Umeshawahi kujiuliza Msichana wenu wa kazi 'wa Miaka hiyo' yuko wapi?

Umeshawahi kujiuliza Msichana wenu wa kazi 'wa Miaka hiyo' yuko wapi?

Mimi nakumbuka hatukuwa na msichana wa kazi, bali kulikuwa na Yaya Maza Mmoja miaka ya 2000-2010 alikuwa mwamba.Yaani zile familia kuishi wengi,halafu vijana madume ndiyo wengi.Kila siku debe moja la unga linakatika (mchana na jioni).Legend kabisa yule Mama.Sema wauni wakamdanganya akasepa zake sijui hata yupo wapi.Kingine alizalishwaga Alitoa kibinti cute kabisaaa,,,,Yaani mpaka raia wakawa wanajiuliza mbegu ya wapi hii au kaiba mtoto kwa Mkunga,,,,,
 
Duh debe Kwa siku linaisha?
 
Aisee umenikumbusha majuzi.kuna mkoa nilienda vijijini ndanindani ambako hata sijawahi kufika toka nizaliwe.
Wakati natembeatembea njiani nikashangaa naitwa jina langu na mmama mmoja hivi,mara ya kwanza sikugeuka nikajua labda anamuita mtu mwingine,akaita tena nikasema majina yanafana tu,akaita mara ya tatu nikageuka.kumuangalia akawa ana furaha,uso wa mshangao kwa pamoja!
Akaniambia najua unashangaa sana nimekujuaje,hata mimi nashangaa pia kumbukumbu yangu iko vizuri kiasi gani,namshangaa Mungu kwakweli kunikumbusha hivi...mimi naitwa flani,niliwahi kua mlezi wako mkoa flani zamani sana ukiwa na umri wa miezi hadi miaka ipatayo 6.
Nilishangaa mno mno maana ni miaka 35 imepita na bado ananikumbuka kama jana!
Tulibadilishana namba,tukaongea mengi sana.

Ni moja ya matukio yaliyonishangaza sana maishani!
Utakuja kutapeliwa
 
Back
Top Bottom