Umepitia/Unapitia changamoto gani tangu umalize chuo mpaka sasa?

Huu uzi ni kwa wavyuoni tu. Sie wa la 7B tutasoma comments tu
 
Komaa mkuu umalizie na Mungu akusaidie baada ya kumaliza iyo MBA akupe chimbo la asali.
 
Unadaiwa sh ngapi? Na mtu akitaka kukusaidia akutumie kwenye namba gani? Maana unakuta kuna mtu anatamani akusaidie
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mbigili ni nini mkuu
 
Nina mashaka na afya yako ya akili
 
Daah maisha ni magumu xannaaa especially ukikosa kazi kulingana na proffesional yako....aaah ni hatari na ni ngumu kuelezea mpaka yakukute...
 
Pia changamoto nyingine kwa sasa nina 27 years ninaona nmechelewa wenzangu wana kazi nzuri wana magari wanapost wanaenda sehem nzuri wanavaa nguo nzuri mi narudia rudia tu nguo
Katika maisha hakikisha haujilinganishi na mtu mwingine utaumia sana, bali jilinganishe wewe mwenyewe. Hakikisha wewe wa jana sio wewe wa leo, na wewe wa leo usiwe tena hivyo kesho
 
Pia changamoto nyingine kwa sasa nina 27 years ninaona nmechelewa wenzangu wana kazi nzuri wana magari wanapost wanaenda sehem nzuri wanavaa nguo nzuri mi narudia rudia tu nguo
ishi maisha yako maisha ya kwenye picha yasikuumize kichwa, kuna unapofikia na uinjoi
 
Maisha ni Vita
Watu tumeshindia chungwa na chai sometime unakamata mende unapika unakula kama mboga.
 
Pia changamoto nyingine kwa sasa nina 27 years ninaona nmechelewa wenzangu wana kazi nzuri wana magari wanapost wanaenda sehem nzuri wanavaa nguo nzuri mi narudia rudia tu nguo
Funny but not funny

Hamna kitu kibaya kama kujilinganisha na mwingine kwenye haya maisha.
Jitahidi kuishi maisha yako na kushukuru kwa kile unachokipata huku ukiendelea kupambana kufika kule unakopataka.
 
Unasoma badaa uwekeze kwenye biashara unazingua
 
Pia changamoto nyingine kwa sasa nina 27 years ninaona nmechelewa wenzangu wana kazi nzuri wana magari wanapost wanaenda sehem nzuri wanavaa nguo nzuri mi narudia rudia tu nguo

Tatizo liko hapa mzee wangu, vijana wengi tunateseka hapa kufanya comparison za kimaisha na washikaji, marafiki tuliosoma nao pamoja. Ili uweze kujijenga zaidi na uweze kupiga hatua kwenye harakati za maisha ni lazima ujilinganishe wewe wa sasa na wewe wa jana hapo ndio turning point ya kukua.
 
Nna miaka 27, sina lolote la kimaisha. Nakaa kwa shangazi na sina kazi ila kuna mahali najitolea miaka miwili sasa hvy angalau chochote kidogo nakipata japokuwa hakiwezi kunifikisha mahali

Usikate tamaa vumilia Wakat wa Mungu ni sahihi
 
Nna miaka 27, sina lolote la kimaisha. Nakaa kwa shangazi na sina kazi ila kuna mahali najitolea miaka miwili sasa hvy angalau chochote kidogo nakipata japokuwa hakiwezi kunifikisha mahali
Mkuu !Pole sana kwa unayopitia kwa sasa.

Kwanza, naomba nikwambie jambo moja USIKATE TAMAA, maisha hayana kuchelewa wala kuwahi, nakwambia siku yako ikifika basi na mambo yako yatanyooka vizuri tu.

SIKILIZA KISA CHANGU

Mwaka 2018 nilikua na miaka 27 kama wewe, na nilikua nimejitolea katika shirika moja na posho yangu kwa mwezi nilikua napewa 42,000/= ( Elfu Arobaini na Mbili tu). Na hii nilikua napewa kama pesa ya sabuni tu lakini uhalisia nilikua ninafanya kazi bure.

Kiukweli kama binadamu na pia kijana wa kiume nilikua napitia wakati mgumu sana, nilikua naona kila kitu kiko against na mm, nilikua na stress sana..ilifika kipindi hata mademu walikua hawanitaki bro[emoji1][emoji1], nilijiona ni mtu mwenye mikosi kwani nilikua nikijaribu kujilinganisha na wana niliosoma nao, nilikua naona wameniacha mbali sana kiuchumi na hata kifamilia(Kosa kubwa sana kujilinganisha na watu).

Lakini broo huwezi amini ilipofika mwaka 2020 milango yangu ya kiuchumi ilifunguka, nikapata kazi ambayo iliniwezesha kuendesha maisha yangu na nikawa na uhakika wa kuingiza 4M kila mwezi, wale niliokua najilinganisha nao nikagundua sikuwa sahihi kwani hata maisha yao ni yakawaida sana, lakini pianilikua najiona nimechelewa kimaisha lakin kumbe nilikua pazuri tu na wala sijachelewa.

Bro USIKATE TAMAA....MAISHA NI KUPAMBANA NA MUDA WAKO UTAFIKA ONE DAY

KUWA STRONG MZEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…