Umepitia/Unapitia changamoto gani tangu umalize chuo mpaka sasa?

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
262
Reaction score
577
Kama binadaamu kuna wakati mtu unapitia magumu mpaka hujui nani wa kukusaidia hata kimawazo.

Leo nimeanzisha thread hii ili tushare mambo au changamoto mbalimbali ambazo tunapitia sisi viumbe wa Mungu.

Orodhesha changamoto na jinsi ulivofanikiwa kutatua ili umsaidie mtu mwingine huko aliko.
1. Changamoto ya ajira.

2. Changamoto ya mapenzi.

3. Changamoto ya biashara au maisha kiujumla
 
Let's pray to God but things are not easy.
 
Kiufupi changamoto ninayopitia kipindi hiki ni biashara zangu kama leo sijauza kabisa kuhusu mapenzi nimejiweka kando kidogo nifocus na maisha japo hali ngumu ajira nazo ngumu kuna sehemu nilikuwa najitolea ila hali ikawa ngumu nimeacha ila now nafanya biashara
 
Napitia changamoto nyingi tu sometimes nakua na depression na sijui kwa jinsi gani naweza kupona mfano lwa sasa nina stress za biashara mf wateja wamekua wachche skuiz
Pole kwa changamoto unazopitia.

Depression na stress ni hali za kawaida za kihisia hasa unapokabiliwa na changamoto fulani, ila waweza jiweka sawa kwa:

- Kufanya mazoezi ya mwili kama kutembea au kukimbia

- Kupata usingizi wa kutosha wa angalau masaa saba kwa siku: Na tambua kuwa usingizi bora huandaliwa ( kula mapema angalau iwe masaa 2 kabla ya ule muda wako wa kulala, punguza au acha matumizi ya kahawa hasa wakati wa jioni.
 
Nilikosa kibarua nkawa sina hata geto naishi porini, baadae kwa ugumu sana nkaja kupata kichumba yaan kijistoo cealing board hakuna upande wa pili choo. Watu wana sifa akiwa anakunya unamsikia anahema na kujamba kana kwamba amekula mbigili, alafu harufu kali kichizi. Nilkua nakereka sana. Alhamdulillah nilivuka.
 
Mtumie kitabu chako Cha low of Attraction, I read and I got some concept
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…