaru 50 wakati hajapeleka kifaru hata kimoja Ukraine?!

Huko Ukraine hakuna silaha ya maana iliyopelekwa,hata ATACMS hazijaenda,long range missiles hawajapeleka,sasa kaangalie long range missiles ambazo NATO wanazo!!!
 
Poland naye vifaru vyake Vingi vimepotezwa huko Ukraine juzi wameagiza vifaru huko Korea kusini ujerumani ndo hali mbaya kabisa na uwezo wa kufanya mass production ya silaha hana
 
Poland naye vifaru vyake Vingi vimepotezwa huko Ukraine juzi wameagiza vifaru huko Korea kusini ujerumani ndo hali mbaya kabisa na uwezo wa kufanya mass production ya silaha hana
Poland alitoa vifaru vyake vya zamani aina ya T-72 sababu alikua kashaangiza vifaru vipya 200 vya Abraham toka Marekani pia wameorder toka South Korea vifaru 1000 vipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…