Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Ukishindwa kufanikiwa Dar basi hakuna sehemu utayoweza kufanikiwa. Huu mji hauhitaji nguvu nyingi bali ni akili tu uweze kupata pesa za kusurvive. Ukiangalia kwa umakini Dar imejaa wageni wengi kutoka nje ya nchi wapo hapa kutafuta maisha ukienda nchi zingine ukiwaambia habari za Dar wanakuambia Dar kuzuri sana hasa kwenye utafutaji. Huu mji unafursa kwa kijana anayeanza maisha.

Shida inakuja apa, vijana wengi kuendeleza starehe na wanawake kwenye huu mji ndio maana unakuta wengi wao wana maisha magumu hawafikirii kesho yao unakuta siku zinakwenda kijana hata kujenga anashindwa na kipato anapata freshj shida ni kuendeleza starehe na wanawake maana huu mji unavishawishi vingi sana usipokuwa makini lazima ufeli lakini kwa kijana mwenye malengo huu mji utamfaa katika harakati za utafutaji kikubwa akae mbali na starehe na wanawake
 
Pia vijana wengi wa huku Dar ni wavivu sana kwenye kujishughulisha, wengi wao wanakesha kutwa nzima kwenye vibanda vya kubeti mipira na hata kwenye mitandao ya kijamii na wanaridhika na maisha wanayoishi.

Image kijana yuko tayari alale na njaa ili anunue bando au abeti vijana wa Dar wanashindwa kushughulisha ubongo wao ni wavivu haswaa
 
Hili umwa umwa limemtoka mtu.
 
Huruma sana.
Boda kila unayemuhoji ni mgeni kutoka mkoa X,z, n.k
Yaani utafute nauli uje dar kuwa bodaboda
Inasikitisha
 
Huruma sana.
Boda kila unayemuhoji ni mgeni kutoka mkoa X,z, n.k
Yaani utafute nauli uje dar kuwa bodaboda
Inasikitisha
Mimi huwa nashindwa kuelewa halafu utakuta anakuja jijini kuishi maisha magumu kula ya taabu halafu kijijini kwao vyakula vya kutosha na biashara za mazao ni uhakika
 
Maisha ni zaidi ya kula
Soma vizuri nimesema walipotoka kuna biashara ya mazao pia.

Huku mjini wanaishia kuishi maisha ya kupanga kachumba kamoja kama stoo au unakuta geto moja wanashare hata watu 3

Mwisho wa siku kajitahidi sana atajenga kachumba kamoja au kachumba na sebule mabondeni au uswahilini kwao kaacha ardhi nzuri na kubwa ya kutosha kujenga na kuwa na compound hata ya kuweka mifugo na bustani

Kuliko kuwa house boy, boda au machinga huku Dar bora uwe mkulima inalipa kwa mbali sana

Pesa wameicha walipotoka.
 
Kalime wewe kama rahisi
 
Kuna MTU alisema DSM pachafu, joto Kali nikamuuliza ulifikia wapi?
Akasema Keko Machungwa alikuja kwenye interview na alikaa siku 4 tu. Alipokuja awamu nyingine nilimtembeza mitaa ya mikocheni ya chini kwa nyerere kupitia mbezi beach ya chini hadi kwa Lipumba kutokea line polisi hadi Ununio kwenda kwenye Nyumba za Lugumi hadi kwa Mh. Rais. Tunapoongea sasa amepata kazi mkoa lakini akipita wiki tatu simu anakuja DSM nimpeleke viwanja
 
Mimi niko Dar mwaka wa 8 sasa ni government employee . Sasa unataka niache kazi ya uhakika nikalime?
Nikitaka kulima huwa nalima mazao ya msimu Njombe viazi mviringo.
Nyie watu mlioajiriwa huwa na kiburi na dharau sana.
Kwa mtu ambaye anatafuta maisha ili atoboe sikushauri uende Lindi, Mtwara,Tabora na Shinyanga mjini. Itakula kwako
 
Ushauri mzuri sana ila shida wanaotoa ushauri wengi wameajiriwa.
Mtu ameajiriwa, hata kuacha kazi ajiajiri hataki ila yy anataka watu wakajiajiri kwenye kilimo.
Cha ajabu akifukuzwa kazi, anaomba kazi ila fursa km hiz hazitaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…