Umeshakutana na shida gani kwenye gari lako upewe suluhisho?

Ilinitokea
Gari kila nikikunja kona hadi mwisho (kulia) inajizima. Naiwasha inawaka naendelea na safari.
Baadaye ikaacha, lakini hadi leo sijui tatizo
 
Gari kutoa moshi mweupe, ilipinduka matairi juu, hakuna leakage kwenye engine, naambiwa oil ilingia kwenye exszost ndo mana inaunguza oil je ni sahihi?
Mie ya kwangu ililala hvo hvo ila ikaanza kunisumbua inamisi hovyo na kupandisha oil kwenye plug. Ikabidi mpaka niifunge ring piston tu.
 
Ahsante mkuu
 
Samahani mkuu ni gari gani kama hutojali
 
Suzuki Escudo engine G 16 automatic transmission ikitembea inakuwa kama ipo free mafundi huku kjijini wanasema ni tatizo la gearbox utatuzi wengine wanasema nifunge gearbox nyingine wengine wanasema kuwa ndani ya gearbox huwa kuna plates za kubadili tu nipo kijijini sijui kipi ni sahihi
 
Fafanua vizuri ikitembea inakuwa free, yaani, gear haziingii au wewe ndiye unayehisi kama gear hazi-engage?
 
Hii ni gari gani inatetema hivyo kama mayele?
Mkuu angalia balance ya upepo pia. Kama moja ya tyre ina pressure kubwa kuliko nyingine hilo tatizo haliepukiki.
Mimi nimekosa muda wa kuziba moja ya tyre langu hilo tatizo nakutana nalo kila baada ya siku tatu. Nikibalance upepo natembea vema kabisa kama niko na Range.
 
Gari kutoa moshi mweupe, ilipinduka matairi juu, hakuna leakage kwenye engine, naambiwa oil ilingia kwenye exszost ndo mana inaunguza oil je ni sahihi?
Gari kutoa moshi mweupe hapo kuna gasket zinavuja oil inachanganyikana na mafuta. Au coolant inavuja. Au fuel injector imekufa hivo kupelekea gari kutumia mafuta mengi kwa umbali mdogo.
 
Premio Automatic Gia D inazingua ukiwa speed ndogo gar inapunguza speed,Gia L na 2 gar inaenda vizur
 
Gari kustuka unapoweka gear river, na pia inawaka taa ya over driver na kulalamika kubadili gear. Hii inasababishwa na nini???
 
Hadi leo hajakujibu hii😁😁😁
 

Gari la bro wangu likiwa kwenye speed linatetemeka amelipeleka kwa mafundi tofauti but wote wamechemka wa mwisho alimuambia achange tire kachange lakini tatizo bado lipo, shauri chochote mkuu.
 
Gari la bro wangu likiwa kwenye speed linatetemeka amelipeleka kwa mafundi tofauti but wote wamechemka wa mwisho alimuambia achange tire kachange lakini tatizo bado lipo, shauri chochote mkuu.
Hahahahah mkuu gari inatetemeka ana hakika bearing ziko sawa pamoja na mountings? Kama viko byee basi afanye mpango wa wheel balance. Isipofaa hapo acheki mfumo mzima wa uchomaji kuanzia air filter, fuel filter, nozzle, oxygen sensor, plugs n.k.

Hakika atapata suluhu katika hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…